Simply, mimi huandaa samaki wangu ambao ni fillet tupu na kuwakata vipande vyembamba vyembamba kama vidole. Then naweka spice yoyote nayopenda kwa wakati huo.
Then naandaa coat yake ambayo ntatumia breadcrumbs, na yai, kwenye yai nachukua only white egg part (naacha egg yolk). yolk ina tabia ya "kukakamaza" ganda la chakula husika. kwenye hili pishi mimi situmii unga wa ngano, huwa nataka coat iwe nyepesi.
Baada hapo nafanya zile process kama za kuchoma kachori au eggchop, yaani kuchukua kipande cha samaki kudumbukiza kwenye yai then kukiweka kwenye breadcrumbs, vipande vyote vya samaki vikishapitia hii process then napasha mafuta moto ready kwa kudeep fry.
Uwiii sijui nimeeleweka? kuelekeza upishi ni kipaji ati!