madindigwa
JF-Expert Member
- Aug 30, 2017
- 2,498
- 2,925
Wakuu habari zenu, binafsi mi mzima wa afya njema kabisa namshukuru Mungu, muumba wa mbingu na nchi.
Imekua ni ngumu sana kwa sisi binaadam kuombana msamaha, au kusameheana,au kusamehe, pasipo kuomba msamaha. Msamaha unashinda sukari na maziwa kwa utamu.
Wengine huthubutu hata kusema kuomba msamaha ni kujidhalilisha; hicho ni kiburi tujifunze kuomba msamaha hasa tunapokoseana. Msamaha huleta amani ndani ya nyumba, kwenye jamiii zilotuzunguka.\
Binafsi napenda sana kuomba msamaha hata kama nahisi sijakosea ila panapo tokea mvurugano wowote huwa sioni tabu kujishusha ili yaishe, msamaha ni silaha tosha kuliko hata AK47.
Tujifunze kuomba msamaha kwa wapenzi wetu/wazazi/marafiki/ndugu/majirani hata kama hawapo hai.
Binafsi nawaomba wazazi wangu msamaha kama niliwakosea huko waliko.
Mama yangu alitangulia mbele ya haki nikiwa kijana ndogo sana wa darasa la nne. Mungu amlaze mahala pema peponi. Nisamehe mama kwa lolote nililokukosea.
Mzee wangu nae ametangulia nikiwa mtu mzima na familia sikufanikiwa kumzika ila nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kumuuguza, Mungu amlaze mahala pema peponi. Mnisamehe wazazi wangu.
Omba msamaha kama kuna member yoyote umemkosea usione haya au soni ni hayo tu wakuu tujifunze kuombana msamaha.
Sent using Jamii Forums mobile app

Kobalt Music Publishing Ltd.