mzalendo iq1
JF-Expert Member
- Mar 10, 2020
- 1,257
- 1,543
UPDATE: Fuatilia hapa > LIVE - Hotuba ya Tundu Lissu - Juni 08, 2020
Leo Tundu Lissu kasema anaongea na taifa la Tanzania kupitia Facebook.
Naweza kusema CHADEMA wanaendelea kujizika wenyewe na kupoteza ushawishi hata kwa mabeberu walioahidi kuwasaidia.
Unatangaza kulihutubia Taifa letu kubwa lenye watu zaidi ya milioni 50 kwa kupitia Facebook ambayo moja kwa moja itaonyesha ni wangapi wanaokufatilia, vipi wasikilizaji wasipofika hata Mia 5 utaendelea kuwaambia mabeberu wakuamini kwani unakubalika Tanzania au itakuwa aibu na fedheha.
Huwezi kusema unalihutubia Taifa Facebook kweli CHADEMA unajua huwa mnafanya vitu mpaka nahisi CCM huenda imewaroga maana hamfikirii nje ya box. Zitto na uongo wake wote hawezi fanya huu ujinga.
Mfano wakikufatilia watanzania Mia 3 hao ndiyo litakuwa Taifa ulilolihutubia?
Mimi ningewashauri ratiba ya leo muache ni bora hata angekuwa Tanzania akahutubia kwenye chombo Cha habari kikubwa ila siyo nje ya nchi tena Facebook halafu unasema unaliutubia Taifa.
Au Kama mnaweza ni bora akaandika hotuba yake halafu mmoja wao kati yao akapewa aisomee kwa niaba yake. Hiyo italeta maana kidogo ila kuja kuanza kusema unahutubia Taifa Facebook ni ujinga.
Pia sitaki kumhoji analiutubia Taifa kama nani ila ningependa nimkumbushe anaowaomba Urais ni watanzania sio wazungu so atuheshimu asiombe uongozi Kama uchumba kwa kuweza kumtumia mtu bila yeye kuwepo.
Kama kweli ana nia aje nyumbani kupambana sio mwili upo kwingine akili ipo kwingine.