Uzi maalumu kwa waliobahatika kupata scholarship na wanaotafuta scholarship.

jf user

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
777
622
Nimeona nifungue huu uzi ili tupeane maujanja ya kupata scholarship nje na ndani ya nchi.
Scholarship hutolewa kwa namna mbili-
1/Full scholarship
- Hii mwanafunzi hulipiwa miaka yake yote ya masomo kuanzia ada, hostel, matibabu, nauli na gharama nyingine.
2/Partial scholarship
-Hii mwanafunzi huchangiwa baadhi tuu ya mahitaji yake kwa mfano ada tuu, hostel au mwaka wa kwanza anapewa yote halafu mwaka unaofuata analipa mwenyewe.

Namna ya kuomba/kuapply.
1/Bure
-Matangazo hutangazwa na vyombo vya habari kama magazeti, TV, mitandao ya kijamii na itandao ya vyuo husika. Hapa unachotakiwa ni kuweka mahitaji wanayotaka tuu mfano vyeti vyako vya form four, six, certificate, diploma na degree, vyeti vya kuzaliwa utaifa, mawasiliano, n.k kama utakidhi matakwa yao utapigiwa au kutaarifiwa kwa email.

2/Kulipia
-Hapa hutoa kiasi Fulani cha pesa ili upate form ya kuapply au kama utatumia agent utamlipa commission Fulani ili akufanikishie. Njia hii ina matatizo lukuki kwani ni kama kubet! unaweza upate au usipate kwa hiyo pesa yako inakua hatarini kupotea.

Hivyo ndivyo navyofahamu wakuu sio mbaya tukabadilishana mawili matatu tupeane uzoefu na wale wadogo zeu i hope watapati kitu.

Kwa kuanzia utatupa uzoefu wako ulipataje zali, itafaa utupe links na contact za wahusika tutafute bahati yetu na sisi.
 
Hapa mimi siwezi kukupa uzoefu wowote maana kila kitu nilitafuniwa. Hadi form nilipewa na kuijaza nilikuwa naelekezwa tu.
Yaani kazi yangu ilikuwa kupiga kitabu tu.
 
Back
Top Bottom