Uzi maalumu kwa sehemu mpya zinazofaa kuanza Maisha au kufanya biashara

stoneblock

Senior Member
Feb 28, 2023
128
357
Habari za asubuhi waungwana katika pita pita zangu nlipata wasaa wa kutembea sehemu mbali mbali sehemu ambazo nimeona mtu yeyote anaweza kwenda kufanya biashara na kutoka kimaisha kwa urahisi
leo naomba niongelee maeneo mawili

Mombo
Halmashauri ya mji mdogo wa Mombo upo wilaya ya Korogwe mkoa wa Tanga
aina ya makabila yanayoish hapo ni Wasambaa na wazigua na makabila meengi yaliyokuja kipindi cha mashamba ya katani
Mombo ni rahisi kufanya biashara yyte hata ya kuuza maji kwakua ndio njia kuu ya mabasi pia kuna mashamba makubwa ya mpunga na mazao mengine kwahiyo vibarua hata vya kupalilia mazao au kupanda vipo

Vyumba vya kuishi ni bei rahisi sana 15 tshs na kuendelea kama una mtaji wa kuhitaji frame zinaanzia elfu 50-150
biashara Mombo zinafanyika masaa 24 niwewe tu na pumzi yako


NJIAPANDA YA HIMO

Kata ya Njiapanda ya Himo ipo wilaya ya Moshi Vijijini shughuli unazoweza kufanya hapo ni biashara na kilimo kama ilivyo Kwa Mombo Njiapanda ni sehemu unayoweza kufanya biashara au vibarua na ukaweza kujitegemea

vyumba vya kuishi vinaanzia sh 20000-50000 vyumba vya biashara vinaanzia 100000-250000 biashara zote zinaweza kufanyika masaa 24 kama ilivyo kwa Mombo

kama unajua mahali wengine wanaweza kupambana na kutoka kimaisha share na wenzako ili tufanikiwe pamoja kumbuka

HUWEZI KUFANIKIWA SEHEMU ULIYOZALIWA KAMA UNATAKA KUFANIKIWA NENDA MBALI KABISA SEHEMU AMBAYO HAKUNA MTU ANAYEKUJUA
 
Asante, kutokaa sehemu uliyozaliwa upo sahihi kabisa.

Nilitaka nisome bible kabda sijatoka,ila hili ni "Neno" langu la Leo.

Upo sahihi,Ubarikiwe!
 
Back
Top Bottom