Uwe Mkulima au Usiwe Mkulima.
Fahamu hapa kua lazima kama ni biashara ufuate utaratibu mahsusi ili ufanye biashara,
Haiwezekani malori yatoke Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya yaingie hadi mashambani, wanunue mazao yote halafu baadae vyakula vipande watu waanze kulia haiwezekani.
Hakuna usalama wa nchi kama hakuna chakula haipo hiyo,
Mkulima Beba mahindi kauze NFRA kwa bei nzuri piga pesa tulia.
Mfanyabiashara, fanya yafuatayo ufanye biashara.
1.sajili kampuni
2.nenda TRA ukadiriwe mapato
3. Watakupatia TIN yako utambulike
4. TRA watakukadiria kodi lipa kodi yako pata tax clearance
5. Nenda halmashauri nako utalipia gharama za leseni ya kusafirisha mazao hapo umekamilika
6.Tafuta kibali cha kuexport mazao wizara ya kilimo ambapo ni chini ya masaa 24 unapata
Hapo unakua na ruksa kusafirisha mazao yako nje ya nchi.
Na baada ya hayo yote iwe marufuku kwenda mashambani, kwa mkulima kununua mazao unachotakiwa kufanya ni kuenda kwenye maghala ya Taifa ambayo yatakua verified unaweza kununua au kwenye vituo vilivyoidhinishwa na serikali.
Faida kubwa serikali itaweza kufahamu kiasi gani kiuzwe nje na kiasi gani kibakie ndani kwa usalama wa chakula na nchi itakua stable.
Haiwezekani nchi iwe shamba la bibi yaani kila mmoja aingie kujichotea atakavyo.
HONGERA Waziri Bashe, hatimaye umeyasikiliza maoni yetu tulio wengi.