Uzi Maalumu kwa ajili ya kukosoa Media za Tz (Hususani Runinga na Redio).

zootopia

Member
May 29, 2016
74
76
Habari za muda huu Wazalendo wenzangu.
Kwa wale wachapa kazi wenzangu, Hongereni sana tena sana kwa Uwajibikaji makini wa kusukuma mbele Gurudumu la maendeleo ya "Tanzania ya viwanda". Hakika tutafika.
Pia niwape Pole sana kwa majukumu mazito waliyonayo wale wenzetu Wavivu, Waongo na Wambea. Poleni tena sana.

Wakati Tukiwa katika maoenyesho Makubwa ya kimataifa ya biashara na viwanda ningependa tujadili kero na matatizo ya industry nyeti kabisa ya Habari, Burudani na Michezo. Lakini ningependa leo tuzungumzie sana Tasnia ya Habari na mawasiliano hususani Tv's na Redio.
Kumekuwa na malalamiko mengi mno kwa wapenzi wa habari kwamba vyombo vyetu vya habari hususani Tv's na Redio havifanyi vizuri kutokana na huduma mbaya za upangiliajia wa vipindi vya redio na tv, pia urushaji wa kubahatisha wa matangazo mubashara. Vile vile Watanzania wengi wanasema vipindi vya kuelimisha ni vichache sana au hakuna kwa baadhi ya Redio na Tv's.
Wewe kama mpenzi wa habari na mawasiliano unadhani ni matatizo gani makubwa ambayo karibia kila Tv's na Redio za Tz lazima huyakute. Pia nini unahisi kikifanyiwa mabadiliko utajisikia huru kuangalia au kusikiliza media za Tz. Kuwa huru kujieleza kama JF ilivyo huru kwa watumiaji wake.

N.B. Kumbuka Uzi huu haujalenga chombo fulani cha habari, kwahiyo siyo sahihi kutaja chombo chochote cha habari au kutaja jina la mmiliki au mfanyakazi husika. Asante.
 
First kucoment,ila redio zooooote naona maruwe ruwe tu labda nisikilize mpira au hotuba fulan bhas na kwaya,kinyume na hapo naumiza masikio tu
 
1. Tatizo la kuwa na ratiba moja inayofanana ya urushaji matangazo. Unakuta habari zote ni Kati ya saa 1 na saa 3 jioni.
2. Kutokuwepo kwa mkalimani wa lugha kwa wasio sikia. Tv nyingi hazina mtu huyu.
3. Lugha moja imetawala karibia vyombo vyote vya habari. TZ ni miongoni mwa nchi zinazotumia Kiswahili and Kingereza kwa wingi, lakini ili kupata habari za ndani kwa Kingereza huna budi kununua gazeti.
 
1. Tatizo la kuwa na ratiba moja inayofanana ya urushaji matangazo. Unakuta habari zote ni Kati ya saa 1 na saa 3 jioni.
2. Kutokuwepo kwa mkalimani wa lugha kwa wasio sikia. Tv nyingi hazina mtu huyu.
3. Lugha moja imetawala karibia vyombo vyote vya habari. TZ ni miongoni mwa nchi zinazotumia Kiswahili and Kingereza kwa wingi, lakini ili kupata habari za ndani kwa Kingereza huna budi kununua gazeti.
Kwanini usisizikilize TBC na Kiss FM?
 
Vyombo vya habari kutokua mlengo unaoleweka ki siasa, hivyo kubinywa kwa Uhuru wao wenyewe kwa unafiki wao. Kutobandika saa kwa juu ili kila mtu anaeangalia tv ajionee muda mwenyewe.
 
binafsi naona tatizo la vyombo vingi vya habar vina shida kwanza ya kuwa na mtililiko wa vipindi vinavyo fanana mfano sio tu habar labda kuwa saa mbili usiku lakini ukifika saa sita usiku wote wanaweka miziki kitu ambacho kwa sisi wengine tunao chelewa kulala hatupendi,lakini pili naweza kuamini waandishi wa habar wengi ni waoga kwani unakuta hakuna habar nyingi za kiuchunguzi ilihali nchi hii ina habar nyingi za kiuchunguzi hasa za serikali lakini waandishi bado sio watu wa kuuliza maswali hasa kwa watawala ukizingatia watawala wakati wa kampeni waliahidi mengi,ningetamani kuwe na vipindi vya maswali magumu kwa watawala hili litawezekana waandishi wakiacha uoga,pia kuna habar za kisheria mfano bunge tumekatazwa kuonyeshwa live bunge ilihali bunge kwa mujibu wa katiba ni sawa na mkutano wa hadhara ambao wana nchi tungependa kusikia yanayo jadiliwa tuwe tunapenda au hatupendi hapa nilitegemea waandishi wangetumia wanasheria kuleta vipindi vya kudadisi kwa wahusika hadi kupata muafaka pia kukosekana vipindi kama vya wanyapori ilihali tuna mbuga ambazo zingetosha kabisa kutengeneza vipindi,leo tuna maonyesho ya sabasaba sijaona waandishi wakijadili kwa kina kuhusu maonyesho hayo ili kuleta maana ya kuwepo kwake leo unakuta habar ni za kishabiki shabiki mfano sasa rais wa nchi ndio amekuwa chanzo cha habar cha vyombo vingi,pia hakuna mijadara ya live ya wanasiasa ambayo ingekuwa inaandaliwa vizuri kwa kuwa na waandishi wanaojua kuhoji kidogo itv wamejalibu kwenye kwenye kipima joto ingawa bado,lakini waandishi wanashabikia sana siasa za ccm kuriko za upinzani mfano unakuta kila chombo kina muhoji katibu wa ccm polepole,lakini huwezi ona wa upinzani wakipewa sana nafasi ni hayo tu kwa leo
 
Back
Top Bottom