Uzi maalum: Uliza chochote kuhusu Drone

Uzi maalum: Uliza chochote kuhusu Drone

Lupamba's grandson

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2015
Posts
1,230
Reaction score
1,199
Habarini wana jamvi,

Najua wote tuna kila sababu yavkumshukuru Mungu kwakutupa uhai na afya njema japo kuna wenzetu ambao wako na taabu na shida mbali mbali Mungu wetu muaminifua atawaponya.

Ok let me start, mimi ni mmoja wa watu wanaotumia drone karibu kila siku kwa sehemu ya kazi zangu na project zangu maeneo mbali mbali ya nchi na sehemu chache za nje ya mipaka yetu , yote ni sababu ya project ninazofanya inanilazimu drone iwe sehemu ya kazi nizifanyazo.

Naipenda kazi yangu, napenda drone, napenda kurusha drone, huwa na enjoy mbali na kuwa sehemu ya kazi pia ni sehemu ya entertainment kwangu. Kwahyo basi wewe kama una swali waweza uliza chochote kuihusu drone.

Karibu.
 
unaweza kutengeneza no fly zone for drone? yaani sehemu fulani isipite? unaweza kuifunga mabomu na kwenda kulipua sehemu? Unaweza ifunga mashine gun na kwenda kujegeja swhemu?
No fly zone inawezekana ,ndio maana Airport Drone huwa hairuki na ukiwasha inazima na inakuletea message kwamba hapa ni no fly zone, ila pale kwenye ramani inakuwa na duara jekundu kubwa na dogo ambapo kwenye duara kubwa jekundu ukiwepo mule drone itaruka ila itakuwa ina blink taa nyekundu mbele na nyuma kukupa warning kwamba hapo no fly zone na ikiwa ndani ya lile duara jekundu kabisa drone huwa inawaka na kujizima kwamba huwezi kurusha kabisa

Na sehemu ambazo kuna no flay zone ni kama Airport
Military base
Kuna baadhi ya sehemu kama sehmu zenye ikulu nk.
RiAsIly.jpg
 
Mkuu hizi drone za bongo hatuwezi kuzifungia silaha na camera kali tukazitumia kwenye operation zetu za kijeshi na kipolisi kama kusaka majambazi mapolini na ikiwadaka inaweza ku engage yenyewe??
Hiyo sasa mpka uwe na technolojia au uende DJI wenyewe waku disignie jinsi unayo taka maana zipo special kwakupeleka madawa au mahitaji mengine, na zikifika on point zina drop ule mzigo
sparrow2.jpg
shutterstock_232490590.jpg
 
No fly zone inawezekana ,ndio maana Airport Drone huwa hairuki na ukiwasha inazima na inakuletea message kwamba hapa ni no fly zone, ila pale kwenye ramani inakuwa na duara jekundu kubwa na dogo ambapo kwenye duara kubwa jekundu ukiwepo mule drone itaruka ila itakuwa ina blink taa nyekundu mbele na nyuma kukupa warning kwamba hapo no fly zone na ikiwa ndani ya lile duara jekundu kabisa drone huwa inawaka na kujizima kwamba huwezi kurusha kabisa

Na sehemu ambazo kuna no flay zone ni kama Airport
Military base
Kuna baadhi ya sehemu kama sehmu zenye ikulu nk. View attachment 714096
Interesting , Nin haswa kinachoizima drone maeneo hayo?
 
Interesting , Nin haswa kinachoizima drone maeneo hayo?
Unapo washa drone mara nyingi itakuomba uwashe GPS so kuna kuwa na page mbili moja inakuonyesha ramani moja inakuonyesha picha au video kutoka kwenye camera iliyo chini ya drone ,na drone inapokuwa katika point ile uwa inarecord kituo ilipo ,ukiangalia kwenye map utaona point uliyopo na unapoinyanyua itakuonyesha ramani yote drone itakapo pita ,hii inasaidia hata drone inapokaribia kusiha chaji kuna buton inaitwa Home uki pres drone itarudi pale ilipoondokea kwakufuata ile map.

Lakini sasa kabla uja press ile button kama uliset kwamba Bettry lever ikifika 15% drone ijioperate kwenda kwenye return home mode basi utasikia saut ikikwambia Low better na return home ita ji autopilot ku return home pale ilipotokea,

Na hata kama drone ilikuwa umbali wowote ule ikapoteza link kwamaana conection ya drone na remote basi kama uliset ikipoteza iwe ina hover au i return home itafanaya hvyo ,

Sasa basi swala la kwanini hairuki ni kwamba unapowasha GPS ika detect kwamba pale kuna maeneo niliyo yataja pale juu kama vile
Airport
Military base
Ikulu na maeneo mengine ambayo ni prohibited
Drone ukiangalia kwenye map itakuwa imekuchorea duara mbili la ndani na nje ,kama kwenye ile map ww uko ndani ya duara kubwa la nje drone itawaka lakini ita indicate red flash lite kwenye wings mbele na nyuma,
But kumbuka kwamba Drone ina light nne yan trobe light ambazo za mbele always zinawaka red
Taa Za nyuma zina rangi tatu:

Yellow light=
ni kwamba no conection between RC/Drone na remote, au ukicheki kwenye remote itakwambia "Aircraft warming up "

Green light=
Hapa ni kwamba drone imesha warming up sasauko tayari kuruka na hapa ni baada ya ku calibrate drone yako itakuandikia pale kwenye remote " Ready ro Go"

Red light =
Hapa kuna mambo mawili au matatu
1: drone ikiwasha red light ikiwa chini ujue kwenye remote ukicheki kwenye map itakuonyesha mahali ulipo ni no fly zone na uko kwenye duara jekundu ,na pale kwenye remote itakuletea notes na maelezo na polices za FAA kuhusu kurusha drone maeneo ambayo ni no fly zone hasa Airport na military base

2:sababu nyingine ya pili kama drone ikawasha red light ikiwa juu basi ujue batter yako iko lowa na wakati uwo huku kwenye remote itakuonyesha betry iko low kiasi gani kwa percent ulizo weka may b uliweka ikifika 15% iku alert .na hapa ndipo pale itaji Autopilot na kurudi ilipotoka au ww uamue ku disengage Autopilot ufanye wenyewe manually
RiAsIly.jpg
 
Drone ni ruksa kwa matumizi hapa TZ?
Drone zilipoingaia watu wengi sana walianza kuzitumia kwa kazi zao za video na wengine hasa wahindi mjini waliwanunulia watoto wao kwaajili ya kuchezea ,kwahiyo siku zimeenda watu wengi wakamiliki drones sasa tatizo limekuja kila mtu ni pilot sasa zile polices za FAA watu hawazifuati maana ile ina apply kwa nchi zote ndio maana week mbili tatu hv BBC na hata CNN walionyesha clip ya kijana anae tafutwa na police paada ya kurusha drone maeneo ambayo ndio njia ya ndege kutua sasa akarusha wakati kamera inashuti ikaonekana ndege kubwa sana inapita chini ya drone sasa lile ni kosa kubwa mno tena sana kwahyo anatafutwa ,
Sasa kwa hapa kwetu majuzi walitangaza kuzuia nakusema mtu anayetaka kurusha lazima awe na kibali maalum kutoka TAA, Wizara ya Uchukuzi sijui na nn ( mmeijuia hii wizara misijui) na pia uwe na kibali cha police ,sasa sijaona kama wameitilia mkazo ila mimi hapa binafsi nilishakamatwa pale mwenge na wanajeshi ,nilirusha drone kuna project nilikuwa nafanya sasa kumbe eneo lote pale ni jeshini sikujua mana GPS sikuwa nimewasha badala yake ilionekana nikafatwa na wenye kofia nyekundu uzuri niliwaeleza poa nikawaonyesha footage na wakanielewa wakasema nilazima kama nataka fanya hvyo nikachukue kibali kwao sasa wengine nao walikamatwa wakaenda kurushwa kichura nadhani walishindwa kujieleza. Hvyo tu dnugu nadhani nimekujibu
 
Hizo drone zinauzwa bei gan? na kwa bongo zinauzwa wap?
Drone ina tegemea kama ni drone ambazo ni DJI amabapo mara nyingi zinatumika ku shutia video kuna

DJI PHANTOM 3 PRO ilikuwa inauzwa dollar $ 1200 sasa waweza pata mpka dollar $ 800
DJI PHANTOM 3 ADVANCE

DJI PHANTOM 4
DJI PHANTOM 4 PRO hizi P4 series zilikuwa zinauzwa dollar $ 2300 sasa waweza pata hata kwa dollar $ 1700

DJI MAVIC PRO
DJI MAVIC AIR hizi ni toleo jipya la dji unaweza pata kwa mpka dollar $ 3000
 
Drone zilipoingaia watu wengi sana walianza kuzitumia kwa kazi zao za video na wengine hasa wahindi mjini waliwanunulia watoto wao kwaajili ya kuchezea ,kwahiyo siku zimeenda watu wengi wakamiliki drones sasa tatizo limekuja kila mtu ni pilot sasa zile polices za FAA watu hawazifuati maana ile ina apply kwa nchi zote ndio maana week mbili tatu hv BBC na hata CNN walionyesha clip ya kijana anae tafutwa na police paada ya kurusha drone maeneo ambayo ndio njia ya ndege kutua sasa akarusha wakati kamera inashuti ikaonekana ndege kubwa sana inapita chini ya drone sasa lile ni kosa kubwa mno tena sana kwahyo anatafutwa ,
Sasa kwa hapa kwetu majuzi walitangaza kuzuia nakusema mtu anayetaka kurusha lazima awe na kibali maalum kutoka TAA, Wizara ya Uchukuzi sijui na nn ( mmeijuia hii wizara misijui) na pia uwe na kibali cha police ,sasa sijaona kama wameitilia mkazo ila mimi hapa binafsi nilishakamatwa pale mwenge na wanajeshi ,nilirusha drone kuna project nilikuwa nafanya sasa kumbe eneo lote pale ni jeshini sikujua mana GPS sikuwa nimewasha badala yake ilionekana nikafatwa na wenye kofia nyekundu uzuri niliwaeleza poa nikawaonyesha footage na wakanielewa wakasema nilazima kama nataka fanya hvyo nikachukue kibali kwao sasa wengine nao walikamatwa wakaenda kurushwa kichura nadhani walishindwa kujieleza. Hvyo tu dnugu nadhani nimekujibu
Umenijibu vizuri na kwa ufahamu ,ila kwa kuwa Wewe ni mtumiaji mzuri wa Drone ili uwe salama ni vyema ukamilishe vibali.
 
Back
Top Bottom