Dawa za meno ambazo ni nzuri kwa ulinzi wa meno

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Wakuu mimi binafsi natumia colget Advanced whitening kina ujazo wa 75mil si nyingi ila bei yake ni Tsh. 4,500 hii nzuri sana watoto wa Arusha utawakamata sana si unajua yale meno yao.

Je wewe unatumia Dawa gani? ili niweze ku shift kama ni nzuri zaidi! kuna hizi wanaziita sensodine naona zipo za aina nyingi na sijazikubali ni vigumu kugundua feki.

========

1591530892643.png


Dawa ya kusugulia meno ni kemikali inayotumika pamoja na mswaki wa kisasa kusafishia meno yazidi kupendeza na kuwa na afya.

Inasaidia kuondoa harufu mbaya, utambo wa meno na mabaki ya chakula katikati yake, pamoja na kuacha aina ya kinga (hasa ya floridi, kwa Kiingereza "Flouride") dhidi ya maradhi ya meno na ya ufizi (nyama inayoambatana nayo) (kwa Kiingereza "gingivitis").

Hata hivyo kwa kiasi kikubwa ufanisi wa usafi unategemea zaidi matumizi ya mswaki wenyewe kuliko ya dawa hiyo.

Badala ya dawa ya meno vinaweza kutumika chumvi na magadi.

Dawa ya meno hayatakiwi kumezwa kutokana na floridi iliyomo. Ikimezwa kidogo si hatari sana, lakini kama ni kiasi kikubwa ni lazima kuomba msaada wa daktari.

Dawa ya meno iliyotengenezwa kwa kusaga mifupa au chaza ilianza kutumika katika Ugiriki wa Kale na Roma ya Kale.

Matumizi yake yalienezwa hasa katika karne ya 19.

Nchi mbalimbali zimekataza aina kadhaa za dawa ya meno kutoka China kwa sababu zina sumu aina ya diethylene glycol (kifupi diglycol au DEG).

Michango ya wadau

World Dentists Association wamekubaliana kwamba dawa za meno ziko kwa ubora kama ifuatavyo:

1. Sensodyne
2. Crest
3. Colgate

Pamoja na ku list hizo dawa hapo kulingana na ubora wake lakini mambo yafuatayo ni lazima kuyatilia maanani

1. Jinsi ya kuutumia mswaki, wengi wetu huwa tuna maarifa haba ya kuutumia mswaki na mara nyingi hulifanya zoezi hilo kwa haraka sana kuliko inavyohitajika

2. Uhalisia wa Bidhaa
Nimeishawahi kutana na Sensodyne zinazotembezwa na Wamachinga zilikiuzwa bei rahisi sana nilipokuja kuzitumia niligundua zimechakachuliwa hivyo hazikuwa na ubora. Dawa ambayo sijaona kuchakachuliwa ni Crest labda kwa sababu siyo maarufu sana sokoni

3. Jina Moja Malengo Anuwai
Unaweza ukalalamika dawa haijakusaidia lakini Sensodyne au Colgate uliyochukua haiko sawa na mahitaji yako. Kuna Sensodyne kwa ajili ya kuripea, kungarisha au kuondosha kutu hivyo ni muhimu kusoma kasha la dawa kabla hujanunua au pata ushauri toka kwa dentists
----
Me natumia colgate maxfresh ambayo ina box kama la redbrown (kuna zenye box la blue)hivii au ukisema maximum spiced unapatiwa iwe dukani kwa mangi au supermarkets zinapatikana 3500-4000 ,hizo sensodyne ,ile aloe hamna kitu japo dr wanashauri
----
Mimi mwanzo nilipata sensodyne kwa 6500 nimetumia imesaidia kidogo ila mara ya pili nikanunua kwa 12000 hii ilikuwa kiboko.

Kuna jino langu limetoboka sasa ikifika usiku linauma balaa,nikawa natumia hii ya 12K basi jino likiuma napaka sensoydne mswaki napiga aisee baada ya dakika maumivu yote yanapotea kama sio jino lile.

Sasa hivi imeisha ni kama wiki hivi natumia mswaki tupu huwezi amini jino haliumi tena kama zamani na hakuna jino linalouma japokuwa limetoboka,nafanya mpango nifumbe macho nikanunue tena duka lilelile nina imani nikitumia kwa mwaka mmoja tu tatizo la meno litaondoka
----
Kuna Colgate ya Maji inaweza kukufaa. Ila Tumia Mouth Wash imeandikwa Lasterine kuna yenye rangi ya kijani na Gold (Nakushauri tumia ya rangi ya Gold ni nzuri zaidi unaweza kusukutua na kupigia mswaki) Then baada ya hapo tumia Colgate Herbal ni poa sana isipokuwa shida fake ni nyingi. Colgate Origanal ni ya Thailand au Brazil.

NB: Kwa meno yaliyotoba kitu kinachosaidia zaidi ni usafi wa meno kupiga mswaki mara tatu/kila baada ya kula nje ya hapo yatakuzingua tu maana mabaki ya chakula yakikaa siku kama tatu yanatengeneza uchafu/usaa unaoleta maumivu na uharibifu zaidi
 
Kiukweli nilijua izo sensodine ni nzuri but hovyoo ni kama AHA ya buku tu, ila kuna Colgate moja nzuri niliitumia kipindi flani ina viparticle kama vya srcub ivi ilirudisha weupe wa meno yangu sana na ufresh wa mdomo unauhisi kabisa.
 
Sensodyne, very good!
Sensodyne very good vry good Mkuu usiache kuitumia hii na huta juta... huuwa vijidudu....unajua unatakiwa kutumia dawa sio tuu inawesafisha meno yawe meupe lakini zaidi iuwe vijidudu vilivyobakia.

Pia msisahau akama mna muda kutumia hata listerine kwa kusukutua mara moja moja.
 
Dr kanishauri nitumie SENSODYNE, cha ajabu humu inapondwa! Daah.
Tumia sensodyne hutojuta Mkuu
Sensodyne very good vry good Mkuu usiache kuitumia hii na huta juta... huuwa vijidudu....unajua unatakiwa kutumia dawa sio tuu inawesafisha meno yawe meupe lakini zaidi iuwe vijidudu vilivyobakia.

Pia msisahau akama mna muda kutumia hata listerine kwa kusukutua mara moja moj....
wanaoponda hawajui na wanaogopa gharama wao wanapenda vitu cheap vya jero...
 
natumia close up mkuu ni nzur inapatikana supermakert zote bei kulingana na ujazo unaoutaka lakn minimum price 2500
Mm mwenyewe naipenda sana hii dawa, cjawahi kutumia dawa ambazo ni expensive ila kwa hizi za mid range-price naona hii ni nzuri sana, japo kwenye maduka ya kawaida ni ngumu kuzipata
 
Back
Top Bottom