Uzi Maalum: Tetesi za soka Ulaya 2017

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 16.06.2017
*Chelsea kunafukuta?
*Real ‘wakomaa’ na Morata
*Giroud kufanywa ‘chambo’
*Ronaldo kuodoka Spain

Kuna ‘hali ya mvutano’ kati ya meneja wa Chelsea Antonio Conte na Diego Costa kufuatia hatua yake ya kumwambia Costa kwa ‘text message’ kuwa hamhitaji tena Stamford Bridge msimu ujao (Gazzetta dello Sport).

Chelsea wanataka kumaliza mzozo kati ya Conte na Costa, na Costa akiwa tayari kufanya hivyo ili kufahamu mustakbali wake, lakini Conte hataki kabisa (Sun)

Wakati huohuo Antonio Conte ametoa masharti kadhaa, ikiwemo kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na mmiliki wa timu Roman Abramovic, kuwa na udhibiti wa kuteua makocha wasaidizi, pamoja na mikataba bora ya kifedha, ikiwa Chelsea wanataka aendelee kubakia Stamford Bridge (Daily Record).

Mazungumzo kati ya Chelsea na kipa Thibault Courtois, 25, yamedorora kutokana na suala la mshahara. Courtois kwa sasa analipwa pauni 100,000 kwa wiki na mkataba wake unaisha miaka miwili ijayo (Times).

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anazidi kughadhibishwa na klabu hiyo kujivuta katika kufanya usajili na huenda akawa tayari kuondoka darajani (Sky Sports Italia).

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema bei ya kipa David de Gea, 26, ni pauni milioni 100, na kama Real Madrid wanamtaka, watoe pauni milioni 45 pamoja na Alvaro Morata (Daily Star).

Cristiano Ronaldo, 32, ameiambia Real Madreid kuwa anataka kuondoka Spain na kuwa habadilishi uamuzi wake huo (A Bola).

Kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, bado anasakwa na Everton, licha ya klabu hiyo kumsajili Davy Klassen kutoka Ajax (Wales Online).

Liverpool wanataka kukusanya fedha kwa kuwauza beki Mamadou Sakho, 27, kwa pauni milioni 30, beki Alberto Moreno, 24, kwa pauni milioni 12 na Lazar Markovic, 23, kwa pauni milioni 20 (Times).

Dau la pauni milioni 17.6 la Arsenal kumtaka winga Juan Cuadrado, 29, limekataliwa na Juventus. Klabu hiyo ya Italia inataka takriban pauni milioni 30 kumuuza mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea (Sun).

Arsenal wametoa pauni milioni 10.5 kumtaka beki wa kati wa Fenerbahce Simo Kjaer, 28, ambaye pia anasakwa na AC Milan na Inter Milan (Turksvoetbal).

Winga wa Inyter Milan Ivan Perisic, 28, tayari anajiandaa kuwa mchezaji wa Manchester United, ingawa timu hizo mbili bado hazijafikia makubaliano ya pauni milioni 44 za uhamisho (Manchester Evening News).

Real Madrid wanasisitiza kuwa wanataka pauni milioni 78 kumuuza Alvaro Morata, 24, licha ya taarifa za kupewa ’mkataba mnono' na Manchester United (Independent).

Baada ya kukamilisha usajili wa beki Victor Lindelof, Manchester United huenda wakarejea Benfica kumsajili kiungo Anderson Talisca, 23, kwa pauni milioni 15. Talisca alicheza kwa mkopo Besitkas msimu uliopita (Daily Mirror).

Mshambuliaji wa Manchester City Patrick Roberts, 20, aliyefunga mabao 11 msimu uliopita akiichezea Celtic, anazungumza na Nice ya Ufaransa kwa ajili ya kwenda kwa mkopo (Sun).
Tottenham ni moja ya timu zinazomfuatilia mshambuliaji wa Lazio, Keita Balde, 22, ambaye ana thamani ya pauni milioni 30 (Daily Mirror).

Southampton wanataka kumfanyia usaili meneja wa zamani wa Ajax, Frank de Boer na pia meneja wa zamani wa Valencia Mauricio Pellegrino, kuziba nafasi ya Claude Puel, na wana matumaini ya kutangaza meneja mpya mwishoni mwa wiki ijayo (Daily Telegraph).
Meneja wa zamani wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel amesema hawanii nafasi ya kazi ya Southampton (Sky Sports).

Stoke huenda wakataka zaidi ya pauni milioni 30, iwapo watamuuza kipa Jack Butland, 24, ingawa wamesisitiza kuwa hauzwi (Stoke Sentinel).

Timu kadhaa za EPL ikiwemo Newcastle United zinamuulizia beki wa kati wa Valencia Aymen Abdennour, 27, kwa pauni milioni 13.1 (Foot Mercato).

Paris Saint Germain wameacha kumfuatilia mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick Aubameyang, 27, kwa sababu bei ya pauni milioni 61 ni kubwa mno, kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa PSG Antero Henrique (Goal.com).

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameanza mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa Real Madrid Toni Kroos (Don Balon).

Real Madrid wanaongoza katika mbio za kutaka kumsajili Gianluigi Donnarumma kutoka AC Milan, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Paris Saint Germain (Sky Sports Italia).
Arsenal wako tayari kumtumia Olivier Giroud kama chambo ili kumsajili Kylian Mbappe au Alexandre Lacazette (Daily Express).

Southampton wanataka kumsajili Ben Gibson ili kuziba nafasi ya Virgil van Dijk (Daily Mirror).
Habari zilizothibitishwa, tutakujuza mara tu zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine, kesho tukijaaliwa.

Tafadhali share tetesi hizi na wapenda soka wote. Weekend Njema!
 

pangalashaba

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
1,235
2,000
Thanks mkuu!!!! Nimeisoma yote mkuu ila Arsenal wanatia hasira sana mana ukiangalia habari nzima ni wao tu ndo wanatangaza kununua kwa bei ndogo kama siyo cheap...... Kwa style hii, hata top four ya EPL wasahau kabisaaaaaaa... Soka la ulaya ni uwekezaji km uwekezaji mwingine... Mtaji mdogo, tegemea return ndogo kutoka kwenye mtaji wako...
 

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,971
2,000
Thanks mkuu!!!! Nimeisoma yote mkuu ila Arsenal wanatia hasira sana mana ukiangalia habari nzima ni wao tu ndo wanatangaza kununua kwa bei ndogo kama siyo cheap...... Kwa style hii, hata top four ya EPL wasahau kabisaaaaaaa... Soka la ulaya ni uwekezaji km uwekezaji mwingine... Mtaji mdogo, tegemea return ndogo kutoka kwenye mtaji wako...
Huyu mzee ni mzigo mkubwa sana pale EMIRATES
 

Kyawanjubu

JF-Expert Member
May 13, 2017
2,388
2,000
Ulaya mkataba ukibaki miaka 2 watu wanahangaika kusaini mwingine tz mkataba mrefu ni miaka mi 2 wanafanya mazungumzo ukibakia mwezi mmoja tuko dunia gani sisi wazee wa makinikia
 

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 19.06.2017

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemwambia wakala wake Jorge Mendes kufanikisha uhamisho wake kurejea Manchester United (Sun).
Manchester United watawapa Real Madrid David de Gea, 26, pamoja na pauni milioni 183, ili kumsajili Cristiano Ronaldo, 32 pamoja na Alvaro Morata, 24 (Tuttosport).
Manchester United itawapa Real Madrid David de Gea pamoja na pauni milioni 175 kumchukua Ronaldo, na pia watamfuatilia Alvaro Morata katika mkataba mwingine tofauti (Daily Mirror).
Iwapo De Gea atakwenda Real Madrid, Manchester United watamfuatilia kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 18 (Calciomercato)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hamtaki Ronaldo kwa sababu anahisi kiwango chake kimeanza kushuka (Diario Gol).
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amempigia simu Ronaldo kujaribu kumshawishi asiondoke Madrid (Marca).
AC Milan huenda wakaamua kumfuatilia kipa wa Manchester City Joe Hart, 30, iwapo kipa wao Donnarumma ataondoka (Daily Express).
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amekuwa akivutia timu mbalimbali nchini Spain, Italy, Uturuki na Marekani pamoja na China, lakini Rooney pia huenda akaamua kubakia Old Trafford (Times).
Chelsea wataongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro, 26, pamoja na kiungo Tiemoue Bakayoko, 22 (Guardian).
Kiungo wa Italy Marco Verratti, 24, anataka kuondoka Paris Saint Germain kwenda Barcelona (Gazzetta dello Sport).
Liverpool bado wapo kwenye mazungumzo na Roma kuhusu uhamisho wa winga Mohamed Salah, 25, lakini hawataki kulipa pauni milioni 35 wanazotaka klabu hiyo ya Seria A (Sky Sports).
Everton watafikisha pauni milioni 60 za usajili wiki hii watakapokamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Malaga, Sandro Ramirez, 21 (Daily Star).
Southampton wanataka kumsajili beki wa kimataifa wa Austria, Kevin Wimmer, 24, lakini wanataka Tottenham kupunguza bei ya pauni milioni 20 (Daily Mirror).
Leicester City wanafikiria kutoa dau la pili kumtaka beki Jonny Evans, 29 kutoka West Brom (Daily Telegraph).
Chelsea wanataka kuongeza dau kufikia pauni milioni 60 kumsajili beki wa Juventus Alex Sandro (Daily Express).
Manchester United wamempa ‘ofa’ya mkataba mkubwa zaidi Blaise Matuidi, kuliko aliokuwa nao sasa PSG (PSG United).
Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 44 kumsajili winga wa Sporting Lisbon Gelson Martins (A Bola).
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang huenda akaungana na meneja wake wa zamani Jurgen Klopp, Liverpool (Le Parisien).
Barcelona watatumia kifungu cha kumnunua tena Gerard Deulefeu kwa kutoa pauni milioni 10.5 kwa Everton (Times).
Marco Asensio huenda akaomba kuondoka Real Madrid iwapo timu hiyo itasajili wachezaji watakaomuweka ‘benchi’, huku Arsenal, Liverpool na Juventus wakiwa wamemuuliza kiungo huyo mshambuliaji (Diario Gol).
Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 26.3 kumsajili kiungo wa Barcelona Arda Turan (AMK).
Mshambuliaji wa Arsenal Takuma Asano, 22, atabakia kucheza kwa mkopo Stuttgart msimu ujao kwa sababu hawezi kurejea Emirates kwa kuwa hajatimiza vigezo vya kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza (Daily Express).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara tu zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Tafadhali share tetesi hizi na wapenda soka wote. Nakutakia Jumatatu njema.
 

sulty25

Senior Member
Aug 25, 2016
133
250
Cr7 nadhani anawatia hofu maboss wake ili waweza kumlipia kodi anayodaiwa
 

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 22.06.2017

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, atakaidi hatua ya Antonio Conte na kukataa kuondoka Stamford Bridge, hadi akubaliwe kurudi Atletico Madrid (Daily Star).

Diego Costa amewaambia Atletico Madrid kuwa anataka kurejea Spain. Kutokana na Atletico kufungiwa kusajili, hata akisajiliwa sasa hatoweza kucheza hadi Januari (Sky Sports).

Thibault Courtois hajasaini mkataba mpya, huku Real Madrid wakimnyatia. Kipa huyo wa Chelsea anataka mkataba wa pauni milioni 10 kwa mwaka (The Sun).

Real Madrid wanasubiri Manchester United kupanda dau la kumtaka mshambuliaji Alvaro Morata, 24, kabla ya mabingwa hao wa Ulaya kuanza kumfuatilia Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Diario Gol).

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane atafikiria kuimarisha safu ya ulinzi kwa kumchukua Leonardo Bonucci kutoka Juventus. Zidane hana mpango wa kusajili mabeki wengine na atatoa nafasi kwa chipukizi ikiwa hawatoafikiana na Juve (Diario Gol).

Hatua ya Ronaldo kubadili mawazo ya kuondoka Real Madrid, imelazimisha Manchester United sasa kuzingatia zaidi usajili wa Alvaro Morata. Jose Mourinho tayari ametenga pauni milioni 60 na wanadhani watamchukua kabla ya mechi za kabla ya kuanza kwa msimu (The Sun).
Cristiano Ronaldo anafikiria kwenda Paris Saint Germain baada ya kupewa dau na klabu hiyo (Marca).

Jose Mourinho ameiambia Manchester United kuachana na Ronaldo na kulenga kumsajili Neymar badala yake (Don Balon).

Juventus wamepiga hatua za mwanzo katika jitihada zao za kutaka kumsajili Matteo Darmian kutoka Manchester United (Sky Sport Italy).

Kiungo wa Manchester City Samir Nasri anatarajiwa kupewa mshahara wa pauni 275,000 kwa wiki, baada ya kukatwa kodi, ili kujiunga na Shanghai Shenhua ya China (The Sun).

Manchester United wamekuwa na mazungumzo na wakala wa Robert Lewadowski katika jitihada za kutaka kumchukua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland na Bayern Munich (Sky Sports).

Zlatan Ibrahimovic anataka kwenda Real Madrid baada ya kuruhusiwa kuondoka Manchester United (Diario Gol).

Mustakbali wa Robert Lewandowski kusalia Bayern Munich utategemea na matokeo ya klabu hiyo ya Ujerumani kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez (The Sun).

Leicester City wanapanga kutoa pauni milioni 25 kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20 (Daily Telegraph).
Leicester wanafikiria hatua ya kuchukua baada ya West Brom kuwaambia watahitaji kutoa pauni milioni 10 ikiwa wanamtaka beki Jonny Evans, 29 (Leicester Mercury).

Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kutoka Monaco kwa pauni milioni 35, hatua ambayo huenda ikasababisha Nemanja Matic, 28, kuondoka na kwenda Manchester United (Daily Mail).

Sakata la Manchester City kumtaka beki wa Tottenham Kyle walker, 27, litaendelea hadi wiki ijayo baada ya Spurs kukataa kushusha bei ya pauni milioni 50. Hata hivyo City wataendelea kumfuatilia pia Dani Alves kutoka Juventus (Independent).

Manchester City wapo tayari kupokea pauni milioni 18 kutoka Lyon ili kumuuza Eliaquim Mangala. City walimnunua Mangala kwa pauni milioni 42 miaka mitatu iliyopita (SportsMole)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Siku njema.
 

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 23.06.2017
Paris-Saint Germain wapo tayari kutoa kitita kitakachovunja rekodi ya dunia cha pauni milioni 119 kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Mirror).

Lakini Arsenal wanajiandaa kutoa dau jipya kumsajili Mbappe, huku Arsene Wenger akiwa na uhakika wa kumpata mchezaji huyo (Metro).

Mbappe hana tatizo la wazo la kwenda Emirates (Telegraph).

Dau la pauni milioni 100 kutoka Liverpool la kumtaka Kylian Mbappe limekataliwa (Marca).

Mbappe inasemekana amekuwa na mazungumzo na meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane (L’Equipe).

Meneja wa Chelsea Antonio Conte yuko tayari kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwenda Manchester United ili aweze kufanikisha usajili wa kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko, 22, kwa pauni milioni 42 (The Times).

Real Spciedad wamekubali kulipa pauni milioni 10 kumsajili winga wa Manchester United Adnan Januzaj, 22 (Daily Mail).

Beki Matteo Darmian wa Manchester United amempigia simu Jose Mourinho na kumuomba amsaidie katika kuhamia Juventus (Sun).
Mwenyekiti wa Stoke City Peter Coates amesisitiza kuwa hana mipango ya kumuuza Xherdan Shaqiri, 25, msimu huu (TalkSport).

Dau la pauni milioni 12 la Stoke kumtaka beki wa Middlesbrough Ben Gibson, 20, limekataliwa. Middlesbrough wanataka zaidi ya pauni milioni 20 (Mirror).

Tottenham wamewasiliana na Fiorentina, kumuulizia kiungo Matias Vecino, 25 (TalkSport).

Tottenham wapo tayari kutoa pauni milioni 17.5 kumsajili winga wa Schalke Max Meyer (Sun).

Spurs pia wanajiandaa kumpa mkataba mpya wa miaka mitano beki wa kulia Kieran Trippier, 26, (Mirror).

Liverpool wameambiwa na Borussia Dortmund kuwa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, 28, atagharimu pauni milioni 63 (Bild).

Liverpool wamekataa dau la pauni milioni 11 kutoka Napoli la kumtaka beki Alberto Moreno 24 (Telegraph).

John Terry anafikiria kwenda Aston Villa, huku akitarajia timu nyingine za Ligi Kuu zitamtaka pia (Guardian).

Antonio Conte amewaambia Chelsea kuwa anamtaka Leonardo Bonucci, 30, wa Juventus au Virgil van Dijk, 25 wa Southampton ili kuimarisha safu yake ya ulinzi (Guardian).

Burnley wana matumaini ya kuwakatisha tamaa West Brom katika mbio za kumsajili beki wa kushoto wa Leeds Charlie Taylor, 23 (Burnley Express).

Bayern Munich wapo tayari kumtoa kwa mkopo winga wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry, baada ya kumsajili msimu huu, huku wakisaka jina kubwa katika ushambuliaji (SportBild).

Lyon wamekubaliana ada ya pauni milioni 16.7 kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Bertrand Traore, 21 (L”Equipe).

Intare Milan wanafikiria kupambana na Juventus katika kumsajili kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny, 28 (Evening Standard).

Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 100 wa Leonardo Bonucci na Alex Sandro kutoka Juventus (The Sun).

Manchester City wanazidi kuamini kuwa wataweza kumsajili Alexis Sanchez, 28, kwa pauni milioni 50. Chelsea nao wanataka kujaribu kupanda dau kumchukua Sanchez na watatoa dau rasmi hivi karibuni (Daily Mirror).

Arsenal wanataka kumfanya Jack Butland kuwa mrithi wa Petr Cech (Daily Star).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Weekend Njema nyote!!
 

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 29.06.2017
Manchester City sasa wanaongoza katika mbio za kumsajili Alexis Sanchez, 28, baada ya Bayern Munich kujitoa kutokana na bei kubwa ya mchezaji huyo wa Arsenal (Daily Mirror).

Manchester City wana uhakika wa kumsajili Alexis Sanchez kwa takriban pauni milioni 50, kwa sababu ya hamu ya mchezaji huyo kufunzwa na Pep Guardiola (Guardian)

Chelsea wanakabiliwa na ushindani kutoka Paris St-Germain katika kumsajili beki Alex Sandro, 26, huku Juventus wakitaka pauni milioni 61 (Daily Mail).

Chelsea wanatazamiwa kukamilisha usajili rasmi wa Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco wiki hii (The Sun).

Wakala wa kiungo wa Chelsea Mario Pasalic, wamekutana na Real Betis kujadili uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Spain (Marca).

Manchester United watazidiwa kete na Paris St-Germain katika kumsajili kiungo kutoka Brazil, Fabinho, 23 anayechezea Monaco (Daily Record).

Dau la Arsenal la zaidi ya pauni milioni 30, la kumtaka winga wa Monaco, Thomas Lemar, 21, limekataliwa, na sasa Arsenal wanafikiria kukamilisha usajili wa Riyad Mahrez, 26, kutoka Leicester (Telegraph).

Barcelona, Manchester City na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazomnyatia winga wa Monaco, Thomas Leimar (L”Equipe).

Arsenal wanamtaka kiungo wa Nice Jean Michael Seri, 25, baada ya Roma kukatishwa tama na bei ya pauni milioni 35 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast (The Sun)

Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud anakaribia kurejea Ufaransa, huku Lyon na Marseille wakimtaka, na Arsenal ikitafuta mtu wa kuziba pengo lake (L’Equipe).

Chelsea huenda wakatibua dau la Zenith St Petersburg la pauni milioni 26 la kumtaka beki wa Roma, Kostas Minolas, huku mchezaji huyo pia akisita kuhamia Urusi (Daily Telegraph).

Michel Keane hatarajiwi kurejea Burnley kwa sababu Everton wanatarajiwa ‘kulazimisha’ usajili wake kabla ya kumalizika kwa wiki hii (Burnley Express).

Michael Keane atagharimu pauni milioni 25 (Times).

Mshambuliaji wa Watford Stefano Okaka, 27, amepewa dau kubwa la kuhamia Shanghai Shenhua ya China (The Sun).

Arsenal wameambiwa lazima walipe pauni milioni 57 ili kumsajili Alexandre Lacazette, 26, kutoka Lyon (London Evening Standard).

Kinda wa Arsenal Kaylen Hinds anajiandaa kuondoka Emirates na kujiunga na Wolfsburg ya Ujerumani (The Sun).

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale yuko tayari kuondoka Spain na kuhamia Manchester United (Daily Star).

AC Milan wanapanga kutoa kitita kikubwa kumsajili kiungo wa Real Madrid Isco (Don Balon).

AC Milan wanakaribia kumsajili Hakan Calhanoglu kutoka Bayer Leverkusen kwa euro milioni 20 (Sky Sport Italia).

West Brom wanakaribikia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez, 27 kwa pauni milioni 12 (Daily Express).

Nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, 36, ameambiwa anaweza kuchukua nafasi ya umeneja wa Aston Villa, iwapo atajiunga na klabu hiyo (Daily Express).

Mchezaji anayenyatiwa na Liverpool Naby Keita, 22, amesema angependa kuchezea moja ya timu kubwa kama vile Barcelona, Real Madrid au Manchester City. Liverpool wanamtaka kiungo huyo wa Red Bull Leipzig (Manchester Evening News).

Beki wa Chelsea Nathan Ake, 22, anakaribia kufanikisha uhamisho wake wa pauni milioni 20 kwenda Bournmouth (Guardian).

Pierre Emerick-Aubameyang, 28, anayenyatiwa na Liverpool anaonekana kukaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Tianjin Quanjian ya China, ambayo imetoa dau la pauni milioni 70 (Daily Star).

Real Madrid bado wanafikiria kuhusu Kylian Mbappe, kwa mujibu wa Rais wa Real, Florentini Perez, ambaye anasema umri wake wa miaka 18 huenda ukawa tatizo katika klabu hiyo ingawa amekiri kuwa Zinedine Zidane yuko karibu na mchezaji huyo na usajili unaweza kufanyika (Independent).

Winga wa Everton Gerard Deulofeu, 23, amekataa nafasi ya kurejea Barcelona, huku AC Milan na Juventus pia zikimtaka (Daily Mail).

Newcastle United wanazungumza na Liverpool kuhusu uhamisho wa mkopo wa winga Sheyi Ojo, 20 (Newcastle Chronicle).

Mkurugenzi mkuu wa Southampton Les Reed amesisitiza kuwa mabeki wake Virgil van Dijk na Cedric Soares hawauzwi. Liverpool na Tottenham zinawataka wachezaji wao (Sky Sports).

Leicester City hawajapokea dau lolote la kumtaka Riyad Mahrez, ambaye amehusishwa na kuhamia Arsenal, Barcelona na Chelsea (Leicester Mercury).

Juventus wanafikiria kumchukua beki wa Real Madrid Danilo, kuziba nafasi ya Dani Alves anayetazamiwa kwenda Manchester City (Corriere dello Sport).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii:
Transfers - June 2017

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Siku njema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom