Al Hilal inamfukuzia Kane Bayern Munich

Al Hilal inamfukuzia Kane Bayern Munich

Miss Halima

Senior Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
170
Reaction score
380
Wawakilishi wa nahodha wa England Harry Kane,33, wamefanya mazungumzo na klabu ya Al-Hilal ya Ligi ya Pro ya Saudi Arabia, huku mshambuliaji huyo wa Bayern Munich akiwa tayari kuhama hapo baadaye.

Wakati huo huo, mshambuliaji wa Aston Villa na England Ollie Watkins, mwenye umri wa miaka 29, amefikia masharti binafsi na Al-Hilal, japo klabu hiyo ya Saudia bado haijawasilisha ofa rasmi ya uhamisho kwa Villa.

Newcastle imeanzisha mazungumzo ya awali na Manchester City kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa Uhispania Nico Gonzalez, mwenye umri wa miaka 24. (The Athletic - usajili unahitaji)
Mpango wa Sunderland wa kumsajili beki wa Toulouse na timu ya taifa ya Ufaransa ya vijana chini ya umri wa miaka 21, Dayann Methalie (20), kwa ada ya pauni milioni 25.7 huenda ukagonga mwamba baada ya tetesi kuibuka kuhusu vipimo vyake vya afya.

1787119676710.png
 
Huyu mwamba akikubali hilo dili, ataoga minoti kama CR7. Ni hatari sana kwa mchezaji wa mpira wa miguu kulipwa pesa nyingi kuliko kawaida!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom