Ah! Kwanza mi nilivyo sijawahi kabisa kugombana na mpenzi wangu wa zamani, na hata kama alitaka tutengane kwa ugomvi, mwenyewe tu atajishtukia! That being said, ma-ex wangu wote wanakuwa ni my friends, na kwa maana nyingine, kuna uwezekano mkubwa tu wa kuwasiliana nao inapotokea issue muhimu, social au hata binafsi!! Majuzi tu, nimewasiliana na ex-wangu wa enzi hizo! Yeye yupo NSSF na nikawa namuulizia issues za mafao ya Bi. Mkubwa! Aidha, kuna wakati nilipata mitihani ya maisha nikawa nimechoka kishenzi! But trust me, mtu ambae alikuwa ni msaada wangu mkubwa sana, tena sana ni ex wangu wa tangu chuo; na hadi sasa ananidai Sh. 350K na nina uhakika ameshasahau lakini mimi sijasahau! Kuna ex wangu mwingine nilikutana nae humu humu JF! Majuzi tu alikuwa na shida fulani serious inayohitaji mkono wa pili, and I supported her!Samahani mimi namuwakilisha myplusbee
Hata hivyo, sijawahi kupasha kiporo kwa yeyote yule, na sioni ni namna gani inaweza kutokea! Wanaopasha viporo ni wale wanaoachana kwa fujo, visa na kila aina ya mitafaruku! Akili zao zikija kutulia, wanajikuta kumbe bado wanatakana kama sio kupendana!! Kwa bahati mbaya au mzuri, that's not my style; kwanza mambo ya kuachana na magomvi najionea ushamba tu!
Sasa kama mtu sina shida nae, kwanini nisiwasiliane nae kunapokuwa na ulazima wa kufanya hivyo?!
