Elections 2010 Uzembe wa mawakala kuwaponza wapinzani

uliwezaje kuwatambua wakati hawana ID za kimavazi au hao walikuwa nazo??
Anyway, mi nimeshapiga kura na nikiwa mle kituoni ukatokea utani fulani nikamsikia wakala mmoja akisema mwaka huu HADUNGANYIKI!!
na mm nikaungana nao kwenye tabasamu, baada ya hapo nikaenda pale kwenye kichumba nikamsalimu Dk wa ukweli na vijana wake nikakunja karatasi zangu na kuzitumbukiza sehemu stahili na tabasamu langu pana nikawapishe wengine nao watoe hukumu..
Nilikuwa wa kwanza kituoni hapo na walipoitwa na msimazi wa kituo wakajitambulisha nilikuwepo na nilisikia mazungumzo yao
 
A lot have happened. sitaki kuamini kuwa ni uzembe wa CHADEMA. kwa mfano, jmosi usiku, shule ya msingi kurasini, mpaka kuelekea saa nne, bado vifaa vilikuwa havijafika - ingawa katika vituo vingine tayari mambo yalishakuwa tayari.
Hawa ni wakazi wa kawaida tu, na nina shaka kuwa kuna mkono wa chama cha mafisadi. utekaji nyara, kuwekewa madawa, and a lot more relevant to their field of theft. CHADEMA walikuwa, na bado wako makini.
Cha msingi ni kuspread information kama NIKUPATEJE alivyofanya. the is still on our side, hakuna kukata tamaa.
 
NAomb kuwakumbusha kuwa kuna majimbo kama Ubungo mbunge mtarajiwa Mnyika ameweka mawakala wengine ambao huwezi kuwatambua hata watendaji wengine wa NEC ni watu wake... jamani acheni kulalamika PIGENI KURA! Mkishtukia kitu pigeni simu! Msiwakatishe tamaa wengine.....
 
Roho inauma ukiibiwa huku unaona lol .

Thanks Mkuu for your comments. Thanks kwa post yako ya kwanza JF kuwa kwangu. Mtu wa kwanza kukupigia thanks ni mimi pia. Thanks. Welcome to Jamii Forums.
 
Jamani tusianze kulaumu tujipange kusaidia hili,mimi nimepiga kituo cha Eliofoo Makongo juu jimbo la kawe,mambo yapo shwari na observers walikuwa wanfuatilia zoezi.
 
Ndugu zangu wana JF, suala la mawakala inaonekana linaweza kutia doa kwenye hatua hii ya mwisho ya kuikomboa nchi kutoka mikononi mwa manyang'au. Inaonekana chadema hawakuweka sawa suala la mawakala. Maeneo mengi matokeo yanaweza kuchakachulikwa kwa sababu tu ya uzembe wa aina hii. Tafadhali viongozi wa chadema lifanyieni kazi suala hili (kama uwezekano huo upo) kabla halijaleta madhara. Taarifa tunazopata kutoka jimbo la nyamagana Mwanza siyo nzuri.
 
Utaratibu uliopo hata mawakala wasipokuwepo sio tatizo hata kidogo... kila karatasi inaandikwa aliyepiga ni card namba ngapi... hili nilikuwa lisijue.
 
Nimefika Mapambano A Sinza, kuna tatizo la upungufu wa wasimamizi waelekezaji wa wapiga kura. Walibandika huko siku za nyuma list ya wapiga kura, leo wametoa pale yalipokuwa na kuyahamishia kwenye madarasa mbali mbali, lakini hakuna mtu wa kuelekeza wapiga kura hili jambo, hivyo watu wanafika na kusumbuka kutafuta majina yao, na wengine kukata tamaa, nimefanikiwa kujaribu kuelekeza watu kama kumi hivi, lakini sioni msimamizi wa kituo, askari na hao wasimamizi wa tume hawana usaidizi wowote wamekaa, kwa sasa watu ni wachache sijui itakuwaje pale kutakapokuwa na watu wengi.
Kama kuna mtu anamjua mtu wa tume anayeweza kusaidia hili ataarifiwe.


Mkuu tunakuomba sana uzidi kujitolea hapo ulipo. Tafadhali sana mkuu. unaweza ukawa ulikuwa na mipango yako miingine, lakini ukifanya hii kazi Mungu anaona!!
 



Nimepitia threads kadhaa hapa na kugundua kuwa kuna baadhi ya members humu wamepiga kura tayari lakini humo ndani waliwakuta mawakala waliowatilia shaka kuwa si wa CHADEMA au hawakuwakuta kabisa. Sasa badala ya kuendelea kupoteza muda, ni vyema mwenye wasiwasi aweke jina la kituo hapa ili hatua zichukuliwe haraka kabla ya zoezi la kuhesabu kura halijaanza. Orodhesheni vituo hapa:
1.
2.
3.
.
.
.
n.
Acheni ujinga wenu mlikuwa wapi kufuatilia na kusaidia majimbo yasiyokuwa na mawakala leo uchaguzi umeanza ndiyo mnajifanya kutaka kusaidi, wezi wakubwa, Jimbo la Ubungo halina wakala hata mmoja haya basi nendeni mkasaidie.
 
Ndugu zangu wana JF, suala la mawakala inaonekana linaweza kutia doa kwenye hatua hii ya mwisho ya kuikomboa nchi kutoka mikononi mwa manyang'au. Inaonekana chadema hawakuweka sawa suala la mawakala. Maeneo mengi matokeo yanaweza kuchakachulikwa kwa sababu tu ya uzembe wa aina hii. Tafadhali viongozi wa chadema lifanyieni kazi suala hili (kama uwezekano huo upo) kabla halijaleta madhara. Taarifa tunazopata kutoka jimbo la nyamagana Mwanza siyo nzuri.

Kaka jiandae kupokea matokeo hasi... hilo likukae kichwani.
 
SWALA LA MAWAKALA ni SHIDA KIDOGO KWAKWELI!

i am dissappointed!
 
Leo takribani saa moja kasoro nilikuwa nimeshapanga foleni, tayari kupiga kura. Walipofungua, na kazi kuanza, nilidadisi kwa haraka mazingira ya pale kituoni.

Nilichogundua ni kuwa kulikuwa na uzembe wa hali ya juu sana kwa mawakala wawili waliokuwa pale (sijui ni wa vyama gani). Walikuwa wamekaa kama mita tano, opposite na ofisa aliyekuwa anapokea kadi, na kuhakiki jina.

Walikuwa hawana karatasi yeyote mkononi, hali iliyomaanisha kuwa, wasingeweza kujiridhisha kama jina lililotamkwa lipo kweli kwenye orodha ya wapiga kura wa kituo kile.

Binafsi niliona si sawa, hivyo baada ya kupiga kura nikamwuliza ofisa mmoja pale, hawa mawakala wanajuae kuwa jina linalosomwa lipo kweli kwenye orodha, na kama kadi ya mpiga kura iliyowasilishwa ni yake kweli. Hakuweza kunijibu, niliondoka nikawasiliana na mgombea ubunge wa chama changu, akasema kweli hata yeye ameona katika vituo vingine. Nilijaribu kuzunguka vituo kama 16 vilivyokuwa jirani, nikaona hali ni ile ile.

Nilijaribu kumuelimisha mgombea udiwani mmoja akapita vituoni kuwakumbusha mawakala majukumu yao. Ameniambia kuwa amewaeleza, lakini sina hakika kama wataweza kuifanya hiyo kazi. Na hiyo ni kata moja kati ya kata 30 katika jimbo hili!
 
Utaratibu uliopo hata mawakala wasipokuwepo sio tatizo hata kidogo... kila karatasi inaandikwa aliyepiga ni card namba ngapi... hili nilikuwa lisijue.

Ndugu zangu, kushinda chama kikongwe kama ccm zinahitajika jitihada na tahadhari kubwa sana. Hivi mna taarifa kwamba NEC na ccm ni kitu kimoja? Mategemeo yetu wananchi tunaotaka ukombozi wa nchi hii yapo mikononi mwa "mawakala" watakaohesabu na kutia saini kwenye matokeo. Usipokuwa na wakala kwenye kituo au ukiwa na wakala goigoi ujue umeliwa. Ndiyo maana ninawakumbusha viongozi wa chadema kama wanaweza kufanya mawasiliano ya haraka basi wachukue hatua stahili ili kutoharibu mambo kwenye dakika hizi za mwisho za kuikomboa nchi yetu. Vinginevyo, udhaifu huu utatumiwa vizuri sana na manyang'au ambao hawalali hata usingizi kuhakikisha Dr. Slaa hakamati dola.
 
Ninachoomba kujua ni je mawakala wana nafasi gani za kutambua kama kweli anayeenda kupiga kura yupo kwenye orodha husika. Au wakati wa kuhesabu kura watakuwa wanacross check kwa kutumia orodha ya wapiga kura kwenye kituo husika? Tafadhali wana JF nifahamisheni.
 
Back
Top Bottom