Uzembe ulisababisha maafa mbagala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzembe ulisababisha maafa mbagala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by grndossy, Oct 15, 2012.

 1. grndossy

  grndossy JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Uzembe wa polisi ulisababisha uharibifu mkubwa uliosababishwa na waislamu waliovamia KKKT usharika wa Mbagala. Nasema haya kwa sababu polisi waliweza kudhibiti shambulio la kwanza la wavamizi hawa kwa mabomu ya machozi badala ya kuimarisha ulinzi katika eneo hilo waliondoka na kuacha eneo hilo katika ulinzi mdogo sana wa walinzi wa kampuni ya ulinzi wanaolinda katika siku za kawaida huku wakijua hao wavamizi walikuwa mitaani wakirandaranda kwa makundi.

  Wavamizi hawa walipoona polisi wameondoka ndipo walipokuja kwa makundi makubwa sana na wakawazidi nguvu wale walinzi wachache waliokuwa wamebaki katika eneo la kanisa hilo na ndio uharibifu huo mkubwa ulitokea na nusura kutoa hata uhai wa mchungaji kiongozi wa usharika huo pamoja na watumishi wengine.

  Kama polisi wangetimiza wajibu wao sawa sawa tatizo hili kubwa namna hii lisingetokea au lingetokea kwa udogo sio katika magnitude hii.

   
Loading...