PreGE2025 UWT yashangaa ukimya wa BAWACHA sakata la mwenezi wao kushambuliwa

PreGE2025 UWT yashangaa ukimya wa BAWACHA sakata la mwenezi wao kushambuliwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,499
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa imeonesha kushangazwa na kitendo cha Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) kutokutoa kauli yoyote baada ya Katibu Mwenezi wa BAWACHA Taifa, Sigrada Mligo (34), kushambuliwa kimwili.

Ikumbukwe kuwa, tarehe 25 Machi 2025, Mjini Njombe, iliripotiwa kuwa Mwenezi Mligo alifanyiwa shambulio la kudhuru mwili na mmoja wa walinzi wa chama hicho wakati wa kikao cha ndani kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akitoa tamko la jumuiya hiyo leo, Ijumaa, tarehe 28 Machi 2025, Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda, ameilaani vikali hali hiyo na kutoa wito kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kuendelea kumsaka mtuhumiwa na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

UWT imesema kuwa inashangazwa na kitendo cha BAWACHA kutokutoa kauli yoyote, na inasisitiza kuwa vitendo vya vurugu havipaswi kuvumiliwa na vinapaswa kupigiwa vita kwa nguvu zote.

Chokochoko za kishamba, inawahusu nini kama sio unafiki na kujikosha tu, kwani suala hilo si lipo polisi, mlitaka waseme nini. BAWACHA wanajitambua hawakulupuki.
For your information, BAWACHA wanataarifa zote za tukio hilo kuliko nyie mliodandia treni kwa mbele
 
Pia UWT msisahau kiongozi wa BAWACHA aliyetekwa, mamlaka za Polisi bado kimya hajasema wamefikia wapi katika uchunguzi

21 October 2024

KATIBU MWENEZI BAWACHA ADAI KUTEKWA NA KUPIGWA, ASIMULIA MAZITO YALIYOMKUTA :

Walijitambulisha Ni Polisi

View: https://m.youtube.com/watch?v=okZ0Rej9kIA
Katibu Mwenezi Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) Taifa, Bi. Aisha Machano, amedai kutekwa na kupigwa na wanaume sita na mwanamke mmoja waliojitambulisha kuwa ni Maafisa wa Jeshi la Polisi, wasiokuwa na sare wala vitambulisho katika Eneo la Kibiti, siku ya Jumamosi tarehe 19 /10/2024 wakidai kwanini baraza hilo lilichoma vitenge vilivyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hasani kama zawadi.

Wakuu,

Back
Top Bottom