Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 2,786
- 7,567
Wakuu,
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) imefanya Dua Maalum ya Shukrani na Kumuombea Rais Samia kwa Uongozi wake mahili katika kipindi cha Miaka Minne ulioleta maendeleo na neema kwa Taifa la Tanzania na kuongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Mustafa Rajab katika Msikiti wa Gaddafi Jijini Dodoma
Pia soma: Pre GE2025 - UVCCM Singida wafanya dua ya kumuombea Rais Samia
Dua hiyo Maalum imeandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali Mkoa wa Dodoma. Ambayo ilienda sambamba na hafla ya Iftar kwa makundi mbalimbali wakiwemo Wajane, Watoto yatima, Madrasat na waumini wa Dini ya kiislam.
Akizungumza baada ya Dua hiyo, Mwenyekiti Chatanda ametoa wito kwa Watanzania hususani Wanawake kuendelea kumuunga Mkono Rais Samia kutokana na dhamira yake Njema ya kuwaletea Watanzania maendeleo.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Mwenyekiti Chatanda amesema, Rais Samia ameimarisha Sekta ya Afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za Wilaya na za Rufaa pamoja na uwepo wa Vifaa Tiba sanjari utekelezaji wa miradi mikubwa katika sekta ya nishati, usafirishaji, Maji pamoja na Elimu"
Ameongeza kuwa UWT ina kila sababu ya kumshukuru na kumuombea Rais kwa kazi hizo nzuri. Kadharika ametoa wito wa tujitokeza Kwa wingi Kushiriki Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba 2025 kumchagua na kumpa ushindi wa kishindo Mpendwa wetu Rais Samia"