Uwt- ccm ficheni upumbavu wenu msifiche hekima zenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwt- ccm ficheni upumbavu wenu msifiche hekima zenu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  UWT zibeni mpasuko wenu, malumbano hayana tija


  LISEMWALO lipo na kama halipo linakuja. Hivi karibuni, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umekuwa gumzo kutokana na madai ya kuwepo mgogoro unaohusisha viongozi wa juu.

  Yapo mengi yanayosemwa juu ya viongozi hao ambao ni Mwenyekiti wa umoja huo, Sophia Simba na Katibu Mkuu wake, Husna Mwilima.

  Inawezekana yanayosemwa ama yasiwepo au yakaongezwa chumvi. Lakini hilo haliondoi ukweli kwamba hali ni tete katika umoja huo.

  Mimi siyo hakimu wa kubainisha hali ilivyo na kutoa hukumu. Lakini hakuna ubishi kwamba mazingira yanaonesha kwamba mpasuko ndani ya umoja huo upo.

  Kwa mfano, kitendo cha baadhi ya viongozi wa umoja huo juzi kutoa taarifa ya kukanusha kuwepo mgogoro, bila kumhusisha Katibu Mkuu, Mwilima anayetajwa kuwa sehemu ya mgogoro huo wakati alikuwepo ofisini, ni mazingira tosha kuonesha kwamba lipo tatizo.

  Inafahamika wazi kwamba UWT ni umoja wa kichama. Lakini katika kufuatilia historia yake, ni umoja ambao unahitaji kuwa na nguvu kubwa kwa kuzingatia kwamba unawakilisha chama tawala chenye sera za kitaifa katika kuwakomboa wanawake wote.

  Nanukuu hotuba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete katika ufunguzi wa mkutano mkuu maalumu wa UWT uliofanyika Dodoma, Julai 27, 2007: “UWT ni chombo cha ukombozi wa mwanamke wa Tanzania na taifa kwa jumla.

  Ni chombo cha kupigania haki na maendeleo ya wanawake na jamii kwa ujumla." Chombo hiki historia yake inatajwa tangu enzi za kupigania uhuru na ukombozi wa nchi kutokana na wanawake kusimama kidete, wakiwa bega kwa bega na wanaume kupambana na ukoloni na utawala wa kisultani.


  Wapo wanawake wengi waasisi wa UWT ambao sifa zao tunaendelea kuzisikia hadi leo. Kwa kuzingatia hilo, Rais Kikwete katika mkutano huo aliendelea kusema, ‘Jukumu la msingi la UWT kwa sasa ni kuendelea kutumia uhalali huo wa kihistoria na mtandao mkubwa ilionao nchi nzima kuendelea kupigania haki, usawa na maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya wanawake wa Tanzania na jamii zao wanamoishi.

  Siyo nia yangu kuainisha historia ndefu ya UWT, mafanikio au changamoto zinazoukabili umoja huo kwani wahusika, hususan viongozi, wanafahamu ukweli.

  Hiki ni kioo pia cha wanawake wa nchi nzima japokuwa hata vyama vingine vya siasa vina vyombo vyao.

  Ndiyo maana tunaona Mwenyekiti wake, Simba, ni kiongozi wa kitaifa tena katika nafasi nyeti ya utawala bora.


  Kwa mantiki hii, ina maana inapotokea aina yoyote ya mpasuko, mgogoro au kuaibishana baina ya wanachama, suala hilo haliwezi kuishia ngazi ya umoja huo, bali linavuka mipaka hadi serikalini.


  Kwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora), Simba ndiye mwenyekiti na ambaye amekuwa akihusishwa katika mgogoro huo, ni vyema atumie busara na nguvu ya wadhifa alio nao serikalini kumaliza hali hiyo.

  Pamoja na kwamba migogoro siyo jambo geni katika taasisi au mkusanyiko wowote wa watu, lakini ni vyema UWT isikubali kuchafua sifa yake.

  Umoja huo uepuke kutoa nafasi kwa jamii inayoamini katika mfumo dume, kuibeza UWT kwa kuhalalisha dhana potofu kwamba wanawake hawapendani na wanaoneana wivu.

  Hatua zichukuliwe haraka kukomesha hali hii kwani mwanamke wa kijijini hana manufaa yoyote na malumbano haya.


  Vikao vibaki kuwa vya kujadili masuala yenye tija ya kumwendeleza mwanamke na si vya kusutana na kupashana.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  UWT=CCM=complications!

  wanayoongea hawa wanawake mtaweza kuyajadili humu! wakati Sofia Simba anamwaga upupu wake wanampigia makofi, JF mnasema ajiuzulu

  mtawaweza hawa!

  Kabali ya mikono inakunyima pumzi, kabali ya between legs inakunyima pumzi, akili, uhuru, utu...name it

  Tuwaache hawa jamani
   
 3. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Mkuu


  hivi naweza kupindisha hii ishuu, hivi-
  • Apolitical ?
  • Social class nightmare?
  • A socialeconomic organ at the helm of power mongering?
  What has CCM got to do with it? hekima au upumbavu?
  Wanawake siku zote kusutana tu na kupashana-wataelewana "frienemies" hawa.
  Apolitical.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  ruksa
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  kwa style hii ya hapo juu nahisi kizunguzungu cha ajabu watu kama wakina pdidy bado wanangangania kadi za uvccm...ccm
  kazi kweli kweli
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  am kid'n br
   
 7. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kama kiongozi wake ni Sophia Simba unategemea nini zaidi ya hayo yanayojiri? Je unadhani SS anabusara yakuweza kusuluhisha migogoro ndani ya UWT zaidi ya kuikoleza?
   
 8. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sasa wewe mtowa Mada unataka WAZAWA wapandwe vichwani ?
   
 9. M

  Mchili JF-Expert Member

  #9
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
   
 10. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nani mwenye habari zozote? Huyu mama alifuata ule ushauri wa Mzee Malechela, au aliamua kuukalia?
   
 11. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo ngoma kwisha ni kuwatimuwa wote wawili,kwani kwa jinsi nijuavyo ni watu wa mipasho sana watu hawa.
   
Loading...