Uwingi wa damu mwilini

Uwingi wa damu mwilini

INSONSILE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,872
Reaction score
2,740
Naomba kujuzwa, uwingi wa damu mwilini rating zake huwa ikoje?

Nimekuwa nikisikia kuwa kwa mtu wa kawaida isipungue 12 au 13.

Hizo namba tafsiri yake ni nini? Yaan 13 juu ya ngapi?

Na kiwango cha juu kabisa ni ngapi?

Mfano, unapoambiwa na daktari kuwa damu yako imezidi, huwa ni kuanzia ngapi ndo inakuwa imezidi? Na standard inayotakiwa ni kuanzia ngapi hadi ngapi?
 
Naomba kujuzwa, uwingi wa damu mwilini rating zake huwa ikoje?
Nimekuwa nikisikia kuwa kwa mtu wa kawaida isipungue 12 au 13...

wingi wa damu au kwa lugha ya kitabibu ni Haemoglobin(Hb)!
Kipimo chak huwa katika SI Units za gm/dl i.e grams per deciliter
Kazi ya Haemoglobin ni kubeba Oxygen kwenda sehemu mbali mbali za mwili na kiungo muhimu kinachoitaji Glucose na Oxygen nyingi ni Ubongo ila hata misuli huitaji oxygen ili kuunguza glucose ili uweze kupata Nguvu e.g Hata gari uitaji air/oxygen kuunguza Mafuta ili gari lipate nguvu ya kutembea.

Ndo maana ukiwa na damu chache/Hb ndogo unakua mchovu unasikia kizunguzungu na wakati mwingine hata kuzimia.
Normal Hb level utegemeana sana sana na jinsia e.g kwa mwanamke Normal level yao iko chini zaidi ukilinganisha na wanaume.
Pia normal levels utegemeana na teknolojia inayotumika mahabara moja na nyingine!
Ili si kuchanganye sana chukua kwamba normal Hb level ni 12-16.5gm/dl

Damu yako inaweza kupungua iwapo unaumwa kwa mda mrefu,Kupoteza damu sana e.g ajali au kwa wamama wakati wa kujifungua au wanawake wanaoingia period zilizopitiliza kawaida,tatizo la kutokula vyakula vyenye madini chuma kama mboga za majani na maini.

Damu chini ya 12g/dl kwa wanaume au 11g/dl kwa wanawake hili ni tatizo huitwa Anaemia
Damu ikiwa chini 6g/dl utaitaji kuongezewa damu au wakati mwingine ukipoteza damu nyingi ambayo imepunguza 2g/dl kutoka kwenye normal yako itakubidi kuongezewa damu.

Damu juu ya 6gm/dl---11gm/dll kama haikupi shida yoyote inaweza kutibiwa kwa kula vyakula vyenye madini chuma(Iron) kama mboga za majani,maini n.k au ukatumia dawa za kisasa zenye madini chuma ndani.

Damu nyingi ambayo inatishia afya yako kwa kitaalamu Polycythemia ni pale unapokua na Hb juu ya 16.5gm/dl kwa mwanamke au 18gm/dl kwa mwanaume.

Damu hii inakua nzito kiasi kwamba inakua sluggish kwenye mishipa na inaweza kuganda na kuenda kuziba mirija kama ya ubongo na inaweza kukupa stroke. Unaweza kulinganisha hii na maji na Oil kipi ukimwaga kitakua kinatembea kwa urahisi.

Ngoja niishie hapo nsikujaze na mambo ambayo hayatakusaidia!

kwa sasa nakaribisha maswali!
 
MIMI pia mkuu damu inapungua nmepima sicklecell sina nimeongezewa damu mara nne na sasa naona dalili zilele kuchoka moyo kwend kasi, kizunguzungu nikiamka au kuchuchumaa kwa mda mref...X-ray nilipiga ikaonyesha moyo umekuw mkubwa pia FBP nimepima iko normal,,,,sas damu inapungua nann.. matunda mboga za majan nmekula sana yaan nmefata ushaur wa daktar lakn bado tu...nisaidien wakuu
 
hauwezi kuwa na ndamu ndogo afu FBP ikaonesha iko normal!
Walau kipengele cha Hb kitakua chini!
Lazima kuwepo na sababu kwa nn damu yako inakaa chini!
Au iron reserves zako ziko chini?
Ungefanya na Iron studies!

Pili ukiwa na tatizo la hivi inakubidi umeze Dawa za kitaalamu za kuongeza damu e.g Ferrous Sulphtae + Folic Acid (FeFol) usiteegemee peke yake eti mboga za majani, ili uweze kurejeshe Iron reserves zako inaitaji utumie hizi dawa kwa 6-12months non stop!

Je hauna ugonjwa mwingine au hauna dawa unazotumia za mda mrefu?
 
hauwezi kuwa na ndamu ndogo afu FBP ikaonesha iko normal!
Walau kipengele cha Hb kitakua chini!
Lazima kuwepo na sababu kwa nn damu yako inakaa chini!...
ugonjwa nilionao kwa sasa nikwenye viungo kama mikononi kwenye maungio nasikia kama vtu vnasagana pia mgongo ukikaa kdogo ukijinyoosha unasikia kha kha kha kwenye kiuno pia hata kweny vdole vya miguu na mikonon
 
hauwezi kuwa na ndamu ndogo afu FBP ikaonesha iko normal!
Walau kipengele cha Hb kitakua chini!
Lazima kuwepo na sababu kwa nn damu yako inakaa chini!...
pia mkuu nifahamishe folic acid inahusu nn?? pamoja na uhusiano na damu
 
hauwezi kuwa na ndamu ndogo afu FBP ikaonesha iko normal!
Walau kipengele cha Hb kitakua chini!...
Pia mkuu vp kuwa na moyo mkubwa kunaongeza upungufu wa damu kwa maana hili tatzo ni la mda mrefu,, yaan unasikia moyo umelipuka ghafla au unasikia kitu knachoma kweny moyo kama kchomi flan
 
wingi wa damu au kwa lugha ya kitabibu ni Haemoglobin(Hb)!
Kipimo chak huwa katika SI Units za gm/dl i.e grams per deciliter...

Asante sana mkuu umekata kiu yangu. Mimi ni mwanaume, na nimepima nikaambiwa nina 17.4, na yule aliyenipima akaniambia damu yako ni ya kutosha sana. Kilichonipeleka kwenda kupima nilikuwa nahisi kuchoka, kichwa kinauma, alafu sina malaria ndo niaamua kupima uwingi wa damu.
Kwa hiyo kwa lugha rahisi natakiwa nipunguze damu siyo?
 
dah kwel binadam tunatofautiana,,yaan wewe unahitaj kupunguza damu mm nahita iongezeke doh
 
MIMI pia mkuu damu inapungua nmepima sicklecell sina nimeongezewa damu mara nne na sasa naona dalili zilele kuchoka moyo kwend kasi, kizunguzungu nikiamka au kuchuchumaa kwa mda mref...X-ray nilipiga ikaonyesha moyo umekuw mkubwa pia FBP nimepima iko normal,,,,sas damu inapungua nann.. matunda mboga za majan nmekula sana yaan nmefata ushaur wa daktar lakn bado tu...nisaidien wakuu
Kuna vingine vingi vya kupunguza damu ambavyo hujapima , minyoo, hematological malignancies, multiple myeloma fika hospitali kubwa wafanye vipimo vya kutosha FBP peke ake haitoshi.
 
Pia mkuu vp kuwa na moyo mkubwa kunaongeza upungufu wa damu kwa maana hili tatzo ni la mda mrefu,, yaan unasikia moyo umelipuka ghafla au unasikia kitu knachoma kweny moyo kama kchomi flan
Moyo mkubwa umefanya kipimo gani kikaonesha hivo!
Hizo dalili zinaonesha una Ischemic heart disease.
 
Hizo nazo zinasaidia kwenye utengenezaji wa cell mwilini ikiwemo cell nyekundu za damu ambao ndo msingi wa mjdala huu!
Itafaa zaidi kama ukarudi hospitali yenye hadhi kubwa zaidi kama hospitali ya wilaya au mkoa ufanye FBP isomwe na uliweza fanya na Iron studies kabisa.
pia mkuu nifahamishe folic acid inahusu nn?? pamoja na uhusiano na damu
 
mama yangu ana umri wa miaka Zaidi ya 70. Kila mara analalamika kuwa anasikia kizunguzungu. Tatizo hili limemuanza miaka mitatu iliyopita. Je anaweza kuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani?
 
Asante sana mkuu umekata kiu yangu. Mimi ni mwanaume, na nimepima nikaambiwa nina 17.4, na yule aliyenipima akaniambia damu yako ni ya kutosha sana. Kilichonipeleka kwenda kupima nilikuwa nahisi kuchoka, kichwa kinauma, alafu sina malaria ndo niaamua kupima uwingi wa damu.
Kwa hiyo kwa lugha rahisi natakiwa nipunguze damu siyo?
Nenda kachangie damu kwenye bank ya damu muhimbili ...alafu fanya mazoezi walau nusu saa kwa siku kukimbia,kuruka kamba nk
 
wingi wa damu au kwa lugha ya kitabibu ni Haemoglobin(Hb)!
Kipimo chak huwa katika SI Units za gm/dl i.e grams per deciliter
Kazi ya Haemoglobin ni kubeba Oxygen kwenda sehemu mbali mbali za mwili na kiungo muhimu kinachoitaji Glucose na Oxygen nyingi ni Ubongo ila hata misuli huitaji oxygen ili kuunguza glucose ili uweze kupata Nguvu e.g Hata gari uitaji air/oxygen kuunguza Mafuta ili gari lipate nguvu ya kutembea...
Nimependa ulivoelezea mkuu.. Nina kaswali kidogo... Je Hio Hb inahusiana na blood group??

Cc Smart911
 
kuna usemi tunasema mtaani kuwa ulaji wa limao kwa wingi pia huwa una dilute damu inakuwa nyepesi sana, ni kweli??
 
Back
Top Bottom