Ndugu zangu nchi hii kwa hivi sasa sijui tunakokwenda kwani matatizo kama haya yanapotokea tunapenda kulaumu vyombo vilivyoweka kusimamia lakini vyombo hivyo vikifanya kazi zake tunavilaumu sana. Kwa mfano siku ya j'mosi iliyopita nilipanda basi la mbeya express kuelekea mbeya na tulipofika morogoro askari aliingia ndani ya basi na kuomba manifest. baada ya kupewa akafanya random check kuthibitisha kama kweli majina ya wasafiri yana kubaliana na list ya manifest. askari huyo alikuta abiria kadhaa ambao majina/na ya tiketi hazikubaliani na list ya manifest hivyo akaamuru kondakta alipte faini palepae stendi. lakini cha kushangaza abiria walilalamika sana kutokana na uamuzi huo wa polisi tena kati ya waliolalamika ni wasomi wa chuo kikuu cha teku ambao walibeba bango hilo hadi likageuka kuwa la kisiasa.
Tanzania ni zaidi tuijuavyo [you are damned if you do and you are damned if you dont] god have mercy on us