ng'adi lawi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2014
- 2,956
- 1,114
Namshauri Meja Generali Gaudence Milanzi katibu mkuu wizara ya mali asili na utalii aanze kupiga vita ujangili kwa kupiga marufuku uwindaji wa kitalii wa kuua wanyamapori na badala yake ahamasishe upigaji wa picha tu. Kampuni moja kubwa ya Arusha TGT imeanza kupiga picha badala ya kuua wanyamapori na inatengeneza faida kubwa kwa kuuza hizo picha. Mamlaka mpya ya wanyamapori inaweza kufanya kazi ya Upunguzaji (cropping) wanyamapori wanaozidi maeneo ya malisho. Kazi hii ilikuwa ikifanywa na TAWICO ambayo ilibinafsishwa kifisadi.