Binti Magufuli
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 7,479
- 5,161
Nimeona nilete hii hoja huku kwenye wengi badala ya kuipost kwenye jukwaa la dini ili meseji ifike kwa wahusika kirahisi. Ni hivi, mbona mada za dini kule kwenye jukwaa husika hazina wachangaiaji wengi? Member wenye access ya jukwaa ni wengi ila mada zikipostiwa utakuta zina wachangiaji hata 10 saa nyingine hawafiki! Mfano mzuri ni mada ya imani na miujiza aliyoposti dada/kaka mmoja (nimemsahau jina) toka juzi hadi muda huu ina michango 3 tu! Hii ni hatari kubwa kwa kizazi cha leo kwani shetani ameamua kuwatawala na kuhakikisha mnabanwa na mada za ulimwengu huu na kuona mada za kiroho kama hazina mshiko! Amelaaniwa yeye ambae hatangulizi mambo ya kiroho mbele......., nimefikisha ujumbe na ukumbuke mjumbe hauwawi!!!
Kule huwa napita tu ni matusi tu nashukuru sijawahi kuchangia chochote.
Tunashindwa kujua kwamba tukiangalia kwa undani
Hakuna au wachache sana waliochagua imani ukubwani
It was by chance tumezaliwa kwenye familia zinazoamini hicho tunachokiamini kwa sasa
Kwa hiyo, mtu yeyote anaweza kuwa chochote kutokana na kwamba amezaliwa wapi.
Wasichangia jukwaa la dini labda ni kwa sababu hawaamini hizo dini, na uwezekano mkubwa ni kuwa hawaamini na huyo shetani
Kwa hiyo mnafata tu bila ya kutafuta ukweli umesimama wapi?
Na ikiwa ni hivyo, majadiliano na watu wanaofata mkumbo tu, yana faida kweli?
Umewahi kusikia kuhusu 'independent investigation of the truth?'Kama ni mada inayokuhusu kwa nini usichangie??
Mwehu akikupiga na yai vinza unataka urudishe??
Wewe changia, akikutukana mpishe kama huoni
Hata rudhia siku nyingine.
Wengine wapo kwa ajili ya ku-undermine imani za watu
Wengine hawana kabisa imani
Tunashindwa kujua kwamba tukiangalia kwa undani
Hakuna au wachache sana waliochagua imani ukubwani
It was by chance tumezaliwa kwenye familia zinazoamini hicho tunachokiamini kwa sasa
Kwa hiyo, mtu yeyote anaweza kuwa chochote kutokana na kwamba amezaliwa wapi.
Mi nadhani tukiheshimu hili
Litatusaidia kuheshimu imani za wengine
Kama ambavyo sio kila anaeenda kanisani anaamini anachofundishwa kule na kujaribu kuyafanyia kazi kwenye maisha yake , na sio kila asieenda haamini/hafuati maandiko ndivyo ilivyo hiyo ya uchangiaji. Yote ni maamuzi ya mtu binafsi. Hamna haja ya kuchangia ili nionekane sijalaliwa na shetani kichwani, ila kuna haja ya kufanya yale yanayoniridhisha mimi mwenyewe na Mungu wangu.
Umewahi kusikia kuhusu 'independent investigation of the truth?'
Hili nalo linahitaji mjadala....mpaka upo wapi?....mambo ya kiroho yanaishia wapi na yale ya ulimwengu yanaanzia wapi?...hasa ukizingatia 'ukweli' kuwa Mungu ndiye 'muunba wa vitu vyote'!....mnabanwa na mada za ulimwengu huu na kuona mada za kiroho kama hazina mshiko!...
Nakubaliana na wewe
Usichangie kwa sababu hujisikii kuchangia
Lakini si kwa sababu watu wengine watakutukana
kwa hiyo unaacha kuchangia kuepusha shari
Siku zote huwezi linganisha utamu wa nyama na chumgwa
Haitaleta maana
Linganisha chungwa kwa chungwa na nyama kwa nyama
Anayeamini na asiyeamini mjadala pekee naouona wanaweza wakashare ni kuulizana kwa nini unaamini na kwa nini wewe huamini
Ikishaningia kwa waaminio kujadili mambo wanayoyaamini sioni ni kwa point gani asiyeamini anaweza akachangia zaidi ya kuheshimu mijadala yao. Wanakuwa wanaongea lugha tofauti kabisa hapo.
Sasa kwa anayetaka kuutafuta huo ukweli wa aidha kuna haja ya kuamini au la aende kwenye mijadala hiyo itampa majibu ya maswali yake.
Sidhani ni sahihi kusema 'Uamini kwa kufuata mkumbo' ni sawa sababu hulazimishwi na wala hukataliwi kutafuta kweli unayoitaka.
Ita apple by apple theory.