Mkuu hiyo gari Mwanza inafika lakini ni
lazima uende spidi za kawaida pia uwe
na vituo vya kutosha njiani kusimama.
Ili kuruhusu injini kupoa kiasi lakini huko
njiani utakuwa unakimbizana kwa spidi na
usitegee kamwe kuiona Mwanza.
Thanx bro,,,uwezo wake wa kutembea bila kusimama ni km ngapi mkuu?manake nawaza kama nitalazimika kusimama moro,dodoma, singida na shinyanga,,,sasa si nitafika baada ya siku mbili mkuu,,au kupumzisha ni muda gani?
Inafika pasi mashaka yote kama gari ni nzima na imefanyiwa service vizuri. Nshaenda Arusha na hicho kidude nilisimama maro moja tu Korogwe pale kupata msosi na mzinga wa konyagi.
Mkuu washa gari moto hiyo, tambaa zako Rock City. Angalizo ni moja tu kuwa kama gari ni nzima na inafanyiwa service vizuri. Bahati nzuri zaidi ni kuwa hilo angalizo si kwa ajili ya Passo tu, hata Land cruiser, Range Rover, Helicopter na chochote kitumiacho mafuta, shurti kifanyiwe hiyo makitu.Nashukuru sana mkuu,,manake kuna watu walikuwa wananiambie eti cc 1000 ni kama pikipiki tu,,duu nikasema sasa imekula kwangu.
Mkuu magari hayahitaji kupumzika labda dereva awe amechoka.Mkuu hiyo gari Mwanza inafika lakini ni
lazima uende spidi za kawaida pia uwe
na vituo vya kutosha njiani kusimama.
Ili kuruhusu injini kupoa kiasi lakini huko
njiani utakuwa unakimbizana kwa spidi na
usitegee kamwe kuiona Mwanza.
Kweli usichokijua...usiku wa kiza. Badala ya kuwashangaa watu wanaokwambia gari inabidi uipumzishe itapata moto sana, unanishaangaaa miye? Kwa taarifa yako gari ikishafikisha operating temp(about 5 - 10min) haijarishi umbali utakao endesha joto litakuwa likicheza anga hizo hizo, unless injini yenyewe mbovu. Unaweza endesha mwezi mzima bila kulizima na gari itakuwa safi kabisa.Acha bangi mkuu,,wenzio tumeshaacha.