Uwezo Duni TBS Unaligharimu Taifa

Mamlaka ivunjwe.

Tuunde mamlaka moja kwa EAC. Itakuwa rahisi kugharamia mafunzo yao na kupata vifaa na miundombinu inayohitajika katika kupima na kutambua ubora wa bidhaa.
Breki za mbele za kigari changu ziliisha nikaenda mjini kwa madealer pair inarange kati ya elfu 40 hadi laki. Ukienda Toyota Tanzania breki similar ni 270,000 aisee ukiifunga unaona tofauti. Hakuna mkwaruzo kama imepakwa mafuta! Bidhaa substandard ni majanga.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Yote tisa,
Kumi hujauziwa kadet nzuri ya kung'aa alafu ukiweka kwenye maji tu inageuka rangi, kama ilikuwa ya kijivu inakuwa nyeupe au njano
Teh teh

Ova
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Yote tisa,
Kumi hujauziwa kadet nzuri ya kung'aa alafu ukiweka kwenye maji tu inageuka rangi, kama ilikuwa ya kijivu inakuwa nyeupe au njano
Kwenye nguo kuna majanga zaidi
 
Ha ha ha! Hakuna tairi ya maana ya gari ndogo ndogo inauzwa chini ya TZS 350,000.
Acha upotoshaji,
Hizo bei kwa gari ndogo (rimsize 15-17) labda kwa Bf Goodrich.

Ila hizi za kina Linglong ,Goodride n.k nyingi zinacheza humo humo kwenye 140,000-160,000
 
Acha upotoshaji,
Hizo bei kwa gari ndogo (rimsize 15-17) labda kwa Bf Goodrich.

Ila hizi za kina Linglong ,Goodride n.k nyingi zinacheza humo humo kwenye 140,000-160,000
... Yokohama ex Japan; Michelin; and the like.
 
Ukitaka kitu bora lazima ujikunjue, China anakutengenezea zana kulingana na pesa ulonayo mkononi.
 
Mamlaka ivunjwe.

Tuunde mamlaka moja kwa EAC. Itakuwa rahisi kugharamia mafunzo yao na kupata vifaa na miundombinu inayohitajika katika kupima na kutambua ubora wa bidhaa.
Wazo zuri Mimi naona kuimarisha ya kwetu ni vizuri zaidi kwasababu bidha nyingi zinagusa maisha yetu,mfano simu nyingi ni feki na vipuri vyake
 
Niliwahi uliza hilo TBS,wakaniambia wao Wana deal na Standard na si class ya vitu,mathalani kama ergonomic imefikiwa Basi imemiti standard according to them ni standard,material ni KAZI yako mnunuzi
 
Juzi juzi nimenunua Disk za brake za gari, ndani ya siku tatu gari ikaanza kutoa milio ya ajabu, kufungua kwa fundi zile disk mpya zimevunjika!
Na hapo sijakwenda safari yeyote zaidi nyumbani na kazini tu.
 
Umenena vema, tiles za goodwill ni takataka kabisa,tiles zimepishana size madhalani tiles ya 40cmx40cm zimepishana zingine 40.2cm mpaka 40.3cm zingine ni 39.8cm.

Kwakweli sujui TBS wanafanya nini?
 
Mamlaka ivunjwe.

Tuunde mamlaka moja kwa EAC. Itakuwa rahisi kugharamia mafunzo yao na kupata vifaa na miundombinu inayohitajika katika kupima na kutambua ubora wa bidhaa.
Hapa unadhani EAC Partner states wote wana nia nzuri baina yao za kiuchumi? Acha inferiority complex TBS inafanya majukumu yake vizuri mno, tatizo pia inawezekana uelewa wako juu ya mambo ya ubora na usalama upo chini. kuna bidhaa bora inatengenezwa kwa ajili ya kuishi mwezi pia kuna bidhaa bora kama hiyo hiyo na yenye usalama huo huo inatengenezwa kwa ajili ya kuishi mwaka. Wewe unapoingia sokoni kichwa kichwa na kulanguliwa bidhaa ya bei rahisi na ya muda mfupi TBS inahusikaje? Jiongeze; TBS inafanya kazi kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kimataifa
 
TBS wanatakiwa wapime ubora wa kiwango cha bidhaa iliyoko dukani na siyo wanayopelekewa na mtengenezaji. Tanzania ni mwanachama wa IBS (Shirika la Viwango la Kimataifa) hata hivyo bidhaa zetu hazikidhi viwango, TBS inapoweka alama yake kwenye vibiriti na mikate ambayo haina ubora hata kidogo ndipo utajua TBS haina manufaa kwetu kwani imekuwa ikipitisha ubora wa viwango kisiasa.
 
Mamlaka ivunjwe.

Tuunde mamlaka moja kwa EAC. Itakuwa rahisi kugharamia mafunzo yao na kupata vifaa na miundombinu inayohitajika katika kupima na kutambua ubora wa bidhaa.
Wazo hili wataalam wetu wa UDSM wanahofia wataalam wetu watamezwa.
 
Nilichokielewa kwa mleta mada nikuwa:

Sio kila mtanzania anaweza kujua thamani ya bidhaa flani, na si bidhaa za ujenzi tu,, mfano kunakipindi serikali iliamua kudhibiti ubora wa simu zinazoingizwa nchini, lengo lilikua ni kwa usalama wa raia na nchi kwa ujumla.

Kwa hio nijukumu la mamlaka Wakati mwingine kudhibiti Jambo hata likionekana kuwa linamanufaa lakini inapaswa kupima kati ya manufaa yatakayopatikana na hasara zinazoweza kutokea hasa za kiafya.
 
IBS kweli ni shirika la viwango la kimataifa? watanzania wenzangu tujenge utamaduni wa kujisomea na kujenga uelewa kwa mambo ya msingi yanayotuzunguka. Tunayotabia mbaya ya kumtafuta wa kumtupia lawama baada ya sisi wenyewe kufanya uzembe.
 
Shika unachokielewa lakini ni hivyo au unaijua B I S ndiyo hiyohiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…