Wadau,
Naombeni msaada juu ya hili,mm ni mtumishi wa Umma ni mtumishi mpya,kwa bahati mbaya sikupata maelezo ya kutosha juu ya mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii nimejikuta nimejiunga na mfuko ambao hauna mafao bora hivyo nataka kuhama kuhamia mfuko mwingine,swali langu je inawezekana kwa mtumishi wa umma kufanya hivyo,kama inaezekana taratibu zikoje?
Kuna taarifa kuwa kuna sheria za mifuko ya jamii zinazokusudiwa kanzishwa lengo ikiwa ni kumbana mteja- mwanachama wa mifuko hiyo. Nijuavyo mimi mifuko hii ilianzishwa ili kumuudumia mteja aliyejisajili, na mifuko hii inawajibika moja kwa moja kwa wateja wake. Swali ni je ikiwa kuna sheria zinakusudia kumbana mteja kiasi kwamba akisha jiunga na mfuko mmoja wapo kati ya hiyo mifuko hataruhusiwa kuhama,au kusitisha mkataba mpaka kwa kiwango cha mda flani na kwa kutimiza kiwango fulani cha mchango wake....mimi naona si sawa..Je sheria hizi ni kwa manufaa ya nani na zinakusudia nini?
WATANZANIA TUSIKUBALI..
mi nina miezi sita sasa toka nimejitoa kwenye mfuko flani. na sasa nimepata kazi serikalini naweza kuhamia mfuko mwingine? na ni mfuko gani mzuri kiuchangiaji na mafao naomba ushauri wenu wadau
nipo ppf mfuko mbovu kuliko yote duniani
Yeah unaweza, mfuko mzuri ni PSPF na LAPF
asante sana kwa ushauri. nitahama faster.
Haiwezekani