Uwekezaji - Sehemu ya kwanza

Ms Fatma

Member
Jan 26, 2019
16
19
UTAMBULISHO KUHUSU UWEKEZAJI
Uwekezaji ni operesheni ambayo baada ya uchambuzi wa kina inaahidi kulinda mtaji pamoja kuleta marejesho (ya kifedha) kutoka kwenye mtaji huo.

Maneno ya kuzingatia hapa ni “uchambuzi wa kina” “kulinda mtaji” na “marejesho”.

Bila vitu hivi vitatu basi operesheni hiyo haijakidhi vigezo vya kuwa “Uwekezaji”


UWEKEZAJI (INVESTING) VS UTEGESHAJI (SPECULATION)

Dhana ya uwekezaji ni nadharia ambayo ina utata bado kwenye uelewa wa watu wengi ikiwa inachanganywa na dhana ya speculation (kubet, kutegesha).

Operesheni yeyote ambayo haijakidhi maana ya uwekezaji iliyopo hapo juu ni SPECULATION.

Mfano unaweka fedha katika opresheni ambayo hujafanyia uchambuzi wa kutosha, ama huna uhakika kama operesheni hiyo italinda mtaji wako, ama kuleta marejesho yeyote, basi wewe ni speculator (mtegeshaji) sio muwekezaji.

Hivyo watu wengi wanaodhani ni wawekezaji mara nyingi huwa ni wategeshaji tu.


AINA ZA WAWEKEZAJI.

Wawekezaji wanaweza kugawika makundi mbalimbali kutegemea na kigezo kilichotumika.

Tukitumia kigzo cha 'risk'

. CONSERVATIVE INVESTORS ni wawekezaji ambao wanaogopa risk hivyo wanawekeza kwenye operesheni ambazo marejesho yake yana uhakika Zaidi na kiwango kidogo cha risk, pia wanapenda kuwekeza kwenye uwekezaji wa muda mfupi.

Pia wanatumia sana dhana ya uwekezaji iitwayo diversification, yani kuwekeza sehemu mbali mbali ambazo ni tofauti kuepuka risk. Mategemeo ni kwamba sehem moja ikifeli nyingine itafanya vizuri hvyo upunguza hasara kwa muwekezaji.

Watu hawa hupenda kuwekeza kwenye vitu kama t bills na bond ambazo zina amarejesho ya uhakika.

Faida yao ni kuwa mara nyingi marejesho yao ni ya uhakika. Na hasara ni kuwa wanapata marejesho madogo ukilinganisha na aina nyingine ya wawekezaji amabayoo ni aggressive investors.

AGGRESSIVE INVESTORS. Ni wawekezaji ambao wapo tayar kupambana na risk hivyo wanajtosa Zaidi kwa kuwekeza sehemu ambazo zinarisk risk kubwa wakiwa wanategemea marejesho makubwa kutokana na uwekezaji wao.

Hawa ni wale tunawaita ‘real RISK TAKERS’. Wawekezaji wa aina hii huwekeza kwenye uwekezaji wa muda mrefu, na pia wengine wanaendelea kufanya “focus investing”, yaani wanawekeza kwenye uwekezaji wa aina moja ama sekta moja ambayo wanaamini itafanya vizuri achilia mbali risk iliyopo.

Watu hawa wanakutaka na kitu kinachoitwa high highs na low lows, yani wakipata wanapata kweli na wakikosa wanakosa kweli.

Wawekezaji wa aina hii wanasimama na msemo maarufu” the higher the risk, the higher the return”

MAANA YA MANENO

RISK: kwa Kiswahili ni hali iliyoambatana na hatari. Katika uwekezaji hatari hiyo ni kule mambo kutokwenda sambamba na vile muwekezaji alivyotarajia baada ya kufanya uchambuzi wake.

Baadhi ya risk ambazo zinaweza tokea katika uwEkezaji ni kupata marejesho madogo au kutopata kabisa, Kupoteza mtaji na kadhalika.
 
So forex trading is betting isn't it..??
FOREX TRADING KWA KIWANGO KIKUBWA NI 'SPECULATION'. HII INATOKANA NA ASILI YA BIASHARA HIYO KWANI 'VOLATILITY' (MABADILIKO YA THAMANI YA FEDHA) NI MAKUBWA NDANI YA MUDA HUSIKA. HIVYO WAFANYABIASHARA WENGI WALIOPO KWENYE FOREX ESPECIALLY WANAOTRADE KILA SIKU (DAY TRADERS) WANAANGUKIA HAPO KWENYE SPECULATION (UTEGESHAJI AU BETTING). HIVYO KUJIHUSISHA NA SHUGHULI YEYOTE YA SPECULATION UNAHITAJI UWE NA UMAKINI MKUBWA SANA KWANI UNAWEZA KUPOTEZA MTAJI MUDA WOWOTE. PIA AINA HIYO YA WANAOTRADE FOREX WANAITWA 'SPECULATORS'
 
FOREX TRADING KWA KIWANGO KIKUBWA NI 'SPECULATION'. HII INATOKANA NA ASILI YA BIASHARA HIYO KWANI 'VOLATILITY' (MABADILIKO YA THAMANI YA FEDHA) NI MAKUBWA NDANI YA MUDA HUSIKA. HIVYO WAFANYABIASHARA WENGI WALIOPO KWENYE FOREX ESPECIALLY WANAOTRADE KILA SIKU (DAY TRADERS) WANAANGUKIA HAPO KWENYE SPECULATION (UTEGESHAJI AU BETTING). HIVYO KUJIHUSISHA NA SHUGHULI YEYOTE YA SPECULATION UNAHITAJI UWE NA UMAKINI MKUBWA SANA KWANI UNAWEZA KUPOTEZA MTAJI MUDA WOWOTE. PIA AINA HIYO YA WANAOTRADE FOREX WANAITWA 'SPECULATORS'
Nini kinakosekana kwa wawekezaji wa hapa Tanzania na kujikuta wakiangukia ndimi..??

Je, Tanzania imefanikiwa kiasi gani ktk sekta ya uwekezaji..??

Ni katika sekta ipi inafaa zaidi kuwekeza kwa Sasa hapa nchini..??
 
Back
Top Bottom