Uwekezaji Ikungi washika kasi, DC Muro atembelea uwekezaji wa alizeti

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Jerry C. Muro leo tarehe 21/10/2022 akiambatana na viongozi wa kamati ya usalama ya wilaya pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya wamefanya ziara ya kutembelea shamba la mwekezaji kampuni ya Alfadaws Investment Company kutoka Jordan ambao wamewekeza kwenye kilimo cha alizeti katika shamba la hekari 1,700 katika kata ya mkiwa kijiji cha Choda.

Katika ziara hiyo Dc Muro amepata nafasi ya kusikiliza kero na changamoto anazokabiliana nazo mwekezaji na kutembelea eneo ambalo limeshasafishwa tayari kuanza msimu mpya wa kilimo kwa mwaka 2023.

Akitoa taarifa kwa wajumbe, msimamizi wa mradi huo Ndugu Anas amesema, katika mradi huo wanatarajia kulima alizeti kwa mfumo wa umwagiliaji wa kisasa na wanatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha kukamulia alizeti kwa mtindo wa kisasa, pamoja na kuzalisha mbegu kwa ajili ya soko la ndani na nje ikiwemo kusaidia wazalishaji wa alizeti nchini na kusisitiza wamejipanga kuanza kulima katika msimu huu.

Dc Muro kwa upande wake amewahakikisha wawekezaji hao wanaendelea kutatua changamoto ikiwemo ukamilishaji wa mchakato wa kuwapatia hati, kukarabati barabara inayoelekea kwenye mradi.

IMG-20221022-WA0016.jpg
IMG-20221022-WA0013.jpg
IMG-20221022-WA0014.jpg
IMG-20221022-WA0012.jpg


Imetolewa na ofisi ya wilaya Ikungi,
21/10/2022.
 
UWEKEZAJI IKUNGI WASHIKA KASI, DC MURO ATEMBELEA UWEKEZAJI WA ALIZETI.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro leo tarehe 21/10/2022 akiambatana na viongozi wa kamati ya usalama ya wilaya pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya wamefanya ziara ya kutembelea shamba la mwekezaji kampuni ya Alfadaws investment company kutoka Jordan ambao wamewekeza kwenye kilimo cha alizeti katika shamba la hekari 1,700 katika kata ya mkiwa kijiji cha choda


Katika ziara hiyo Dc Muro amepata nafasi ya kusikiliza kero na changamoto anazokabiliana nazo mwekezaji na kutembelea eneo ambalo limeshasafishwa tayari kuanza msimu mpya wa kilimo kwa mwaka 2023

Akitoa taarifa kwa wajumbe, msimamizi wa mradi huo Ndugu Anas amesema katika mradi huo wanatarajia kulima alizeti kwa mfumo wa umwagiliaji wa kisasa na wanatarajia kujenga kiwanda kikubwa cha kukamulia alizeti kwa mtindo wa kisasa, pamoja na kuzalisha mbegu kwa ajili ya soko la ndani na nje ikiwemo kusaidia wazalishaji wa alizeti nchini na kusisitiza wamejipajga kuanza kulima katika msimu huu

Dc Muro kwa upande wake amewahakikisha wawekezaji hao wanaendelea kutatua changamoto ikiwemo ukamilishaji wa mchakato wa kuwapatia hati, kukarabati barabara inayoelekea kwenye mradi

Imetolewa na ofisi ya wilaya ikungi
2110/2022
Yaani wote wameamka na kuanza kujitangaza ili Mama aone wako busy, mkeka usiwasahau.
 
Back
Top Bottom