Kwa mipango inayoendelea pale, kiusalama hapafai kufanya uwekezaji wo wote na hata wale wanaoishi pale wako ktk hatari kubwa sana kiafya. Kuna gesi pale, kuna mitambo ya umeme mikubwa miwili yenye kuunguruma mchana kutwa. Kuna huo ujenzi wa flyover ya nguvu, kuna mwendo kasi, kuna matanki ya maji na mabomba yake. Upande wa Udsm kuna mto Ng`ombe unapanuka kila siku, upande wa Riverside kuna mto mwingine nao unapanuka kila kukicha. Kuna yale mawaya makubwa ya umeme, haaa.