SoC02 Uwekaji wa akiba ya pesa(money saving)

Stories of Change - 2022 Competition

InnoErie

Member
Dec 7, 2019
5
5
Hii ni moja ya tabia muhimu za pesa(financial behaviour) ya kuwa nayo.Hii ni tabia ambayo anaweza kuwa nayo mtu yeyote bila kujali jinsia yake na ukubwa/udogo wa kipato chake.Watu wengi tuna mitazamo tofauti na uwekaji wa akiba ya pesa.Unaweza sikia sentensi kama;

- Kipato changu ni kidogo
  • Tumia pesa ikuzoee(extravagance)
  • Furahi(enjoy) leo,kesho itajijua yenyewe.
  • Kesho nitapata tena.

Hii ni mojawapo ya visingizio vinavyosababishwa na utamaduni wetu na kutokuwa na elimu(financial literacy) na kupelekea kutokua na utamaduni wa kuweka AKIBA.Lakini ni muhimu kutambua kuwa haijalishi ni kiasi cha pesa unachotengeneza bali unachotunza na matumizi ya pesa(hata yasiyo ya lazima) huongezeka sambamba na kuongezeka kwa kipato. Kesho ywtu ni matokeo ya maamuzi ya leo.Katika uzi huu tutagusa maeneo matatu ambayo ni sababu zinazopelekea watu wasiweke akiba,njia na mbinu za kuweka akiba na faida za kuweka akiba.

Katika utamaduni wa hiari wa kuweka akiba,watu wengi wanashindwa lakini wanaweza kuweka akiba kwa kutumia mifumo lazimishi pengine bila kutambua mfano mifumo ya kibenki na pensheni.

Kwanini utamaduni wa kutunza akiba haupo kwa watu wengi? Kuna sababu mbalimbali kama vile;
i.Mtazamo binafsi wa pesa
ii.Matumizi horera ya pesa
iii.Kiasi cha kipato
iv.Aina ya chanzo cha kipato

I. MTAZAMO BINAFSI WA PESA
Mtazamo binafsi wa mtu juu ya pesa ni nyenzo muhimu na kichocheo kikubwa cha kuweka akiba.Mtu akiwa na mtazamo hasi juu ya uwekaji wa akiba hawezi kamwe kuweka akiba.Mtazamo hutokana na malezi aliyopitia pindi anakua na elimu ya pesa(Financial literacy).Elimu ya pesa na malezi ya familia ni muhimu katika kumjengea mtoto mtazamo mzuri wa pesa haswa katika suala la kuweka akiba.

II. MATUMIZI HORERA YA PESA
"Mali bila daftari hupotea bila habari".Katika jamii yetu kukutana na mtu hana bajeti ya pesa ni jambo la kawaida.Kukosa bajeti hupelekea kukosa vipaumbele katika matumizi na kutumia pesa horera kwa kufanya manunuzi yasiyo ya lazima.
Bajeti husaidia kujua unatumia kiasi ganj cha pesa na katika eneo lipi na huepusha kutumia pesa kwa vitu ambavyo sivyo vipaumbele.

III. KIASI CHA KIPATO
Kipato kinawezakuwa kikwazo cha kuweka akiba? Kimahesabu kipato siyo kikwazo.Unaweza weka akiba bila kujali ukubwa/udogo wa kipato.Tuna mtazamo kwamba watu wasiokuwa na kipato kikubwa hawawezi weka akiba lakini unaweza weka akiba hata ya Tsh.1,000/= kwa kila unachoingiza.

IV. AINA YA CHANZO CHA KIPATO
Kuna aina za vyanzo vya vipato vikuu ambavyo ni Mshahara na Faida itokanayo na biashara.Tuna kasumba kwamba huwezi akiba kutoka kipato kitokanacho na Mshahara lakini bila kujali aina ya chanzo cha kipato mtu anaweza weza akiba.

Mtu anaweza kuwa na malengo ya kuweka akiba lakini akashindwa namna na mbinu za kuweka akiba.

NJIA NA MBINU ZA KUWEKA AKIBA
a.kuweka Lengo/Malengo ya akiba.
b.Kurahisisha mtindo wa maisha(Lifestyle simplifications)
c.Kuweka akiba.

A. KUWEKA LENGO/MALENGO YA AKIBA
Ni vyema kuwa na sababu ya kuweka akiba.Naweka akiba kwaajili ya nini?.Pesa haikosi matumizi.Unaweka akiba kwaajili ya matumizi ya baadae.Kila mtu ana malengo yake pengine lengo la kujenga, mahali, kununua gari, Ada ya watoto, Mtaji kwaajili ya kuwekeza au nauli.Kwahiyo lengo ni chachu ya kuweka akiba. Ili mtu awe wazi katika hili ni vizuri awe na vitu kuu vitatu ambavyo hurasisha kutimiza malengo;

  • Sabubu ya akiba(lengo lenyewe)
  • Kiasi cha akiba
  • Muda wa kuweka akiba.

B. KURAHISISHA MTINDO WA MAISHA(LIFESTYLE SIMPLICATIONS)
Kurahisisha mtindo wa maisha kwa kutumia chini ya kipato tunachoingiza(Living below our means).Matumizi yasizidi kipato,yawe chini ya kipato.Hii ni moja ya njia muhimu ili kuweka akiba na inahitaji nidhamu ya hali ya juu(Financial discipline).

Tunaweza kufanya hivyo kwa kuzingatia kwanza mahitaji maalumu(basic needs) ambayo ni chakula,mavazi na malazi na hii husaidiwa na kuwa na bajeti ili kuepuka matumizi horera.

C. KUWEKA AKIBA
NB;Kabla ya matumizi.
Mazoea ya waliowengi huweka akiba baada ya matumizi yaani hutunza kile kilichobaki baada ya matumizi.Kwa nidhamu ya pesa, njia nzuri na sahihi,akiba hutunzwa kabla ya matumizi.Hivyo,kabla ya matumizi inabidi kuweka % ya sehemu ya kipato kwaajili ya akiba.

FAIDA YA KUWEKA AKIBA YA PESA
i.Akiba husaidia kutimiza lengo ulilojiwekea.

Kabla tumeangalia njia na mbinu za kuweka akiba.Kuwa na lengo ni njia mojawapo.Hivyo,akiba huja kutimiza lengo ambalo mtu kajiwekea.

Ii.Akiba husaidia katika dharura.
Akiba husaidia kujiokoa na tukio la dharula ambalo linahitaji msaada wa haraka wa Fedha pengine inaweza kuwa dharula ya kiafya au mahitaji binafsi.

iii.Husaidia katika uwekezaji
Mojawapo wa vyanzo vya mtaji ni akiba(personal savings).Pesa iliyotunzwa hutumika kuzalisha pesa nyingine zaidi(financial multiplication).

Hitimisho,Ukija katika suala pesa wengi hufikiri pesa hutafutwa ili zitumike hapohapo tu(spending) lakini pesa ina kazi zaidi ya tatu ambazo ni;
  • Matumizi (spending)
  • Akiba (saving)
  • Kuwekeza (investing)
  • Kutoa msaada (Donationa)

FB_IMG_16209933341514342.jpg
 
Sie wengine wenye madeni ambao tukipata mshahara tunalipa halafu tunakopa tena siku hiyo hiyo tunaruhusiwa kuchangia....?
 
View attachment 2329322
Asante Mkuu kwa Darasa Murua
 
Hizi story za akiba ni kwa watu wenye vipato vizuri. Sasa hela yenyewe ugali maharage mpaka pumbuz zitoke jasho kweli uta save nini.
Leo una kibarua kesho hakipo wapi na wapi. Mambo mengine tusiongelee tuu content tuagalie na context
 
Kama ukiwa unafanya biashara akiba utawekaje, wakati biashara inakutaka kila shilingi iingie katika mzunguko?
 
Back
Top Bottom