Uwekaji maji kwenye rejeta ya gari

Uwekaji maji kwenye rejeta ya gari

Zogoo da khama

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2013
Posts
639
Reaction score
611
Wanabodi mliowazoefu wa magari hasa gari ndogo za binafsi naomba mnijulishe
A) Gari ndogo inapaswa kuwekwa maji baada ya muda/siku ngapi?
B) Coolant zipo ndogo na kubwa za ltr 1 kila baada ya siku ngapi unaweka na unaweza kuchanganya vyote kwa wakati mmoja yaani coolant imeisha na ujazie maji.
Na kwa safari ndefu za mikoani Arusha nashaurije kuhusu swala la maji/coolant niweke baada ya km ngapi. Naomba msaada wenu ule msimu wetu wa hija za kwetu hauko mbali.
 
Kama gari sio mbovu na hakuna leak kwenye cooling system utakuwa hauna haja ya kuongeza maji/coolant maana ile ni closed system maji yanapata joto kupooza engine then yanakuja kwenye radiator yanapozwa then yanaenda kupooza engine hayaendi kokote. Now kunaweza kukawa na leak ndogo ya mvuke au maji ambayo itakulazimu kuongeza coolant kila baada ya miezi kadhaa au hata mwaka, hapo utaamua mwenyewe kama ni bora kuongeza collant au kujaribu kutafuta na kuziba hiyo leak ambayo inaweza kuwa gharama kubwa na kuleta matatizo mengine.
 
Wanabodi mliowazoefu wa magari hasa gari ndogo za binafsi naomba mnijulishe
A) Gari ndogo inapaswa kuwekwa maji baada ya muda/siku ngapi?
B) Coolant zipo ndogo na kubwa za ltr 1 kila baada ya siku ngapi unaweka na unaweza kuchanganya vyote kwa wakati mmoja yaani coolant imeisha na ujazie maji.
Na kwa safari ndefu za mikoani Arusha nashaurije kuhusu swala la maji/coolant niweke baada ya km ngapi. Naomba msaada wenu ule msimu wetu wa hija za kwetu hauko mbali.

Kinachonishangaza mimi ni wapi mnapotokea madereva nyie msiojua hata vitu vidogo vya msingi kabisa kwenye gari? We ndugu umejifunza kuendesha gari kweli? Au unajua kushika usukani tu.......na hapo unataka uingoe barabara ya mkoani Dar- Arusha. Halaf tunasikitika ajali zikitokea.
 
mkuu hebu tusaidie wewe maana mi mwenyewe hahitaji kujua alilouliza mkuu hapo juu... coolant inawekwa kila baada ya mda gani?
 
Mkuu Kang asante kwa ufafanuzi Wako, sasa kama gari unaweka maji/coolant kila baada ya siku 4 hapo ni tatizo, waswahili wanasema mtu kidole kwa hapa Dar mafundi wazuri wa cooling system wanapatikana wapi kwani mi ni mhanga wa tatizo hilo.
Ndugu yangu GeoMex hili ni jukwaa la kuelimishana sio la mipasho ukiona swali linaukakasi kwa upande wako lipotezee.
 
Wanabodi mliowazoefu wa magari hasa gari ndogo za binafsi naomba mnijulishe
A) Gari ndogo inapaswa kuwekwa maji baada ya muda/siku ngapi?
B) Coolant zipo ndogo na kubwa za ltr 1 kila baada ya siku ngapi unaweka na unaweza kuchanganya vyote kwa wakati mmoja yaani coolant imeisha na ujazie maji.
Na kwa safari ndefu za mikoani Arusha nashaurije kuhusu swala la maji/coolant niweke baada ya km ngapi. Naomba msaada wenu ule msimu wetu wa hija za kwetu hauko mbali.
Kama ni coolant pale kwenye container kwenye gari si imeonyeshwa level yake?? kuna max level na unatakiwa uobserve isipungue.mi nna gari ya cc 2000 nimeweka collant ikakaa miezi 9 ndio imepungua so suala la kuongeza baada ya masaa hapo kuna leakage na pia gari hilo sio Zima.
 
Mkuu Kang asante kwa ufafanuzi Wako, sasa kama gari unaweka maji/coolant kila baada ya siku 4 hapo ni tatizo, waswahili wanasema mtu kidole kwa hapa Dar mafundi wazuri wa cooling system wanapatikana wapi kwani mi ni mhanga wa tatizo hilo.
Ndugu yangu GeoMex hili ni jukwaa la kuelimishana sio la mipasho ukiona swali linaukakasi kwa upande wako lipotezee.

Chunguza kama kuna leak yoyote unapopaki gari sehemu moja na kurun engine pia angalia kizibo cha radiator hiki ni muhimu sana na kinatakiwa kuwa kimefungwa sawa, kinafit na kipo kwenye hali nzuri kuzuia maji kutoroka kwa mvuke.
 
mimi kwa uelewa wangu coolant haipungui labda kama kuna leak halafu wabongo tunakosea radiator haiwekwi maji. Watu huweka maji kwa ajili ya ubahili tu hasa wa malori ila gari ndogo usiweke maji, kwanza epuka coolant za kibongo wanajaza maji na rangi nunua za nje. Halafu coolant org haipati joto ata ukiweka kwenye jua.
 
kama gari haivuji maji na haina tatizo kwenye mfumo wa ingine huwa haipungui maji
 
Haina haja ya kuweka maji ndugu labda yawe yanavuja kama gari mpya nakushauri toa thermostat mi ninayo Toyota passo cjawahi weka maji toka japan mwambie fundi nahitaj toa thermostat.

Usitoe thermostat mkuu kwa namna yoyote. Chunguza maji yatakuwa nanavuja sehemu then pazibwe. Kama ni radiator au hose pipes au kifuniko cha radiator vinaweza kuwa sababu. Ukitoa thermostat engine halitakuwa linapata joto lake stahiki na hivyo haitadumu. Thermostat kazi yake ni ku regulate joto la engine lisipungue wala kuzidi. Wametengeneza kwa hesabu mkuu usifanye hilo kosa.
 
Kwa uelewa wangu aliyeshauri kutoa thermostart yuko sahihi. Ni kweli pia thermostart inawekwa kwa madhumuni hayo ya kumaintain proper engine working temperture ila hilo linazihusu nchi zenye baridi kali. Kinachofanyika kwenye nchi za baridi ni kuzuwia mzunguko wa maji kwenye engine mpaka pale joto la engine linapopanda kufikia kiwango fulani ndipo thermostart inafungua na kuruhusu maji kuzunguka na kupoza engine. Kwa nchi za joto kama hapa kwetu thermostart inasababisha engine kuchemka na mwishowe coolant/ maji kupungua na ni hatari kwa usalama wa engine. Coolant ikipata exessive tempersture, pressure kwenye radiator nayo inapanda hivyo usishangae leakages za kulazimishwa
 
Wanabodi nawashukuru wote kwa michango yenu tumeelimishana bila kukizana. Bigup Sana nitayafanyia kazi hasa katika kununua coolant iliyo bora awali nilikua nanunua ya 1ltr kwa Tsh 5,000 nikijua zote ni sasa nikaacha ya Tsh. 10,000 mbayo kwa ujazo ni ndogo. Nahukuru sana
 
Asante, kweli tumeelimika wengi, shukrani za pekee kwa mleta uzi na pia kwa wachangiaji wote.
 
Wanabodi mliowazoefu wa magari hasa gari ndogo za binafsi naomba mnijulishe
A) Gari ndogo inapaswa kuwekwa maji baada ya muda/siku ngapi?
B) Coolant zipo ndogo na kubwa za ltr 1 kila baada ya siku ngapi unaweka na unaweza kuchanganya vyote kwa wakati mmoja yaani coolant imeisha na ujazie maji.
Na kwa safari ndefu za mikoani Arusha nashaurije kuhusu swala la maji/coolant niweke baada ya km ngapi. Naomba msaada wenu ule msimu wetu wa hija za kwetu hauko mbali.

Hutakiwi kuongeza.maji wala coolant kwenye rejeta...kwani ni mzunguko tuu wa maji ...ukiona rejeta yako haikai na maji basi kuna tatizo...nina mwaka sijaongeza maji kwenye gari yangu...na kila napocheki hali ni shwari same water level...
 
1. Hauhitaji kuongeza coolant Mara kwa mara kwenye Gari, kama inapungua basi kuna leak. Peleka gerage ikatengenezwe.

2. Msiweke maji kwenye radiator (maarufu kama rejeta), wekeni coolant tu. Maji yana tabia ya kutengeneza kutu. Kutu hula vyuma na kuvitoboa. Pengine kuisha kwa hayo maji unayoweka badala ya coolant kumesababishwa na kutu Katika mfumo wa upozaji (cooling system.)
 
Kinachonishangaza mimi ni wapi mnapotokea madereva nyie msiojua hata vitu vidogo vya msingi kabisa kwenye gari? We ndugu umejifunza kuendesha gari kweli? Au unajua kushika usukani tu.......na hapo unataka uingoe barabara ya mkoani Dar- Arusha. Halaf tunasikitika ajali zikitokea.
Acha mipasho, haukulazimishwa kujibu
 
Back
Top Bottom