Uwe makini na tovuti bandia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwe makini na tovuti bandia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Nov 22, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Uwe Makini na Tovuti Bandia

  Kumekuwa na tatizo la wanunuzi wa vitu kwa njia ya mtandao kupelekwa Kwenye tovuti bandia kwa ajili ya kununua bidhaa Fulani Kwenye tovuti hiyo wakati mwingine bila ya wao kujua yaani anapotafuta kitu kutumia search anapata kiunganishi cha tovuti hiyo na kufuata tovuti hiyo kwa ajili ya manunuzi lakini mwisho wa siku ndio atakuwa ameweka taarifa zake Kwenye tovuti hiyo na kuibibwa kwa ajili ya kufanya uhalifu sehemu nyingine pamoja na kutumia kwa ajili ya kununua vitu na mhalifu huyo au kuchukuwa pesa .

  Ingawa kuna baadhi ya antivirus pamoja na internet security zinazoweza kutambua tovuti za aina hiyo sio watu wote walioweka bidhaa hizo Kwenye computer zao na hata kama wameweka sio wote ambao wana antivirus zenye uwezo wa kutambua tovuti za aina hiyo au kama zinazo kuna wengine wanapuuza kufanya updates Kwenye programu zao hizo kwahiyo kila mtu unakuta anashida yake hapo .

  Kuna baadhi yao wanadanyanyika kwa majina tu akiona kwa mfano tovuti inaitwa www.mipasho.co.in anapoangalia co.in anafikiri tovuti hiyo lazima iwe India au www.mipasho.co.uk Kwamba tovuti hiyo lazima uwe UK kwa ufupi tovuti inaweze kuendeshwa kutokea sehemu yoyote duniani , kujua jina la tovuti haiwezi kusaidia wewe kupata usalama zaidi unapofanya mambo yako Kwenye mtandao na haimaanishi kwamba tovuti hiyo inalindwa au kuendeshwa na tovuti ambayo iko Kwenye nchi hiyo .

  Pamoja na hayo yote kuna vitu vya msingi wewe kama mtembeleaji wa tovuti na wenzako ambao wanatembelea tovuti Fulani kwa ajili ya manunuzi na aina nyingine za biashara kwa njia ya mtandao inabidi uvijue ili huko mbeleni viweze kukusaidia zaidi .

  Unaweza kupunguza uwezekano wa kuingia kwenye tovuti bandia kwa ajili ya manunuzi au vitu vingine vinavyohusu biashara na mawasiliano kwa kufanya yafuatayo .

  1 – Angalia kama kuna hakiki yoyote ya tovuti hiyo ( Review ) ingawa ni tovuti chache zenye review kama ni ya biashara lazima itakuwa imeandikwa sehemu kwa asilimia ndogo , huko ilipoandikwa ndio unaweza kuchagua

  2 – Unaweza kutumia programu au kutembelea www.whois.ws kwa ajili ya kuangalia kampuni iliyosajili tovuti hiyo na inayoiendesha ili ujiridhishe , kuna tovuti na programu zinazoweza kutoa taarifa za kina zaidi .

  3 – Tafuta namba za mawasiliano ya kampuni hiyo na anuani zingine za sehemu ambapo kampuni husika ipo na kuwasiliana nao kama unaweza , ukitumia google maps yote hii inaweza kufanya kwa sekunde tu .

  Kwahiyo kama unafanya manunuzi au biashara yoyote kwa njia ya mtandao hiyo ni mambo machache tu ya kuangalia kuna mengi zaidi ya kuangalia na kujifunza unaweza kujua hayo kwa kuuliza na kutembelea tovuti zingine kwa ajili ya mijadala inayohusiana na vitu hivi

  Usiku Mwema

  www.wanabidii.net www.naombakazi.com www.askmaro.blogspot.com
   
Loading...