Uwaziri kwa CCM ni ULAJI

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,131
0
Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, alipoulizwa CCM imepokeaje uamuzi wa Bw. Chenge alionekana kutokuwa tayari kuzungumzia suala hilo. "Uwaziri wa Bw. Chenge mimi unanihusu nini, Uwaziri kilikuwa ni kibarua chake kilikuwa kikimsaidia yeye na watoto wake, sasa CCM iseme nini? Alihoji Bw. Makamba na kuongeza: "Wewe kama unataka niulize mambo yanayohusu muafaka, kuna mambo mengi yanayohusu CCM," alisisitiza Bw. Makamba.

Chanzo:http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6415
 
FDR Jr

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
249
0
Huyu mzee ametoa majibu haya kweli au? Januari anaona babake anavyokipalia makaa chama chetu yeye anakula juice Ikulu!!!
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,190
0
Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, alipoulizwa CCM imepokeaje uamuzi wa Bw. Chenge alionekana kutokuwa tayari kuzungumzia suala hilo. "Uwaziri wa Bw. Chenge mimi unanihusu nini, Uwaziri kilikuwa ni kibarua chake kilikuwa kikimsaidia yeye na watoto wake, sasa CCM iseme nini? Alihoji Bw. Makamba na kuongeza: "Wewe kama unataka niulize mambo yanayohusu muafaka, kuna mambo mengi yanayohusu CCM," alisisitiza Bw. Makamba.

Chanzo:http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6415

Poor Makamba,

Zile cheche zote alizokuwa nazo pale Dar na kumwaga mabusu motomoto kwa Manji sijui zimeishia wapi!?
 
Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
19,480
2,000
ndo vibaraka wenyewe hao, sasa yeye hataki kuzungumzia kibarua cha chenge kwa kudai ile ni kazi inayomsaidia yeye na watoto wake, na amesahau kuwa huyo chenge alikuwa anawatumikia watanzania, na kasahau chenge ni mwanachama wa CCM na yeye makamba ndie katibu wa chama hicho, sasa sijui alitaka tukamuulize dr slaa au?
 
WembeMkali

JF-Expert Member
Jun 16, 2007
282
0
Asha,

Kumbe uwaziri ni wakumsaidia mtu na watoto wake! mimi nilifikiri uwaziri ni utumishi kwa taifa na wananchi wake kumbe ...
 
Kiungani

JF-Expert Member
Feb 2, 2007
274
195
Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, alipoulizwa CCM imepokeaje uamuzi wa Bw. Chenge alionekana kutokuwa tayari kuzungumzia suala hilo. "Uwaziri wa Bw. Chenge mimi unanihusu nini, Uwaziri kilikuwa ni kibarua chake kilikuwa kikimsaidia yeye na watoto wake, sasa CCM iseme nini? Alihoji Bw. Makamba na kuongeza: "Wewe kama unataka niulize mambo yanayohusu muafaka, kuna mambo mengi yanayohusu CCM," alisisitiza Bw. Makamba.

Chanzo:http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6415

Mmmh, ukiangalia Makamba hapo kajibu hovyo ila kasema ukweli pengine bila kujijua.

Ni ukweli kuwa u-Waziri wa Tz ni kwa faida ya huyo mtu binafsi na watoto wake. Hili Makamba na CCM wanalijua na ndiyo maana hawalivalii njuga kunapokuwepo na masuala ya wizi, ufisadi, uzembe kazini, rushwa, ku-forge degrees, n.k.

Jiulize watu kama akina Ngasongwa, Kingunge, Mungai, Nchimbi, Karamagi, Chenge, Lowassa, Kikwete, Msabaha, Mathayo, Mramba, Kahama, Keenja, n.k. wamesaidia nini na u-Waziri wao zaidi ya kujineemesha wao na watoto wao?

Kama u-Waziri ungekuwa ni kwa faida ya Taifa na/au chama, basi wote waliopo madarakani sasa hivi wangekuwa jela, na chama t(w)awala kingekuwa kinara wa kulaani maovu yanayofanywa na 'viongozi ma-waziri' hao.

Tumlaani Makamba kwa kusema ovyo ila tukubali kuwa kafunua kikombe kabla mwanaharamu hajapita.
 
KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
1,225
Hii kali sikutegemea katibu wa chama kuanika hili. Hapa tunazidi kupata majibu kwa nini watanzania ni masikini haswa kumbe hawa jamaa wao madaraka ni ya familia zao?

Asante makamba
 
Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,330
1,250
Jamani mambo magumu kiasi kuwa sasa kila mtu na chake mambo ya kuinganisha CCM na watu wake hawataki, Chenge ni kiongozi wa juu wa CCM hakuna jinsi ambavyo CCM wanaweza kumkana maana ni kiongozi wao na yuko kwenye kamati ya maadili maadili gani anasimamia fisadi kama yeye, atweza kumwambia fisadi mwenzio ahache ufisadi wakati yeye ndo anaongoza?
Wanajaribu kuitenganisha CCM na mafisadi lakini hilo halitafanikiwa kwa kuwa mafisadi wengine bado wamo CCM na wataendelea kuumbuliwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom