Uwanja wa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwanja wa Taifa

Discussion in 'Jamii Photos' started by Makoye Matale, Jun 22, 2011.

 1. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Soccer City.jpg Soccer City.jpg

  Tangu mwaka 2006 Watanzania na viongozi wetu tumekuwa tunajidai kuwa tunao uwanja wa michezo wa kisasa kabisa huku tukisahau kuwa tunahitajika kujenga viwanja vingine zaidi katika miji kama Arusha, Tanga, Mbeya, Mwanza na Dodoma angalau tupate sifa ya kuandaa mashindano ya Cup of African Nations (CAN) au hata hiyo CHAN.

  Hapo juu ni uwanja wa Soccer City katika Jiji la Johannesburg huko Afrika ya Kusini. Kwa kulinganisha uwanja wetu na uwanja huu wa wenzetu haitufundishi kwamba safari yetu ni ndefu katika ujenzi wa viwanja vya Michezo?

  Tubadilike badala ya kujisifu kila kukicha huku tumelala usingizi mnono!
   
 2. S

  Stanley Ngugi New Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ni uwanja mzuri sana, mimi sio kwa kuona kwa picha tu bali nimefika katika uwanja huu. Lakini, tusijidharau sana kuwa Tanzania hatuna uwanja mzuri kwa kujilinganisha na wenzetu, lugha nzuri iwe 'ni mwanzo mzuri ila tunahitaji kusonga mbele.' Ukiangalia katika Afrika mashariki na kati, uwanja wetu Tanzania bado ni changamoto kwa wengi. Tunawasikia wengi wakisema, 'well done Tanzania, keep up the good work.' Cha muhimu tusijisahau tukafikiri ndo tumefika, tunahitaji kupiga hatua mbele ili tusiachwe na wakati.
   
 3. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu umesukumwa na nini kusema hivyo.Je soka letu lipo chini sababu ya kiwanja,Hivi Ivory cost wanaviwanja vingapi vya kisasa,Zaire wanaviwanja vingapi.Je mkuu ndo suruhisho la soka letu butu?
   
 4. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Nimeleta hoja hii baada ya kuona hakuna juhudi zozote za kujenga viwanja vingine ambavyo vitatoa nafasi kwa vijana wetu kujiendeleza kimichezo badala ya kuwa na viwanja vya ajabu ajabu kama Ali Hassan Mwinyi pale Tabora, Jamhuri pale Dodoma na Morogoro, Kambarage pale Shinyanga, Kaitaba pale Bukoba, Mkwakwani pale Tanga n.k. Viongozi wameendelea kujisifu tu kwa uanja ule wa Taifa badala ya kujenga viwanja vingine. Hata hii bajeti iliyopitishwa jana bila shaka hakuna fungu la kujenga kiwanja angalau kimoja.

  Kwa kuangalia viwanja vya wenzetu, tujifunze kuwa safari yetu haijafika mwisho, tujenge angalau kiwanja kimoja cha kisasa katika kila mwaka wa fedha na huo uwezo tunao.
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Wewe mwenzetu umehama mada,mwenyeji kaleta mada ya tathimini ya viwanja kwa kuongelea hadhi ya kiwanja chetu

  kimsingi uwanja wetu ni wa kati make viwanja vipo vilivyo bora sana na vinajulikana na kweli tusiangalie tuna vingapi tukaridhika,la muhimu ni kulenga mbali zaidi hata tufikishe kumi,is okay,umuhimu wake unaeleweka..mfano ni kiwanja cha Uhuru-Morogoro unaona kinastahili kuhost CECAFA ama basi tu

  kwani kama JK anahaidi kingine kama hiki kabla ya 2015 kuna ubaya gani? let us be ambitious.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  kwenye picha juu mbona naona viwanja vyote viwili ni soccercity?
  Maximo stadium sijauona, au umeme umekatika ndio maana hauonekani sababu ya giza?
   
Loading...