Uwanja wa Azam ni mzuri sana

maiyanga1

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
1,317
1,790
Naangalia mchezo wa kirafiki Azam na Coast Union.

Pamoja na burudani hiyo ninashangazwa na ubora wa uwanja, hasa eneo la kuchezea.
Nalinganisha ninachokiona na hali za viwanja kama Mkwakwani Tanga, Sokoine Mbeya, Jamhuri Morogoro/Dodoma, Sheikh Amri Abeid Arusha na vinginevyo ambavyo ni vya serikali ya CCM.

Najiuliza inawezekanaje S.Bakheresa aweze kujenga uwanja mzuri kama huu serikali ishindwe?
 
Huo mchezo wa kirafiki niliutizama itoshe kusema laiti kama klabu zote zingekuwa na viwanja angalau vya namna hiyo aisee ligi kuu ingekuwa ya moto sana. Union wemecheza vizuri sana.
 
Naangalia mchezo wa kirafiki Azam na Coast Union.

Pamoja na burudani hiyo ninashangazwa na ubora wa uwanja, hasa eneo la kuchezea.
Nalinganisha ninachokiona na hali za viwanja kama Mkwakwani Tanga, Sokoine Mbeya, Jamhuri Morogoro/Dodoma, Sheikh Amri Abeid Arusha na vinginevyo ambavyo ni vya serikali ya CCM.

Najiuliza inawezekanaje S.Bakheresa aweze kujenga uwanja mzuri kama huu serikali ishindwe?

Miradi ya serikali huwa haiendelei, management mbovu, walaji ni wengi. refer Shule za kata, viwanda, nyumba za msajili, migodi inawashinda kuiendesha mpaka wanarudisha kwa wawekezaji n.k.

Inasemekana nyumba za msajili walijenga wahindi kwa pesa zao, serikali ya nyerere ikawapokonya/taifisha.
 
Sidhani kama serikali inatambua umuhimu wa michezo katika kutengeneza ajira na muendelezo wa soka kwa kuwa na viwanja bora. Kwa mfano mpira sasa hivi umeajiri vijana wengi achilia zile ajira ambazo si za moja kwa moja.
Fikiria kwa mfano Simba wametia nanga jijini Mwanza kucheza mechi yao hapo. Biashara nyingi za mahoteli, migahawa, mama ntilie, mabasi, boda boda, bajaji, wauza jezi n.k. wote hawa hufaidika na ujio wa timu kama Simba. Mzunguuko wa pesa unakuwa mkubwa ghafla achilia mbali ukweli kwamba hii ndio ligi pendwa katika ukanda huu. Sasa kama Zambia, Kenya, Uganda, Burundi, mitandaoni n.k. wanafuatilia ligi hii kwa ukaribu, iweje tuwe na viwanja vibovu? Sababu mojawapo iliyomkimbiza Calinho ni hivi viwanja vibovu na inasemekana alikuwa anapata shida sana kucheza katika viwanja hivyo.
Kama tunataka soka letu liendelee ni lazima turekebishe viwanja hivi.
Hongera Azam kwa kututoa kimaso maso katika suala la kurusha matangazo mubashara lakini viwanja ndio bado changamoto.
 
Back
Top Bottom