Uwanja mpya wa Taifa aibu tupu!

Uwanja mpya wa Taifa aibu tupu!

yahoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
3,526
Reaction score
1,410
Kwa wale walibaatika kuingia uwanja wa taifa na kukaa sehenu tofauti tofauti watakubaliana na mimi kwamba uwanja unaonekana mzuri lakini upo chini ya viwango kwa kiwango cha kutisha na kwamba miaka hamsini ijayo utakuwa hoi kama sio kuanguka.Ukichunguza vizuri utakutana na nyufa sehemu nyingi za uwanja.Viti vyenyewe lawama sio kama vya uwanja wa zamani ambapo hata ucheze kiduku juu ya kiti hakingoki.Kofia haijafunika vizuri uwanja (vip wanaloa mvua).Nashangaa kwanini hatuwahoji wachina badala yake tunazidi kuwapa tenda nyingine.
 
.......safi sana kwa kuliona hilo na kuliongelea; kwa vile bado Wachina wanaendelea kuusimamia bado tuna nafasi ya kuhoji. I support you Man.
 
Kwa wale walibaatika kuingia uwanja wa taifa na kukaa sehenu tofauti tofauti watakubaliana na mimi kwamba uwanja unaonekana mzuri lakini upo chini ya viwango kwa kiwango cha kutisha na kwamba miaka hamsini ijayo utakuwa hoi kama sio kuanguka.Ukichunguza vizuri utakutana na nyufa sehemu nyingi za uwanja.Viti vyenyewe lawama sio kama vya uwanja wa zamani ambapo hata ucheze kiduku juu ya kiti hakingoki.Kofia haijafunika vizuri uwanja (vip wanaloa mvua).Nashangaa kwanini hatuwahoji wachina badala yake tunazidi kuwapa tenda nyingine.

Binafsi wazo la kuwa na liuwanja likuubwa, halafu kimpira hamna kitu sikulipenda tangu awali.
Bora tungetumia pesa kidogo kuurekebisha ule wa Taifa Original kuuleta kwenye capacity ya 40,000 hivi.
Mradi mpya matatizo chungu nzima...
 
Kosa si la wachina ni letu sisi, si tulimpa u consultant architecture Mushi? sasa yeye na kamati yake walikuwa hawkuipitia michoro?
Kama kuna kasoro zozote nyufa na n.k anatakiwa aitwe ajibu maswali
 
Ule upande wa yanga ndo uko taabani zaidi. Nashkuru wachina walijua pa kuweka ile screen otherwise!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
uwanja umejengwa yatupa kuutunza. kwanini uende kucheza kiduku kwenye kiti?. Ile ndo ramani ya uwanja so vip kuriwa ni lazima. but kwenye nyufa naomba unielekeze ni wapi umeona nyufa au utuwekee picha hapa tuone. Sema ule uwanja unaweza shika namba moja katika viwanja vya africa kwa uchafu. pale chini ya sehemu wanapo kaa wachezaji wa akiba kuna matank matatu ya kuhifadhi maji ya mvua ambayo yanatumika msimu mzima kumwagilia nyasi. kwanini wastumie maji yale kusaficha vyoo na viti?. mia
 
Back
Top Bottom