ligendayika
JF-Expert Member
- Aug 31, 2012
- 1,183
- 199
Jana nilikua katika mjia mafinga naangalia mechi kati ya Majimaji ya songea wana lizombi na timu ya kurugenzi mafinga. Kilichonsikitisha sana kama mdau nuliesafiri toka songea ni uwanja huo kutokua na sifa za kuchezewa mashindano kama haya ya ligi daraja la kwanza. Washabiki walikua wakileta fujo kiasi cha kutupa mawe na wengine kuwachapa viboko wahezaji mfano mchezaji mmoja wa majimaji akijiandaa kupiga mpira wa goal kick alipigwa na mshabiki wa mafinga na kipande cha mti. Pamoja na askari kupiga mabom ya moshi washabiki hao waliendelea kufanya fujo. Kwa mtazamo wangu uwanja huu hauna usalama wa kutosha tff mian h alia nini kuuacha uwanja huu uchezewe ni vyema mkaliangalia hili