Uvutaji sigara ndani ya Tahfif

Uvutaji sigara ndani ya Tahfif

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,465
Wana JF, kwa siku kadhaa nimekuwa nikiingia katika duka linalouza vifaa vya elimu la Tahfif, Mtaa wa Mansfield -jirani kabisa na Benki ya Mkombozi. Huyu jamaa (Mhindi) anayeonekana kuwa mmiliki wa duka hili anavuta sigara kwa fujo sana. Anavuta bila kujali idadi kubwa ya watu waliojazana kununua vifaa hasa wakati huu wa shule kufunguliwa. Anajua kabisa sheria za nchi zinazuia, lakini haonekani kuogopa wala kuheshimu. Wateja nao wamekuwa wakiumia kwa moshi pengine kwa sababu wana shida ya vifaa vya elimu au kwa sababu ya woga wa Kitanzania.
Nashauri ikiwezekana tususe kununua vifaa ndani ya duka hili hadi atakapoacha kuvuta sigara kwa dharau bila kujali afya za wateja na wafanyakazi katika duka hilo.

Nawasilisha
 
Mmewahi kumwambia mkuu? Hebu mfikishieni ujumbe kwanza alafu akikataa uje tujadili hatua za kuchukua
 
Mmewahi kumwambia mkuu? Hebu mfikishieni ujumbe kwanza alafu akikataa uje tujadili hatua za kuchukua


Mara kadhaa Watanzania ni wa ajabu kabisa. Nimejaribu mara kadhaa kukemea uhuni wa aina hii kwenye mabasi, nimegeuziwa kibao na wenzangu. Mfano mzuri ni kwenye mabasi. Lakini nadhani kwa ushauri wako kuanzia kesho, moja ya kazi zangu ni kumtazama uso mwangavu kabisa na kumweleza adha anazowasababishia wateja pamoja na wafanyakazi wake.
 
ulijaribu kumwambia.....? au na wewe uliogopa kama wengine....?
 
Mara kadhaa Watanzania ni wa ajabu kabisa. Nimejaribu mara kadhaa kukemea uhuni wa aina hii kwenye mabasi, nimegeuziwa kibao na wenzangu. Mfano mzuri ni kwenye mabasi. Lakini nadhani kwa ushauri wako kuanzia kesho, moja ya kazi zangu ni kumtazama uso mwangavu kabisa na kumweleza adha anazowasababishia wateja pamoja na wafanyakazi wake.

Itakuwa sawa kabisa mkuu, mweleze wazi wazi ubaya wa hicho kitendo na makosa ayafanyayo, anaweza kukuelewa inshaalah
 
ungemwambia kwanza kabla ya kuja apa,angekataa ndio ungekuja apa
 
Back
Top Bottom