Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,628
- 46,273
Mkaa unauzwa bei rahisi sana nchi hii, huwa nashangaa kama kweli tunayo miti mingi ya kuiteketeza kiasi hicho! Je, Serikali inafanya utafiti wowote kuhusu athari za kukata miti ya asili na biashara ya mkaa inavyoleta athari kubwa katika mazingira na kilimo chetu kwa ujumla?
Serikali inajua ni miti kiasi gani inayokatwa kutengeneza gunia moja la mkaa linalouzwa elfu 20,000?
Serikali inajua inachukua muda gani kupanda mti utakaokua na kufaa kukatwa tena kwa ajili ya mkaa?
Serikali inafahamu ni kiasia gani cha miti inakatwa kila siku kwa ajili ya kutengeneza mkaa?
Serikali inafahamu ni kiasi gani cha ardhi inayobaki wazi kila siku kutokana na kufyekwa kwa miti ili kutengeneza mkaa?
Serikali inafahamu ni lini nchi hii itafikia ukomo wa kuwa na miti ya kukata kutengeneza mkaa?? Ukweli ni kwamba ipo siku tu miti yote ya kutengenezea mkaa itaisha kama ilivyoisha sehemu nyingine duniani.
Je, tunajiandaje ?