Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,498
- 28,723
Isaac Newton, anayejulikana kwa kufanya uvumbuzi wa aina mbalimbali na muhimu katika sayansi, hesabu, na elimu ya anga, kwa kweli, “hufikiriwa na wengi kuwa mwanasayansi mkuu kabisa na mwenye ushawishi wa pekee sana kuliko wote aliyewahi kuishi.” Ukweli usiojulikana sana wa Isaac Newton ni kuhusu ugunduzi wake katika mambo ya dini, ikiwemo imani yake kuwa mfumo wa Ukatoliki wa Rumi ulikuwa ndiyo mamlaka ya mpinga Kristo. Watu wengine wengi mashuhuri walikuwa na mtazamo huohuo kama vile Mfalme James, Martin Luther (Mwanzilishi wa Kanisa la Lutheran), John Calvin (Mwanatheolojia Mashuhuri), John Wycliffe (Profesa wa Chuo Kikuu cha Oxford), Thomas Cranmer (Askofu Mkuu wa Canterbury), John Knox, na wengi sana miongoni mwa wanamatengenezo wa Kiprotestanti.
Kwa nini Newton pamoja na watu hawa waliofahamika kuwa na uwezo wa juu kabisa wa kiakili, baadhi yao wakiwa waanzilishi wa makanisa, waamini mambo hayo yasiyovutia kuhusu taasisi ambayo inaendesha vituo vya watoto yatima, shule, hospitali, na waumini ambao ni mfano wa kuigwa kama vile Mama Teresa? Kwa ufupi kabisa, walikielewa kitabu cha Danieli, hasa sura ya saba, kwa namna ambayo wengi wameisahau.
Mwelekeo wa Hoja
Hivyo ni kitu gani ambacho Isaac Newton na wengine walifahamu kuhusu kitabu cha Danieli ambacho kiliwafikisha kwenye uamuzi kwamba kumpinga Papa? (Zingatia: ili kuelewa aya chache zinazofuata, utatakiwa kusoma taratibu na kwa kutumia Biblia yako.) Hapa kuna ufafanuzi uliorahisishwa zaidi: Danieli sura ya pili na ya saba ni sura zinazoshabihiana ambazo Mungu, kupitia mifano, anatabiri juu ya kuinuka na kuanguka kwa falme nne kubwa za dunia: Babeli, Umedi/Uajemi, Uyunani, na Rumi. Hivi ndivyo mataifa haya yalivyoainishwa: sura ya pili huelezea sanamu yenye aina nne za madini zikiwakilisha falme nne. Kisha Danieli sura ya saba huelezea, si aina nne za madini, bali wanyama wanne wakiwakilisha falme hizohizo huku ikitoa maelezo ya kina zaidi kwa njia ya vielelezo. Kisha katika Danieli 7:20 mwelekeo hubadilika kutoka kwenye mnyama wa nne (Rumi) kwenda kwenye pembe kumi. Hizi huwakilisha nini? Fungu la 24 huonesha kuwa zile pembe kumi huwakilisha wafalme/falme kumi zilizoinuka baada ya na kutoka Rumi. Kwenye hizo pembe 10, chanzo cha Ulaya ya sasa kilitabiriwa.
Mwisho, mwelekeo hugeuka na kuhamia kwenye “pembe ndogo” ambayo ndiyo watu hawa wasomi walielewa kuwa mamlaka ya mpinga Kristo (ambayo pia hujulikana kama mfumo Katoliki/ Upapa). Mtu fulani anayesoma kijizuu hiki anaweza kufikiri sasa, “Inawezekanaje pembe ndogo inayotajwa katika kitabu cha Danieli kuwa mpinga Kristo? Ni vitu viwili tofauti.” Kwanza, neno “mpinga” katika “mpinga Kristo” humaanisha mambo mawili “kinyume” na “badala ya”: hivyo wanateolojia wengi, wakifahamu hili, wanaelewa neno “mpinga Kristo” kuwa humaanisha watu au taasisi ambazo Biblia huzielezea kuwa zinajidai kutwaa haki za Kristo.
Vivyo hivyo, sehemu nyingine ndani ya Biblia ambazo hutumia maneno tofauti kama vile, “mtu wa dhambi,” “mnyama,” “pembe ndogo,” “kahaba mkuu,” zote huwakilisha mamlaka ya mpinga Kristo kwa sababu zimeelezwa kuwa zinajidhihirisha zenyewe kwa njia ya udanganyifu kwamba zina mamlaka ya Kristo. Hivyo Wycliffe anaelezea, “katika sura ya saba ya Danieli, Mpinga Kristo anaelezewa dhahiri kabisa kwa pembe….”