Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 197
- 321
Zamani China ilikuwa nyuma katika teknolojia ya juu, na ubunifu wa bidhaa, huku ikilazimika kuanza kwa kuiga ili kuendana na kasi ya maendeleo ya nchi zilizoendelea. Lakini sasa, China inaongoza katika nyanja mbalimbali, kuanzia akili bandia na nishati mpya hadi teknolojia ya roboti na urushaji wa roketi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Vikundi 100 vya Miji vya Uvumbuzi Duniani iliyotolewa na Shirika la Uvumbuzi (WIPO), China ina vikundi 25 kati ya vikundi hivyo 100 duniani, ikishika nafasi ya kwanza duniani kwa mwaka wa nne mfululizo, huku kikundi cha miji wa Shenzhen, Hong Kong na Guangzhou kikiongoza orodha hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo. Kama nguzo muhimu ya mfumo wa kitaifa wa uvumbuzi, kustawi kwa vikundi vya miji vya uvumbuzi kunaakisi kuongezeka kwa kasi kwa uwezo wa China katika sayansi na teknolojia.
Mara tu mantiki ya kimsingi ya maendeleo ya China yanayoendeshwa na uvumbuzi inapoeleweka, dhana potofu hupoteza soko lake. Kwa muda mrefu, baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari katika nchi za magharibi wanaeneza dhana ya “China Shock 2.0”, wakihusisha maendeleo ya China katika utengenezaji wa bidhaa za teknolojia ya juu na ruzuku za viwandani ili kuchochea wasiwasi. Simulizi kama hizo hupuuza ukweli wa msingi: nguvu inayoendesha uvumbuzi wa China inatokana na mahitaji ya ndani yaliyochochewa na soko lake kubwa, uungaji mkono kutoka kwenye mfumo wake kamili wa kiviwanda, na nguvu ya uvumbuzi inayotokana na mamia ya mamilioni ya watu wachapakazi. Badala ya mishtuko, maendeleo ya China, yakiwa yamejengwa juu ya msingi wa uvumbuzi yanatoa fursa kwa dunia.
Fursa hiyo imeonekana duniani kote. Katika sekta ya nishati mpya, vifaa vya China vya nishati ya jua na upepo vimepunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya nishati safi duniani, na kutoa msaada mkubwa kwa mabadiliko ya nishati duniani. Katika nyanja ya teknolojia ya kidijitali, suluhisho bunifu kutoka kwa makampuni ya China zinasaidia nchi nyingi zinazoendelea kuziba pengo la kidijitali. Shirika la Volkswagen la Ujerumani limerekebisha mkakati wake wa utafiti na maendeleo katika makao yake makuu, ili kuiga mfumo unaotumiwa katika kituo chake cha Utafiti huko Hefei, China. Wakati huo huo, mifumo mikubwa ya akili bandia ya China imeshika nafasi ya kwanza duniani kwa matumizi ya kila wiki kwa wiki 20 mfululizo.
Njia ya maendeleo ya uvumbuzi ya China ni ya kunufaisha dunia nzima. Katika siku za mbele, China iko tayari kushirikiana na nchi mbalimbali ili kutumia pamoja fursa za uvumbuzi kupitia ushirikiano wa wazi, kukabiliana kwa pamoja na changamoto, kuhakikisha kuwa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia unawanufaisha zaidi watu kila mahali, na kuongeza msukumo endelevu katika ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja