Uvivu huu ni too much sasa

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,517
Kitendo cha wazazi kufurahia shule kufunguliwa huku wakisema maneno mfano:- "afadhali watuondolee usumbufu nyumbani". ..

Hii inaonesha wazi kabisa leo wazazi kuwapeleka watoto shule ni kukwepa usumbufu na kusukumia jukumu la msingi la malezi ya watoto kwa watu wengine... Na si kwa lengo la kuwafanya wapate elimu kama inavyodhihirika...

Kwa msingi huu... Kila mafanikio ya tendo linategemea NIA na KUSUDIO... Basi tusishangae FAILURE, JOBLESS, SINGLE MOTHERS, DRUG ABUSERS na mienendo mingine mitaani mibovu. .. Haya yote ni MATOKEO YA NIA YA MSINGI TULIYOIWEKA AMBAYO NI KUPUNGUZA USUMBUFU NYUMBANI. ..

UVIVU WA JUKUMU LA MALEZI YA WAZAZI KWA WATOTO NI CHANZO CHA YOTE:-
1. Mtoto anaachishwa ziwa mapema anakabidhiwa YAYA wa DayCare. Hujui wanayofanyiwa huko. . .Ni Allah tu anawalinda ukirudi unawakuta wazima.

2. Mtoto katika umri mdogo wa miaka 5 hadi 8 anapelekwa NURSERY BOARDING...

HII SI KWA SABABU UNA PESA BASI UNAMTAFUTIA ELIMU BORA, HAPANA LENGO SIO HILO... LENGO LENU NI KUEPUSHA USUMBUFU KATIKA MALEZI.

NAWAHAKIKISHIA NDUGU ZANGU TUNALITENGENEZA BOMU HATARI SANA AMBALO MADHARA YAKE NI MAKUBWA SANA BAADAE...

KWANINI HATUJALI KIZAZI TUNACHOKIACHA NYUMA.

MZAZI UKIJITAHIDI KUSIMAMIA MWENYEWE MALEZI YA MWANAO VIZURI.UTAMTENGENEZA MTOTO NAMNA BORA AMBAYO IPO KATIKA NDOTO ZAKO.

Utayaangalia madhaifu yaliyotokea katika malezi uliyokulia wewe na njia zako za maisha na utayarekebisha kwa mtoto wako mwenyewe. . . ILI YASIJIRUDIE MAKOSA.

LAKINI KUKWEPA HUKU KWA MALEZI KUTATUGHARIMU SANA AINA YA KIZAZI TUTAKACHOKIACHA...

TUSIKIMBIE WALA KUWATUPIA WENGINE JUKUMU LETU LA MALEZI KWA WATOTO WETU TULIOWAZAA KWA STAREHE ZETU. ..
 
Mimi mwanangu nitamlea mwenywe nikiwa hai Inshaa Allah. . . Kule nilipokosea mimi sitokubali apite huko...

Nitasahihisha makosa yaliyofanyika kwangu kwa mwanangu...
 
Siwezi mpeleka mwanangu mdogo boarding!
Kweli,ni kumuonea na kumnyima mahitaji yake kama mtoto...ila nilipokuwa boarding nilikutana na watu ambao wazazi wao wamewashinda yaani ni wakorofi sana na uvutaji wa sigara+pombe kali hao watu pia wamesoma shule za msingi boarding maalumu za watoto watundu na walioshindikana huko Manyara,shule yao ilikuwa katikati ya mbuga ya wanyama siijui inaitwaje.

Watoto wengine ni watundu kupitiliza unashindwa umfanyeje kuliko umpige umuue bora umpeleke shule huko maporini.
 
Mtoto kuwa mtundu au mkorofi.. . NDIO MATOKEO YA WAZAZI KUWA LELEMAMA KWENYE MALEZI. ...

WAZAZI ZAMA HIZI TUNAOGOPA WATOTO WETU WENYEWE. ..
 
Mimi mwanangu nitamlea mwenywe nikiwa hai Inshaa Allah. . . Kule nilipokosea mimi sitokubali apite huko...

Nitasahihisha makosa yaliyofanyika kwangu kwa mwanangu...
Na ndio hivyo mkuu.inatakiwa iwe hivyo pesa sio kila kitu kiasi kwamba ikulelee mtoto.. never ever.
 
Wazazi wa leo hovyo kabisa, kama kunyonyesha tu wanakwepa ati maziwa yatalala unadhani wataweza kulea watoto hali hata wahenga walichemka kulea watoto japo walijikaza kisabuni huku wakija na msemo "kazi si kulea mimba, kazi kulea mwana".
Hawa wazazi wanaweza kufundisha vitoto vyao kukata viuno na kuvaa nusu uchi tu ndo maana ukipita mitaani vitoto vinashindana kukata mauno na kuvaa nusu uchi tu.
 
Back
Top Bottom