Binafasi nimefurahi sana Nchimbi kukosa watu wake.
KIla kitu kitakuwa wazi sasa. Sina kambi yoyote, ila ninapenda sana mawazo huru kwa kitu. Hii ndiyo inafanya nchi zingine zinaendelea sana. I mean kitendo cha Nchi kumkandamiza Nape was injustice and untimely.............
UVCCM na vikumbo vya vigogo
MATOKEO ya uchaguzi wa wenyeviti wa mikoa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) pamoja na wajumbe wa Baraza Kuu la umoja huo Taifa, yanatarajiwa kudhoofisha sana kundi la uongozi wa juu wa sasa wa umoja huo ambalo ni kati ya makundi yanayovutana sana ndani ya Chama cha Mapinduzi ( CCM), imefahamika.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa baadhi ya vigogo wa kitaifa wa CCM, walilazimika kufunga safari kwenda kusaidia ushindi wa wagombea waliomo katika kambi zao dhidi ya kambi nyingine mikoani.
Sababu kubwa ya vigogo hao kujitosha wazi wazi katika dakika za mwisho kusaidia wagombea wanaowaunga mkono katika kinyanganyiro cha uenyekiti wa UVCCM mkoa na ujumbe wa Baraza Kuu la umoja huo, ni kuhakikisha makundi yao ya kisiasa ndani ya CCM yanakuwa na misuli katika jumuiya hiyo.
Inaelezwa kuwa kama kundi mojawapo litafanikiwa kuwa na idadi kubwa ya wenyeviti wa mikoa wa UVCCM, litakuwa limejiimarisha vizuri kutekeleza malengo yake ya kisiasa ndani ya umoja huo, na katika chama hicho kikongwe nchini.
Kwa mujibu wa baaadhi ya wanasiasa walizoungumzia hali hiyo, kinacholengwa sasa na kila kundi ndani ya CCM ni kuwa na nguvu katika Baraza Kuu la UVCCM.
Baraza Kuu la UVCCM ni kati vya vyombo muhimu na vyenye nguvu katika kupanga mustakabali wa umoja huo, ambao nao umejikuta ukitumbukia katika mivutano ya kisiasa.
Tofauti na ilivyotarajiwa, katika miaka ya hivi karibuni UVCCM imekuwa ikitumbukia zaidi katika mivutano ya kisiasa na baadhi ya wanachama wake, badala ya kutazama mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2005 ya CCM.
Kutokana na matokeo ya awali ya uchaguzi wa wenyeviti na wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, inadaiwa kuwa hali ya kundi mojawapo kati ya hayo yanayovutana ndani ya CCM ni mbaya baada ya safu ya wagombea wake kuanguka.
Taarifa zaidi zinadai kuwa hata nguvu za Mwenyekiti wa sasa wa UVCCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, ambaye analazimika kuachia madaraka hayo Jumapili, Desemba 14, zipo shakani.
Wasiwasi uliopo ni kwamba kama Dk. Nchimbi atafanikiwa kupata wajumbe wachache wanaomuunga mkono katika Baraza Kuu la UVCCM, hasa baada ya uchaguzi wa wenyeviti na wajumbe kutoka mikoani kukamilika huo unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wa misuli yake katika UVCCM.
Alama za nyakati zinabainisha kuwa kama sehemu kubwa ya safu ya wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM baada ya uchaguzi itakuwa haiko upande wa Dk. Nchimbi, huenda maamuzi yake aliyowahi kufanya awali na viongozi wenzake yakatenguliwa na Baraza hilo jipya.
Ikumbukwe kuwa kati ya majukumu ya awali yatakayofanywa na Baraza hilo jipya la UVCCM ni pamoja na kusikiliza rufaa ya kada machachari wa CCM na UVCCM, Nape Nnauye.
Nape alivuliwa uanachama wa UVCCM akidaiwa kusema uongo, hatua ambayo iliibua hisia za kisiasa kwamba ni njama za kundi linalompinga ndani ya CCM ili kumkwamisha asigombee uenyekiti wa umoja huo ngazi ya Taifa.
Nape alivuliwa uanachama wake baada ya siku kadhaa kupita tangu atamke kupinga mradi wa ujenzi wa jengo la kitenga uchumi katika makao makuu ya UVCCM, jijini Dar es Salaam .
Licha ya Nape kuvuliwa uanachama, uongozi wa Dk. Nchimbi ulipendekeza kada huyo anyanganywe nyadhifa zake zote ndani ya CCM, mapendekezo ambayo yaliungwa mkono na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba.
Hata hivyo, mapendekezo hayo yalipuuzwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete ambaye alitamka ndani ya Kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM mjini Dodoma hivi karibuni kuwa Nape ataendelea na nyadhifa zake zote ndani ya CCM.
Kwa muda mrefu sasa CCM imekuwa katika mvutano wa kisiasa, inayochangiwa na msimamo tofauti miongoni mwa wanachama wake.
Mvutano huo umevuka mipaka kutoka katika chama hicho hadi kupenya katika baadhi ya mihimili ya Taifa, huku dalili zikibainika kuwa Bunge na Serikali ni kati ya taasisi nyeti zilizoingiliwa na hisia za mivutano ya kisiasa.