Hii kitu inaitwa ufisadi kama ndio sera ya CHADEMA basi hawafai kuongoza nchi hii. Mnatakiwa kabla ya kuiunga mkono CHADEMA mjue itatatua vipi matatizo ya watanzania. UFISADI siyo kitu ya CCM tu ni kitu watanzania wote tunayo. Hawa mafisadi wakubwa wapo kwa sababu tu wamepata nafasi ya kufanya ufisadi mkubwa. Lakini amin amini nawaambia watanzania wengi ikiwepo nyie mnaopiga makelele fisadifisadi ni vifisadi vidogovidogo. Unamwajiri Mtanzania dukani kwako ukimwacha mwezi hujamkagua tu ukija kupiga hesabu amekuliza. Unaenda dukani kwa Kanjubai kununua vitu mfanyakazi anakwambia bosi hii kitu nitakuletea kwako nipe namba ya simu nikutuletee nitakuuzia kwa nusu ya bei, tayari Kanjubai kalizwa. Unakwenda bandarini kodi unajua kabisa ni 5m mtu anakwambia nipe 1.5m nikufanyie kodi yote 3m; watanzania hawahawa tena wengine ni CHADEMA wakeleketwa kabisa na wengine CCM wakeleketwa kabisa tatizo ni watu sio CCM. Unaenda dukani kununua kitu muuzaji anakuambia unataka risit au nikupe risiti ya kutembea na mzigo, ukikubali tayari wote mmefanya ufisadi. Mkipewa dili ya mabilioni mtafanya kama hao manaowalalamikia tu. Mtu anakuja kukuuzia gold ukienda kuuza unaambiwa gold fake wote huu ni ufisadi na unafanywa na watanzania wa vyama vyote. Sijui kama wafanyakazi wote wa serikali, mashirika na binafsi ni wanaCCM kuna makesi mengimengi ya wizi wa mali za umma na za binafsi unaofanywa na wafanyakazi wa serikali na wa kampuni binafsi ambao wengine ndio nyie wengi mnaopiga kelele za fisadifisadi. CHADEMA wamekuwa wapokea misaada mingi toka kwa vyama rafiki na pia ruzuku hamjiulizi kwa nini mpaka leo hata ofisi ya hadhi wameshindwa kuwa nayo. Ukichunguza utakuta fedha ya ujenzi wa jengo kubwa lenye hadhi ya CHADEMA imetolewa lakini imechakachuliwa huu wote ni ufisadi na hauko CCM. Ugomvi wa kina zito na CHADEMA halafu baadae na CCM ulitokana na kuhoji kwa nini akaunti zao zisikaguliwe na mkaguzi mkuu wa serikali wote waliogopa kwa sababu kuna viufisadi. Kwa hiyo suala la viufisadi limo miongoni mwa watanzania wote na sio upande mmoja yaani CCM kama wanasiasa wanavyojaribu kuingia ndani ya vichwa vyenu. Sikatai kuwa kuna wanacCCM ni mafisadi lakini msikatae pia kuna wanaCHADEMA ni mafisadi. Hawajapata chance to ya kufanya ufisadi mkubwa kwa kuwa hawako kwenye utawala. Watupe mkakatu mahsusi watapambanaje na ufisadi wa watanzania na sio wa CCM. Maana ukiondoa wa wanaCCM tu bado tatizo halitaisha wataibuka wa CHADEMA. Hii kitu mtu anaoneshwa 10billion anavunja katiba ya chama chake na kuvunja mtazamo wa chama chake ni dalili tosha akiingia kwenye raslimali atazishughulikia tu. Najua kuna watu wana hasira na CCM kwa sababu mbalimbali. Yeyote anayekuwa madarakani lazima ataonekana mbaya na baadhi ya watu na mzuri na watu wengine. Tujaribu kutafuta mtu anayeweza kupata suluhu ya hayo matatizo na sio kukimbilia ufisadi ufisadi. Kwa sehemu kubwa sera za CHADEMA zimechotwa kutoka CCM na hata vitabia vingi vya CCM CHADEMA amevichota na hata hotuba za waasisi wa CCM ndio CHADEMA anazitumia ikiwepo kumpokea mgombea wake wa urais wa sasa. Hivyo tegemea "mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya" Chupa zikiwa ni CHADEMA na CCM. Mimi nadhani badala ya kuifanya siasa kama yanga na simba tutambue siasa ni kitu kinachogusa maisha. Wanasiasa wanatafuta zaidi ulaji wao na familia zao. Kwa kuwa sioni jipya kwa CHADEMA bado nadhani CCM iendelee kupewa dola huku tukitafuta Chama kitakachojipambanua kutatua matatizo ya watu kuliko inavyofanya CCM. Chama cha kuirithi CCM na kuleta mabadiliko kwa sasa sikioni; labda kama anatolewa tu kwa chuki binafsi. UKAWA imebeba vyama vyote vya upinzania na kuviingiza shimoni. Haya mwanzilishi wa UKAWA huyoooo. Mnabaki kutafuta sentesi za kuperemba; ukweli hiyo kitu si sawa. Ila iko siku wale wazuri kutoka CCM, CHADEMA na vingine vidogodogo wataungana na kuleta chama cha kuibadili CCM kama haitarekebisha baadhi ya mapungufu yanayolalamikiwa na wananchi.Ukimtaja lowasa kuwa ni fisadi ujue yeye alikuwa ni cha mtoto wenye ufisadi wamo ndani ya nyumba (CCM). Bado majambazi hawa wanatutawala ee Mola waangamize maficcm
Kijana wa UKAWA 1anapiga vijana wa ccm 
Unajua Seif Sharif Hamad aka Maalim Seif ameshamkata ng;ombe kamba ya pua aka ujamu ,sasa ni vijana kujihami popote pale hao wanaokiita vijana wa CCM wakitokeza pua basi liwalo na liwe ,ila haya sio kwa sasa kunasubiriwa kashkash za mikutano zianze ,yaani jamaa wanakisasi kibaya na wanaojiita vijana wa CCM ,haswa wale wanaokaa barabarani kusubiri wanaorudi kwenye mikutano ,safari hii mtazisikia habari rediona ,wacha wao wajipange na upande wapili wajitayarishe ,lazima miccm itakubali kama samaki haishi nchi kavu.
VIJANA WENYEWE UNAOWAASA WAMEDATA AKILI KWA DHIKI NA SHIDA
ajabu sana/