Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wakiwemo Wenyeviti wa Mikoa wameungana kwa sauti moja kulaani vikali kile walichokiita vitendo vya baadhi ya wanaharakati na watu wengine kutoka nchi jirani wanaojaribu kuvuruga amani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Msimamo huo umetolewa siku ya Jumamosi katika Jiji la Dodoma mbele ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Ali Kawaida, wakati wa uzinduzi wa matembezi ya amani ya Kijani First Time Voters, yaliyoandaliwa na UVCCM kwa ajili ya kuwahamasisha vijana wapiga kura wa mara ya kwanza kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Wenyeviti hao wa UVCCM kutoka mikoa mbalimbali wameeleza kuwa amani ya nchi ni tunu isiyopaswa kuchezewa na kwamba vijana wa Tanzania hawawezi kukubali kuona taifa lao likivurugwa kwa hila au ushawishi wa watu kutoka nje.
Wamesisitiza kuwa vijana wa CCM watasimama imara kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa kisiwa cha amani, na kwamba wataendeleza juhudi za kuelimisha wenzao kuhusu umuhimu wa kuilinda nchi dhidi ya ushawishi wenye misingi ya kuchochea fujo au uchochezi wa kisiasa.
Source: Jambo TV