AK-47
JF-Expert Member
- Nov 12, 2009
- 1,373
- 202
UVCCM leo wameonyesha ukomavu wa hali ya juu na kuguswa na maslahi ya taifa baada ya kutoa matamko kadhaa likiwemo la kuitaka serikali kuwataja hadharani wamiliki wa Richmond ili wabebe mzigo wa kuilipa Dowans sh bilioni 94 inayodai Tanesco. Aidha wametaka bodi ya mikopo ivunjwe kwa kuwa imeshindwa kazi kiasi cha kuzusha maandamano ya wanafunzi wa vyuo kila kukicha. Kama haitoshi wameitaka serikali kutoa ajira kwa vijana badala ya kuacha hali ilivyo sasa ambapo vijana wengi wapo mitaani hawana ajira jambo ambalo ni hatari.