UVCCM wawasaka BAVICHA Dodoma, waandaa vijana 3000

UVCCM wawasaka BAVICHA Dodoma, waandaa vijana 3000

N
Umoja wa Vijana CCM, wametua mjini Dodoma ambapo Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unatarajiwa kufanyika wiki hii huku wakiwatafuta wajumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) ambao awali walipanga kuzuia kufanyika kwa mkutano huo.

Akiwa katika Ofisi za UVCCM – Dodoma jana, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefika mjini hapo pamoja na mambo mengine kusimamia ulinzi wa chama na viongozi wa chama hicho lakini hawaoni BAVICHA.

“Nipo hapa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuongoza shughuli za ulinzi wa chama na viongozi wetu, kama Mtendaji Mkuu na mtoa maelezo ya itifaki. Kwa bahati mbaya kwa muda wote sijaona dalili wala harufu ya BAVICHA. Hii inadhihirisha kwamba kusema na kutenda ni vitu tofauti,” alisema Shaka.

Aliongeza kuwa wamejipanga vizuri na wameandaa vijana 3,000 maalum watakaofanya kazi ya kulinda mkutano huo uliolenga kufanikisha kumkabidhi Uenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kwa mujibu wa katika ya chama hicho tawala.

Aliwahakikishia usalama wajumbe wa Kamati Kuu akiwataka kuwa na amani kwani wataingia na kuondoka mjini humo wakiwa salama.

Juzi, BAVICHA walitangaza kurudi mjini Dododoma kwa lengo la kufanya Mkutano wao wa Kamati ya Kiutendaji baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwataka kusitisha adhma ya kutaka kuzuia kufanyika kwa mkutano wa CCM.

Chanzo: Dar24
Ni vijana 30,000. Ni sawa na kamji kadogo kama Kimandolu. Batalieni 30 - sawa na kikosi cha Brigedia Kimario kilichowateka Walibya na PLO kwenye vita vya Kagera.
 
Kama wako imara hao vijana wa ccm basi wawaambie Polisi wanaosombwa mikoa jirani wakiwa na vifaa vya kijeshi waondoke Dodoma wao watalinda mkutano wao halafu wasikilizie mziki Wa Bavicha.
 
Sijawahi kuona kijana anayeandaliwa kuja kuwa kiongozi hapo baadae ana akili finyu kama hawa sijui UVCCM, kama BAVICHA wangeenda Dodoma wangekutana na Polisi, sasa ina maana hawa UVCCM wanataka kutuaminisha kuwa Jeshi la Polisi linazidiwa na hao BAVICHA mbona halijatoa taarifa ya kushindwa na kama wangeshindwa wangewasemesha ndugu zao JWTZ, hebu nyinyi UVCCM muwe mnaomba busara kutoka kwa wazee ndani ya chama kabla ya kutoa hayo matamko yenu, au UVCCM pia siku hizi inafanya uanaharakati na kuhamasisha vurugu au labda mimi nimepitwa na jambo hili.
 
Ole Sendeka amewakataa UVCCM amesema hamna ulinzi wowote wanaofanya wanasherehesha genge tu.
 
Aliongeza kuwa wamejipanga vizuri na wameandaa vijana 3,000 maalum watakaofanya kazi ya kulinda mkutano huo uliolenga kufanikisha kumkabidhi Uenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kwa mujibu wa katika ya chama hicho tawala.
Sasa huyu anamaanisha polisi nao ni sehemu ya UVCCM?
Mimi siku za nyuma niliona kwenye TV magari ya polisi na polisi
wakifanya mazoezi ya kulinda mkutano huo,na pia msemaji wa
polisi alishasema BAVICHA wakienda dodoma watakutana na mkono wa dola
sasa huyu M_UVCCM anawakilisha kundi gani?
 
Waelekeze nguvu kwenye lengo la uchaguzi wakicheza karata vibays eti wanakuja na hoja za kupambana na BAVICHA JPM ataifuta UVCCM maana yeye anaangalia watetezi wa wanyonge.
kwahiyo mtetezi wa wanyonge ni nani mkuu?
 
we vipi?thread imesema walioko dodoma ni uvccm ambao wanawatafuta bavicha hewa maana walishasema hawatakwenda baada ya zuio la mwenyekiti wao.kwa hiyo hao uvccm ndio wazururaji hapo dodoma.
Kumbe hamuendi tena, ila wasiokua na kazi niwale wanaovamia sherehe isiyowahusu..
 
Back
Top Bottom