UVCCM wawasaka BAVICHA Dodoma, waandaa vijana 3000

Tunzo

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
4,066
2,363
Umoja wa Vijana CCM, wametua mjini Dodoma ambapo Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unatarajiwa kufanyika wiki hii huku wakiwatafuta wajumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) ambao awali walipanga kuzuia kufanyika kwa mkutano huo.

Akiwa katika Ofisi za UVCCM – Dodoma jana, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefika mjini hapo pamoja na mambo mengine kusimamia ulinzi wa chama na viongozi wa chama hicho lakini hawaoni BAVICHA.

“Nipo hapa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuongoza shughuli za ulinzi wa chama na viongozi wetu, kama Mtendaji Mkuu na mtoa maelezo ya itifaki. Kwa bahati mbaya kwa muda wote sijaona dalili wala harufu ya BAVICHA. Hii inadhihirisha kwamba kusema na kutenda ni vitu tofauti,” alisema Shaka.

Aliongeza kuwa wamejipanga vizuri na wameandaa vijana 3,000 maalum watakaofanya kazi ya kulinda mkutano huo uliolenga kufanikisha kumkabidhi Uenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kwa mujibu wa katika ya chama hicho tawala.

Aliwahakikishia usalama wajumbe wa Kamati Kuu akiwataka kuwa na amani kwani wataingia na kuondoka mjini humo wakiwa salama.

Juzi, BAVICHA walitangaza kurudi mjini Dododoma kwa lengo la kufanya Mkutano wao wa Kamati ya Kiutendaji baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwataka kusitisha adhma ya kutaka kuzuia kufanyika kwa mkutano wa CCM.

Chanzo: Dar24
 
Watu wanahamu ya kuleta vurugu, jamani hiyo si kazi ya polisi au UVCCM wamekuwa polisi
 
Waelekeze nguvu kwenye lengo la uchaguzi wakicheza karata vibays eti wanakuja na hoja za kupambana na BAVICHA JPM ataifuta UVCCM maana yeye anaangalia watetezi wa wanyonge.
 
, wamesubiri polisi wamewasafishia bavicha kwa kuwakamata halafu ndo wanajitokeza huku wanabana pua" tunawatafuta BAVICHA"

Wawaambie polisi wakae kando wasikilizie mziki wa BAVICHA ,
 
Watu wanahamu ya kuleta vurugu, jamani hiyo si kazi ya polisi au uvccm wamekuwa polisi
unajua sisi watanzania machafuko ya kisiasa tunaona kwenye TV ndio maana hatujui maana yake yakitokea watu wakafa watu wakapata ulemavu hakuna mtu atajaribu tena waulizeni wakenya wanasimulia hadi leo
 
Nilichojifunza kwenye hili suala ni kwamba UVCCM sio wabunifu bali wanawaiga BAVICHA. Na sio hilo tu, hata CCM kwa kiwango kikubwa sio wabunifu bali huwaiga CHADEMA.
 
Nilichohifunza kwenye hili suala ni kwamba uvccm sio wabunifu bali wanawaiga bavicha. Na sio hilo tu, hata ccm kwa kiwango kikubwa sio wabunifu bali huwaiga cdm.
Sumaaye:Nimekuja kuwapa uzoefu Chadema

Lowasssa:nitakibadilisha chadema kutoka chama cha wanaharakati na kuwa chama cha siasa.

Hizi ni kauli za makapi ya CCM
 
Hivi;siasa nchini imeshakua uadui?Vijana wenzetu mliomezwa na itikadi za vyama,chukueni tahadhari na kuivuruga amani huko Dodoma.
 
Sumaaye:Nimekuja kuwapa uzoefu Chadema

Lowasssa:nitakibadilisha chadema kutoka chama cha wanaharakati na kuwa chama cha siasa.

Hizi ni kauli za makapi ya CCM

Maneno ya hao vimeo wa ccm ni kama.kujifurahisha, lakini ukweli ulio dhahiri hao vimeo wenu wataendelea kukutana na wakati mgumu ndani ya cdm. Tupe muda utaamini maneno yangu.
 
Hahaha baada ya BAVICHA kusitisha safari yao UVCCM ndio wanaibuka? siasa tamu sana ukiwa na hasira utaumia
 
Kwa nini hawa nao wasikamatwe na kufikishwa mahakamani kwa matamshi yao yanayochochea chuki? Kwanza mkutano ni tarehe 23, hawa wote wako Dodoma kwa kibali? Polisi acheni double standard bana, nchi ni yetu sote hata tusio na vyama.
 
Ule msako wa makonda sasa uhamie na dodoma maana majobless wa ukawa wamehamia huko kwa muda..
 
Maneno ya hao vimeo wa ccm ni kama.kujifurahisha, lakini ukweli ulio dhahiri hao vimeo wenu wataendelea kukutana na wakati mgumu ndani ya cdm. Tupe muda utaamini maneno yangu.

Walisha wanunua
Hamna jipya
 
Ule msako wa makonda sasa uhamie na dodoma maana majobless wa ukawa wamehamia huko kwa muda..
we vipi?thread imesema walioko dodoma ni uvccm ambao wanawatafuta bavicha hewa maana walishasema hawatakwenda baada ya zuio la mwenyekiti wao.kwa hiyo hao uvccm ndio wazururaji hapo dodoma.
 
we vipi?thread imesema walioko dodoma ni uvccm ambao wanawatafuta bavicha hewa maana walishasema hawatakwenda baada ya zuio la mwenyekiti wao.kwa hiyo hao uvccm ndio wazururaji hapo dodoma.
hapo sasa
 
Back
Top Bottom