UVCCM Wapinga Balozi Juma Mwapachu Kurejea CCM, Wataka Waliompokea Watimuliwe

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
1.jpg

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Hai (UVCCM),Arnold Swai amepinga ya kurejea ndani ya chama hicho kwa mwanadiplomasia na mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Juma Mwapachu.

Balozi Mwapachu, juzi alitangaza kurejea CCM kwa madai ya kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.

Akizungumza na wanahabari jana mkoani hapa,Swai alisema kuwa chama hakipaswi kumpokea mwanasiasa huyo kwa madai kuwa ni msaliti huku akienda mbele zaidi na kutaka waliompokea wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa kanuni za chama.

"Ni lazima tujiulize, hivi mwanadiplomasia huyo angekuwa tayari kurejea CCM kama mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa angeshinda urais?" alihoji na kuongeza:

"Hatuwezi kumpokea msaliti kama huyu, wakati chama kilipokuwa kwenye mapambano aliondoka tena kwa kejeli, leo chama chetu kimesimama imara chini ya mwenyekiti wetu Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ndio anarudi na wimbo uleule kwamba chama kimemlea, haikubaliki."

Alisema wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,baadhi ya makada maarufu wa CCM walikisaliti chama huku wakitoa kauli za kejeli na kusababisha mpasuko ndani ya chama ambao majeraha yake hayajapona.

Mwenyekiti huyo alieleza kukerwa na kauli ya Balozi Mwapachu kwamba chama ndo kimemlea na kwamba hayo si maradhi ya kumuua mtu bali yanatibika, lakini dhambi ya usaliti haitibiki

"Nguvu kubwa iliyotumiwa na CCM kuwanadi wagombea wake ilisababishwa na wasaliti kama hawa,nawaomba viongozi wa ngazi za juu kutofumbia macho jambo hili kwani ni hatari kwa ustawi wa chama chetu." Alisema

Balozi Mwapachu alirejea CCM juzi na kupokelwa na mwenyekiti wa CCM kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, Athuman Mareenda, ambaye alimkabidhi tena kadi ya uanachama wa chama hicho.

Chanzo: Mpekuzi
 
Wana hoja; dawa ya msaliti ni kumtumbua sio kumbeba!
 
Ni ngumu ila ndiyo tena. Vyama ni vya wote. Suala la kumkataa ni lazima liwe na nguvu kikatiba. Ukichukulia alikua muwazi wakati wa kutoka kama ilivyokuwa wakati wa kurudi
 
ACHENI ULAGHAI NYIE! CCM TOKA LINI KIMEKUWA KISAFI HIVYO?! CCM NI CHAMA AMBACHO HATA OSAMA NA WAFUASI WA BOKO HARAM NA ISIL WANA SIFA NA HAKI YA KUJIUNGA.!
 
jana:chadema hatupokei mafisadi
leo:lowassa apokelewa chadema
KILA JAMBO LINA ASILI YAKE, NA LOWASSA KUNA MAHALI ALITOKEA, HUKO ALIFUNDISHWA,HUKO KUNA WAALIMU, NDIO KWETU, NDIKO WANAKOTOKEA WENGI,WENGINE WANARUDI,NDIKO PANAKOSAFISHWA KWA SASA, NI KWETU, NI PACHAFU....
 
Rais Magufuli ni erratic. Sijui huyu chipkizi analalamika nini. What is the condition of the Daesassalaam Stock Exchange?
 
Nadhani ikifika wakati wa kusafisha chama kwa kutimua wasaliti hatapona
 
Huyo kijana wa UVCCM ana jina la Kaskazini, tumchunge isije ikawa anatumiwa na upinzani.
 
CCM inabidi imuangalie vzr uwenda alichotaka hakikufanikiwa sasa anarudi kujipanga tena...
Aangaliwe kimakini sana kwa hata Mwenyezi amoendi MTU msaliti..
 
Back
Top Bottom