UVCCM wamfukuza mjumbe Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM wamfukuza mjumbe Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 30, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  [​IMG]BARAZA Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha limemfukuza Mjumbe wa Baraza la Vijana Taifa anayewakilisha mkoa huo, Mrisho Gambo, kwa madai ya kukihujumu chama hicho.

  Mrisho anatuhumiwa kuunga mkono vyama vya upinzani na kusababisha Jimbo la Arusha lichukuliwe na mbunge kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Hatua hiyo ilitangazwa na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Arusha, James Millya, juzi usiku. Tangazo hilo lilipokewa kwa shangwe na wajumbe wenzake.
  James alisema kuwa uamuzi wa kumfukuza Gambo umetokana na tuhuma na taarifa zenye ushahidi kuwa Gambo amekuwa ni kiini cha kukivuruga chama na kushawishi vijana wa CCM kuchagua upinzani.

  “Sisi wajumbe wa Baraza tumechoka na Mrisho Gambo, tunasema basi, inatosha, kama anataka kwenda upinzani aende moja kwa moja, hatutaki kuendelea kumuona anaendelea kutuvuruga, tunamwangalia, na hapa tunaandika barua rasmi kwa Baraza la Vijana Taifa kuwa hatumtaki na sisi ndiyo tuliomchagua na sasa hatumtaki, ushahidi tunao wa kutosha wa jinsi anavyohujumu chama,” alisema Millya.

  Kwa upande wake, Gambo alipoulizwa na MTANZANIA juu ya uamuzi wa kufukuzwa, alisema, “Bado sijapata barua rasmi kuhusu suala hilo, lakini mimi ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa na mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa, kwa mantiki hiyo uteuzi wangu wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Jakaya Kikwete, na ambayo kwa mujibu wa Katiba ya CCM ndiyo yenye mamlaka ya kunivua uongozi.
  “Lakini lazima ujue kuwa nitaendelea kusimamia itikadi ya chama changu ya kusema ukweli daima na fitna kwangu mwiko.”

  Baraza hilo limesema linamtambua na kumjali Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na kumtaka afanye kazi zake kwa biidi na asikubali kutishwa.
  “Rais Kikwete ni Rais imara, sisi tuko naye na tunamwambia asitishiwe nyau na mtu yeyote,” alisema Millya

  Vijana hao pia wametaka makundi ya kisiasa ndani ya CCM yafe na viongozi wasiendeleze malumbano ya nani atakayekuwa rais wa kipindi kijacho.
  Millya alisema kuwa ni jukumu la wananchi kujadili na kuona ni nani anayefaa kuwa kiongozi wao.
  Alisema ni wajibu wa wananchi kuamua ni nani awe rais wao ajaye hata kama atakuwa akitoka upande wa Kaskazini mwa nchi.

  Katika hatua nyingine, vijana hao waliomba Serikali irejeshe huduma ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), na kueleza kuwa ni aibu kwa nchi kukosa huduma hiyo.
  “Haiwezekani Rwanda na Burundi wakawa na huduma ya ndege zao wenyewe, sisi tukakosa huduma hiyo, tunamuomba Rais Jakaya Kikwete avalie njuga suala hili,” alisema Millya.

  Pia walipongeza huduma ya dawa inayotolewa na Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila, na kutaka Serikali isaidie kuboresha miuondombinu.
  Wageni rasmi katika Baraza hilo walikuwa ni Mbunge wa Arumeru Magharibi Godluck ole Medeye, aliyefungua mkutano saa tano asubuhi; na Mkuu wa Wilaya ya Longido, James ole Milliya, aliyefunga mkutano huo saa tatu usiku.
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Tumewazoea...muda huu nina kazi siwezi fatilia habari za hawa wapuuzi....
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WATANZANIA HADI KUFIKA 2015 MAADUI ZETU MAFISADI WALIOKO NDANI YA CCM NA WALE WALIOJIFICHA NDANI YA VYAMA VYA UPINZANI WATAKUA WAMEBAINIKA WAZI ZAIDI NA KWA AIBU SANA

  Kadri siku zinavyoendelea, Wa-Tanzania tutegemee watu wazuri kwetu wakidhalilishwa na hata kufukuzwa CCM huku MAFISADI na Mawakala wao katipigiwa makofi na kuitwa mishujaa.

  Siku zote chanda chema huvishwa pete, Mrisho na LIKE-MINDED Tanzanian Youths ndani ya CCM na wala msitikisike kitu hapo tena ondokeni mapema kabla nyumba hiyo haijaanguka kwa madhara moto mkubwa ulioishika hivi sasa huku kila mmoja tukijua fika kwamba kule chumbani kumefichwa mipipa ya petroli (MAFISADI) ambayo moto utakapo yafikia miaka michache ijayo basi hali yenyewe haitoelezeka kwa CCM na hatima yake nchi.

  Amini msiamini kuna A MAJOR POLITICAL RE-ALIGNMENT inakuja nchini kabla ya 2015 ambapo matokeo yake itakua tu ni sawa na Wa-Tanzania kuchagua kuwavua uchi wa mnyama MAFISADI wakirundikana kwenye kona moja kisiasa.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ACHENI JAKAYA KIKWETE AISHI KWENYE MABAWA YA MIDEGE ANGANI AKICHAGUA ILMRADI GHARAMA YA KODI ZETU KUIFADHILI MIRADI HIYO HAIZIDI ROBO YA TIJA TUNAYOVUNA KWENYE MAPENZI YAKE HAYO!!!

  Hivi PakaJimmy, huenda huyu mwenye bandiko lake,anayeshabikia ovyo matembezi ya Mhe Jakaya Kikwete Wizara moja baada nyingine bila kutupa VERIFIABLE FACTS and FIGURES juu ya ushabiki wake, akawa ni Rweyemamu wa Ikulu kule Magogoni, Katibu Mwenezi na Propaganda CCM au ndio tuseme Zilipendwa Mzee Tyson Wassira Waziri wa Uhusiano leo hii kaamua kutoka Ki-Doti-Komu vile nini??

  Tathmini ya huu Mradi wa ziara ya Mhe Kikwete Mi-Wizarani kamwe haitofanywa na akili za kilabuni hivi; tutakwenda mbele kidogo na kutaka ripoti iliyoandaliwa baada ya kutumia vigezo vya kisayansi (Project Monitoring and Evalution) ili kubaini kwamba tangu anapanga ziara hii.

  Ni sharti JK atujibu kwa mtaji wa kodi zetu anazoendelea kutumia hivi sasa katika 'Kikwete Tembelea Wizara Project' (KTWP) na wal si kutupigia kelele za kishabiki hapa; huko kwenye siasa za kishabiki Vijana hatumo bali ni kwamba TIJA tu ndio tuwekewe mezani kweupe. Washiriki wa KTWP watujibu maswali kama vile Kikwete: (1) alikua na makusudio yepi, (2) kakuta hali halisi ikoje, (3) hali hiyo inajilinganisha vipi na kipinda cha mara ya mwisho mradi kama huo ulipotendeka, (4) Wa-Tanzania tumelazimika kuwekeza kiasi gani katika hiyo Month-Long Kikwete Project na iko wapi thamani ya kodi zetu mle????

  Dr Bila ripoti tunaomba tangu ziara na familia yako mbugani na kote huko mikoani. Wapinzani na wabunge wote kwa ujumla nanyi tutawabana sana juu ya jinsi gani Viongozi Waandamizi wanavyotumia kodi zetu na TIJA za wazi zinazopatikana kwenye kile watendalo tukilinganisha na gharama iliotumika. Tukizingatia nidhamu kama hii tangu ikulu hadi nyumba kumi mitaani kwetu basi wananchi tutaona ACCOUNTABILITY wa hali ya juu!! Huko nyuma JK ameripotiwa kuwa na ziara nyingi sana na hata wakati mwingine kudaiwa kuwakera walipa kodi.

  Kwangu mimi sitojali ziara zake ni nyingi kiasi gani ba ni thamani ya tija iliyopatikana ukilinganisha na gharama tulizowekeza mle. Tena mimi nitamuunga mkono sana JK akiweza basi kila siku awepo tu kwenye pipa angani kila kukicha ilmradi UNPOLITICISED WATCHDOG POLITICAL GROUPS AND PARLIAMENT wanaturidhisha katika hili bila swali kubaki kichwani mwetu.

  Tunasupibi ripoti bungeni juu ya matumizi kwenye mradi huu na vile vile kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi akajikite katika TIJA zenye kugusika na kuonekana tulizozivuna kwenye KTWP. Hatutaki blaa blaa na longo longo nyingi za mwaka wa 47 ambayo ndio haswa imetunashisha kama taifa kwenye huu umasikini gundi mabegani.

  Mhe Kikwete kama CEO wa Tanzania kwa sasa, kama angelikua anaongoza kampuni ya kibiashara lazima angelazimika kuridhisha Wajumbe wa Bodi (Wahe Wabunge, nchi wahisani na Asasi za Kiraia husika) na haswa wamiliki wa kampuni (sisi wananchi) juu ya kila atendalo na faida ya kuonekana bila siasa, kwa nini ishindikane kwa ngazi ya taifa endapo kweli hatukusudii kuja kupata misaaada to Rwanda au hata Kenya kutupa LIFTI KWENYE NDEGE YAO toka kwenye hatari Libya????
   
 5. m

  mao tse tung Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UVCCM wafukuzeni wale wote wasafi, wawazi waadilifu na makini mbaki huko wale mafisadi wa kutupwa,mafisadi, msio kuwa na uwezo, mnaofanya kazi kwa hisia kwa misukumo ya matumbo yenu na matakwa ya babazenu walioifilisi nchi na kuifikisha hapa ilipo.
  udumu ufisadi ndani ya CCM na maotea yake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii mbona inaeleweka, huyu Gambo hanunuliki na ana akili timamu na msimamo. hao huwa wanakomoliwa ndania ya CCM. Sio lazima, laki nafikiri kuna chama kinachomfaa zaidi.:rip:
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  things fall apart.....
   
 8. Joyum

  Joyum Senior Member

  #8
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yangu macho na masikio mwaka huu nitaona na kusikia mengi toka kwenye lichama letu tawala na babe lisilo na mwelekeo sisiemuuuuuuuuuuu
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Huyu Gumbo si alitoa kauli last week kuhusu wazee wa CCM?...au ndio sababu
   
 10. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  chadema chukua huyo jamaa...! VITA YA PANZI FULAHA YA MWEWE..!

  SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA...! R.I.P SISIEMU!
   
 11. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Kikao cha mkoa hakina mamlaka ya kumtimua mjumbe wa ngazi ya mkoa nadhani Lowasa & Co wanaweweseka.Ningekuwa mshauri wa Gambo Mrisho hakika nisingemshauri aondoke CCM ningemshauri abaki huko huko kwani tunahitaji kusikia sauti mbadala.
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kwa mtindo huu wa kufukuzana sijui kama SHY-ROSE BHANJI atanusurika!! Nategemea wakati wowote kusikia kuwa nae alisaidia Chadema kushinda kiti cha Kawe!! CCm ya Makamba wanavituko kweli, kwani hawakosi sababu wakitaka kumfukuza mtu.
   
 13. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #13
  Apr 7, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ni hekima kuwa na msemaji mmoja ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Zamani kulikuwa na Chuo cha viongozi wa CCM pale kigamboni, ambacho kiliweza kutoa viongozi wazuri na wenye kuelewa maadili. Itakuwa vyema kama chuo kile kitarudishwa ili kuepuka haya yatokeayo leo ndani ya CCM, tafadhali ninaomba CCM walifanyie kazi suala hili.

  Suala la Mhe. Jakaya kutembelea wizara sioni ubaya hata kidogo. Aliwateua mawaziri husika na kuwakabidhi wizara pamoja na nini cha kufanya. Ziara zake ni katika kuangalia kama maagizo aliyoyatoa yametekelezwa ama hapana. Na kama yametekelezwa ni kwa kiasi gani, na kama hayajatekelezwa kwanini?. Hili linawafanya mawaziri kuwajibika ipasavyo na wala si kulala usingizi.
  Kumbekeni Sokoine alivyokuwa anafuatilia masuala yote aliyokuwa anayatolea maagizo jinsi yalivyokuwa yanatimizwa ipasavyo na kwa muda unaotakiwa.

  Kwa wale wazazi tunaelewa kwamba hata majumbani mwetu ukiwapa watoto majukumu inakubidi kuwauliza ama kufuatilia ili kujua maagizo yako yamefanyika ama hapana na kwanini. Tuone haya kidogo kumshambulia Jakaya kwa mazuri anayoyafanya.
   
 14. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  no longer atease
   
 15. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #15
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Millya ni kibaraka wa Lowassa,hawana jipya hao zaidi ya kutumika vibaya.
  Gumbo kaza buti kwani wakati wa mafisadi kutusumbua umeisha.
  Tanzania Simama
   
Loading...