UVCCM Tabora wamwonya Mengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM Tabora wamwonya Mengi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MmasaiHalisi, May 3, 2009.

 1. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #1
  May 3, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imeandikwa na Maulid Ahmed; Tarehe: 1st May 2009

  Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Mkoa wa Tabora, wamemtaka Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, kuacha kutukana viongozi wa chama hicho na kama anataka siasa aingie kwenye chama chochote na kupambana na wanasiasa majukwaani. Sambamba na hilo, wamemtaka kuwaomba radhi wana CCM wa Tabora kwa walichadai ni kumkashifu na kumdhalilisha Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kuwa miongoni mwa mafisadi papa watano aliowataja.

  “Tunahoji nafasi yake ni nini kwenye CCM… Mengi ana historia ya kulumbana kwa kashfa na mawaziri wengi nchini, tunamtaka aache mara moja na kama anataka siasa aingie kwenye ulingo wa siasa na tutakutana naye kwenye majukwaa ya kisiasa,” alisema Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Patrick Kabaye, aliyesoma tamko la viongozi hao wa UVCCM Tabora mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam.

  Kabaye aliyefuatana na Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Tabora, Robert Kamoga na wenyeviti wa UVCCM wa wilaya zote za mkoa huo, alisema wanalaani kitendo cha Mengi kumkashifu kiongozi wao ambaye wananchi wake wana imani naye.

  “Tumefuatilia kwa karibu mwenendo wa ziara za Mengi akiwa na msafara wa wabunge, huku akitoa misaada mbalimbali na tumepata taarifa anakuja Wilaya ya Tabora, UVCCM inatoa angalizo kama misaada yake inaendana na kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu, hatutavumilia hilo, wananchi wa Tabora wana matatizo, lakini wanaheshimu utu na viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia,” alisema.

  Viongozi hao waliitaka serikali kuchunguza kauli za Mengi na kumchukulia hatua kali za kisheria ili iwe funzo na watu waheshimu utawala wa sheria. “Tunaiomba serikali iangalie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kuleta mtikisiko kwenye nchi na serikali ipige marufuku tabia hii ya Mengi kutumia umasikini wa Watanzania kupandikizia chuki watu wengine,” alisema Kabaye kwa niaba ya wenzake.

  Walisema vijana hawatakuwa tayari kuwabeba wabunge mwaka 2010 wanaoshiriki katika ziara za Mengi ambazo wameziita zinakichafua chama na serikali kupitia kivuli cha kusaidia wanyonge. Viongozi hao wameeleza kumuunga mkono Rostam na kutokuwa tayari kuona anadhalilishwa bila kuwa na ushahidi wa jambo lolote na imani ya serikali haitaruhusu tabia ya watu kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuchafua wengine.

  Rostam ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mjumbe wa NEC wa Mkoa wa Tabora na Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Igunga. Kauli hiyo ya vijana hao ni mfululizo wa watu waliopingana na Mengi tangu kutoa tamko lake la kuwataja mafisadi papa watano kati ya 10. Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na watuhumiwa wenyewe akiwamo Yusuph Manji waliodai kauli hiyo inaleta uchochezi kwa jamii na kuonyesha ubaguzi wa rangi.
   
 2. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2009
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mnanisikitisha sana vijana wa UVCCM -TABORA mnaonyesha jinsi gani upeo wenu wa kufikiri ulivyo mdogo na mko tayari kuuza nchi yenu na utu wenu kwa mafisadi kama Rostam,mnamtetea kwa kipi kikubwa alichowafanyia huko kwenu Tabora,pamoja na kutuibia mapesa yote hayo je amefanya nini huko Tabora, kwani mkoa wenu hauna maendeleo hata kidogo kielimu unashika mkia, barabara mbovu,na ndio maana hata baadhi ya watumishi wa serikali wakihamishiwa mkoa wa Tabora wanaacha kazi,leo watu ambao wanaiba mabilioni inafikia hatua serikali inashindwa kuweka miundo mbinu huko kwenu mnatetea,acheni uupuuzi
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Vita vyao hivi ,upinzani usijihusishe kabisa.
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hawa si wako mfukoni kwa RA! Ndo wanamtetea..ni mizizi ya ufisadi ndugu zangu!
   
 5. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  This is quite interesting. Cha msingi hapa ni kutambua watu wowote wenye nguvu za kiuchumi wanawatu nyuma yao. Inapotokea mapambano basi ujue ni sisi kwa sisi tutaumana.
   
 6. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Bunch of hypocrite
   
 7. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nonsense!
   
 8. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Walichotetea vijana wa Tabora, ni ile hali ya mtu kujivika upelelezi na uhakimu kwa wakati mmoja, wakati mwenyestahili ya kumhkumu mtu au raia yeyote yule ni mahakama pekee, vijana wa Tabora walichokifanya ni kumtetea kamanda wao wa vijana, Mbunge wao, MNEC wao, wao ndio wanaojua umuhimu wa RA ni kama vile vijana wa kyela walivyompokea Mwakyembe, au kama vile vijana wa kilimanjaro walivyomtetea Mengi. kila mtu ana haki ya kuamini kile anachokiamini wala si lazima imani kwa mmoja iwe ni imani ya wote! infact tunaandaa mapokezi makubwa sana kwa RA hapa Igunga yatarushwa si na TBC tu nadhani hadi CNN,SKYNEWS nk
   
 9. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  How are they getting involved in the pay roll without protecting their "SHARK" through propaganda? Wow they are bunch of Monkeys they will not be able to reflect their back until they are being discovered by somebody. Lets wait and see. By the way R.A is like king there.
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kila laheri M-bongo !
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wanyamwezi twatia aibu? Kuanzia Sitta, Kapuya, RA, Lipumba, na sasa hawa vikojozi wetu, duuuu............... Wanyantovola.....
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Namhala uleita kinehe...unakwenda na wewe kwenye mapokezi ya mjumbe wa NEC na Mbunge wa Igunga...kumpokeza kwa kuwa papa?
   
 13. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  tangazo lao ni la hatari sana kwani inaonesha wamejiandaa hata kufanya vurugu ilimuradi wabunge wanaosapoti vita dhidi ya mafisadi waanguke....
   
 14. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Sina haja ya kusome ile habari kenye thread ya kwanza lakini hiyo mijamaa ya uvccm ni mijinga mijinga haina akili kabisa. Khaa... sasa wakasome Mengi alivyo kuja na evidence juu ya shutuma za RA wajionee kwamba watu wana facts!
   
 15. k

  kosamfe Member

  #15
  May 5, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani walikurupuka, wangengoja kwanza yeye mwenyewe ajitetee kwanza. Je kama angekubali tuhuma zile wangeweka wapi nyuso zao?
   
 16. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama vijana ambao ndiyo watakuwa viongozi wa baadaye ndiyo hivi unategemea nini kwenye chama hiki cha Mafisadi! Hawa wote hakuna kitu upstairs ni bendera ufuata upepo. Kwanini wanamjibia yeye ana mdomo?
   
 17. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hamna kitu mbaya duniani kama njaa!
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Masa,

  Utashangaa kuwa hadi leo hii sijawahi hata kwenda kwenye uchaguzi wa hawa wana siasa. Ila mwakani nafikiri ntaenda maana inaonekana mambo yatabadilika sana sasa Tanzania.

  Marehemu binamu yangu aliyekuwa akifanya kazi kwa ofisi moja mkoani Tabora, alikuja na msafara wa sijui Kingunge gani mkoani. Basi kijiji chetu wakawa wamechanga vipesa vyao eti vya maendeleo ya Mkoa. Mzee Mwanafungameza akapewa kazi ya kukabidhi. Mzee akaenda na alipofika akainama kwa kuchuchumaa kama mwanamke hadi chini pale chini ya meza na kukabidhi kibahasha mtu sawa na mwanae. Baadaye binamu yangu anasema hawakufika hata Tabora mjini, wakakifungua kibahasha na kugawana hivyo vihela. Hiyo ni siku niliwachukia sana Wanasiasa.

  Wakati wanajenga uwanja wa Mpira nako walikomba sana. Kila sehemu hata ukienda kusaga Mahindi unaambiwa hela ya uwanja. Halafu leo niende kumpokea M-NEC wetu? Huyo M-NEC, sasa hivi nasikia ameanza kutengwa na mafisadi wenzie. Sasa kuna mawili au akimbizwe nje ya nchi na au abaki Wamtose na ikionekana atabwabwaja sana juu ya KAGODA, basi wata M-Kolimba huyoo kama kawaida. Achague haraka au Wam-Ballali au wam-Kolimba. Kazi anayo.
   
 19. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Kwa unyenyekevu mkubwa nakiri kusema kweli uongozi wa nchi siyo mchezo,na kwa wale waliokuwa wanafikiri ni rahisi basi waangalie malumbano haya... sijajua JK anajisikiaje kama Watu hawa wachaache wenye influence wanavyojitokeza na kuanza kuitana majina ya ajabu ajabu kukanusha kuzusha nk...Hainingii akilini Mfano: Mimi kama mkuu wa nchi nakaa kiiimya kisha wenye matarumbeta (Vyombo vya habari)wanalumbana ikiwemo tarumbeta la taifa... Mmmmhhhhh labda nina hasira za....kufungwa na Man..u...re naishia hapa...
   
  Last edited: May 6, 2009
Loading...