UVCCM: Magufuli akubalika asilimia 85

UVCCM: Magufuli akubalika asilimia 85

Ukitaka kuthibitisha hilo usitumie ushabiki nenda mtaani waulize kura watampa nani watakuambia. Leo nimekaa maeneo matatu tofauti walio weng wanasema kilichopo vichwani mwa watu sasa mikutanoni wanakwenda kwa Lowasa ila kura watampa Magufuli. Please weka ushabiki pembeni

MKUUU hakika umesema kweli, mm pia nipo na watu hapa wamevalia pamba za M4C lakin wanasema kura n kwa magufuli tu wanadai amsha amsha za chadema znawafanya waonekane wajanja mjin hapa
 
TATHMINI; siku 10 za Kampeni ya Dr John Magufuli.

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Pombe Magufuli amehitimisha mzunguko wa Kwanza wa Kampeni yake kwa mikoa 6 ya kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini ambayo ni KATAVI, RUKWA, MBEYA, NJOMBE, RUVUMA na MTWARA.

Katika kampeni zake Dr Magufuli amefanya mikutano ya hadhara takribani 49 pamoja na mikutano midogo ya kusalimia wananchi zaidi ya 126 ambapo katika mikutano yote wananchi walijitokeza kwa Maelfu kumsikiliza akiwasilisha Ilani ya CCM ya 2015-2020.

Dr Magufuli ametembea takribani Kilometa 5,900 kwa kutumia gari na maeneo mengine akitembea kwa miguu ili kukutana na Wananchi wa Makundi mbalimbali akinadi sera za CCM.

Tafiti za awali za Mashirika mbalimbali ya nje na ndani ya nchi yalionyesha kuwa CCM itashinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa zaidi ya asilimia 60, lakini baada ya kuanza kwa Kampeni na mgombea kuzunguka akifanya mikutano mikubwa ya hadhara ambayo imekuwa ikirushwa moja kwa moja (live) kupitia vituo mbalimbali vya televisheni, magazeti, redio pamoja na mitandao ya kijamii na kuwafikia watanzania takribani milioni 30, Umaarufu wa CCM na uwezekano wa kushinda umeongezeka kufikia asilimia 85 (tafiti za ndani)

Mambo yaliyopelekea CCM kuongeza umaarufu wake ni pamoja na rekodi nzuri ya uadilifu na uchapakazi aliyonayo mgombea wake, pamoja na uwezo mkubwa wa mgombea (Dr Magufuli) katika kutambua na kutoa suluhu ya matatizo yanayowakabili wananchi wa kada zote na maeneo yote ya Mijini na Vijijini.

Ilani ya CCM na namna mgombea anavyoinadi (Body language) imeongeza imani ya wananchi kwa CCM, mfano Dr Magufuli akisema anaichukia rushwa, mwili, haiba na sura yake vinaonyesha kuwa anamaanisha anachokizungumza. Ilani ya CCM imejikita katika kuleta mabadiliko kwa kuondoa Umasikini na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa Vijana, kuendeleza Vita dhidi ya Rushwa na Ubadhirifu, Kuboresha huduma za jamii na kuendeleza Umoja wa Kitaifa pamoja na kudumisha Ulinzi na usalama.

Wakati Umaarufu na kukubalika kwa CCM kunaongezeka, bado inapata upinzani hafifu ktk kampeni zake. Rekodi zenye mashaka za wagombea wao zinazohusisha kashfa za rushwa, ufisadi, utendaji mbovu na uzembe. Hali tete na migogoro ya ndani ya vyama vya Upinzani ambayo imeshika kasi ktk kipindi hiki hasa kuhusu wagombea kwa nafasi ya Urais na baadhi ya majimbo. Hali ya Afya za wagombea wao ambazo zimewafanya kutoweza kufika katika baadhi ya maeneo waliyopanga kufanya mikutano mfano Ludewa na Tunduru ambapo wananchi walishakusanyika na mgombea akashindwa kutokea. Vyama vya upinzani kukosa Ilani madhubuti na hivyo wananchi kupunguza imani yao kwao.

NB;
Katika moja ya utaratibu bora kabisa wa Chama Cha Mapinduzi ni ule wa kujifanyia tathmini katika kila hatua ya mpango ama jambo lake lolote, utaratibu huu umeiwezesha CCM kubaki kuwa relevant na kuendelea kuaminiwa na kupendwa na watanzania walio wengi.
ccm ingekuwa na uwezo wa kujitadhini ingekuwa imeshatuachia nchi yetu
 
…ule msemo wa "kujitekenya na kucheka mwenye" hapa unahusika…
 
Toa tathimini yenye ushahidi hadharani......kwamba magufuli atashinda kwa 85 percent
 
Attachments

  • uploadfromtaptalk1441449273793.jpg
    uploadfromtaptalk1441449273793.jpg
    21.2 KB · Views: 142
Thank's

mwanzo mzuri na hii mikoa ndo mikoa korofi;

sijui uwanja wa nyumbani - kanda ya ziwa na kati itakuwa 100%
 
Hivi mtu unawezaje kuandika pumba ndeeeeeefu kiasi hiki???? Hili nalo ni tatizo
 
kwa uchaguzi huu sioni kama kuna mgombea yeyote anayeweza kupata zaidi ya 60%, do not underestimate these nyumbus. Huo utafiti wa twaweza unazua mashaka.

lowasa kakimbia nyanda za juu kusini - kuzodolewa; kuna majimbo hajakanyaka , ludewa, mwakyembe, mwandosya, kambi ya wakimbizi katavi, baadhi ya majimbo kakuta watu wanashangaa

kigoma ; kapokelewa na watoto na kazomewa na kafulila.

Dar alileta mabasi kila mmbunge mabasi 6 wa ukawa na boat mbilitoka zanzibar

85% ni ndogo sana
 
mwaka huu mpaka yagonge kunako....
ukawa sio sawa na ccm
 
Chanzo cha hii habari ni kituko.
Habari hii imeandikwa na gazeti la UHURU na utafiti umefanywa na UVCCM.

Mabadilikooooooooooo
 
lowasa kakimbia nyanda za juu kusini - kuzodolewa; kuna majimbo hajakanyaka , ludewa, mwakyembe, mwandosya, kambi ya wakimbizi katavi, baadhi ya majimbo kakuta watu wanashangaa

kigoma ; kapokelewa na watoto na kazomewa na kafulila.

Dar alileta mabasi kila mmbunge mabasi 6 wa ukawa na boat mbilitoka zanzibar

85% ni ndogo sana
Nimetafuta clip ya kuzomewa kafulila nimeshindwa kuipata, waweza saidia?!
 
TATHMINI; siku 10 za Kampeni ya Dr John Magufuli.

Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Pombe Magufuli amehitimisha mzunguko wa Kwanza wa Kampeni yake kwa mikoa 6 ya kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini ambayo ni KATAVI, RUKWA, MBEYA, NJOMBE, RUVUMA na MTWARA.

Katika kampeni zake Dr Magufuli amefanya mikutano ya hadhara takribani 49 pamoja na mikutano midogo ya kusalimia wananchi zaidi ya 126 ambapo katika mikutano yote wananchi walijitokeza kwa Maelfu kumsikiliza akiwasilisha Ilani ya CCM ya 2015-2020.

Dr Magufuli ametembea takribani Kilometa 5,900 kwa kutumia gari na maeneo mengine akitembea kwa miguu ili kukutana na Wananchi wa Makundi mbalimbali akinadi sera za CCM.

Tafiti za awali za Mashirika mbalimbali ya nje na ndani ya nchi yalionyesha kuwa CCM itashinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa zaidi ya asilimia 60, lakini baada ya kuanza kwa Kampeni na mgombea kuzunguka akifanya mikutano mikubwa ya hadhara ambayo imekuwa ikirushwa moja kwa moja (live) kupitia vituo mbalimbali vya televisheni, magazeti, redio pamoja na mitandao ya kijamii na kuwafikia watanzania takribani milioni 30, Umaarufu wa CCM na uwezekano wa kushinda umeongezeka kufikia asilimia 85 (tafiti za ndani)

Mambo yaliyopelekea CCM kuongeza umaarufu wake ni pamoja na rekodi nzuri ya uadilifu na uchapakazi aliyonayo mgombea wake, pamoja na uwezo mkubwa wa mgombea (Dr Magufuli) katika kutambua na kutoa suluhu ya matatizo yanayowakabili wananchi wa kada zote na maeneo yote ya Mijini na Vijijini.

Ilani ya CCM na namna mgombea anavyoinadi (Body language) imeongeza imani ya wananchi kwa CCM, mfano Dr Magufuli akisema anaichukia rushwa, mwili, haiba na sura yake vinaonyesha kuwa anamaanisha anachokizungumza. Ilani ya CCM imejikita katika kuleta mabadiliko kwa kuondoa Umasikini na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa Vijana, kuendeleza Vita dhidi ya Rushwa na Ubadhirifu, Kuboresha huduma za jamii na kuendeleza Umoja wa Kitaifa pamoja na kudumisha Ulinzi na usalama.

Wakati Umaarufu na kukubalika kwa CCM kunaongezeka, bado inapata upinzani hafifu ktk kampeni zake. Rekodi zenye mashaka za wagombea wao zinazohusisha kashfa za rushwa, ufisadi, utendaji mbovu na uzembe. Hali tete na migogoro ya ndani ya vyama vya Upinzani ambayo imeshika kasi ktk kipindi hiki hasa kuhusu wagombea kwa nafasi ya Urais na baadhi ya majimbo. Hali ya Afya za wagombea wao ambazo zimewafanya kutoweza kufika katika baadhi ya maeneo waliyopanga kufanya mikutano mfano Ludewa na Tunduru ambapo wananchi walishakusanyika na mgombea akashindwa kutokea. Vyama vya upinzani kukosa Ilani madhubuti na hivyo wananchi kupunguza imani yao kwao.

NB;
Katika moja ya utaratibu bora kabisa wa Chama Cha Mapinduzi ni ule wa kujifanyia tathmini katika kila hatua ya mpango ama jambo lake lolote, utaratibu huu umeiwezesha CCM kubaki kuwa relevant na kuendelea kuaminiwa na kupendwa na watanzania walio wengi.

Lile neno maarufu la kujitekenya na kucheka mwenyewe ndo limedhihirika. make katika utafiti uwezi Fanya tafiti za kukubalika kwenye mkutano ambao wengi wa waloudhuria either ni wafwasi tu wa chama or ni waoga kusema ukweli wao kutokana na attention iliyopo pale .hivyo kama ndo utafiti wenu ni sawasawa na kusema nampenda mimi wakati hata usiposema ni kawaida mtu kujipenda.
 
Ukisema wananchi wa kundi la uvccm, ni kweri anakubalika hivyo, ila kwa wananchi wa kawaida ni kinyume chake.
 
MKUUU hakika umesema kweli, mm pia nipo na watu hapa wamevalia pamba za M4C lakin wanasema kura n kwa magufuli tu wanadai amsha amsha za chadema znawafanya waonekane wajanja mjin hapa

Hata walioandamana juzi walikuwa wamevaa jezi za M4C lakini mwisho wasiku kumbe Masabuli at work.
 
nimetafuta clip ya kuzomewa kafulila nimeshindwa kuipata, waweza saidia?!

mbona za kumwaga toka facebook

angali jamii
uchaguzi ; zipo kibao
 
Back
Top Bottom